Tuna mahakama maalum ya mafisadi, tuna ufisadi lakini hatuna mafisadi wa kuwashtaki

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,294
Hii ndio Tanzania.

Mwaka 2015 wakati wa uchaguzi mkuu mgombea urais wa CCM Magufuli alitoa ahadi ya kuanzisha mahakama maalum ya kushughulikia ufisadi. Baada ya kushinda uchaguzi aliitimiza ahadi hiyo na kuianzisha hiyo mahakama.

Watanzania tuliamini kwa kuwa kuna mahakama maalumu ya mafisadi suala la ufisadi kama sio kumalizika basi litapungua kwa kiasi kikubwa. Matokeo yake yamekuwa kinyume na matarajio ya watanzania kwani kasi ya ufisadi imeongezeka kila sekta lakini hatuoni mafisadi kukamatwa hali ambayo hata uwepo wa hiyo mahakama hauna maana tena.

Watendaji wa serikali na mashirika na taasisi za umma wamekuwa wapigaji wakubwa wa fedha za serikali na vyombo vya umma vya kupambana na huo ufisadi vipo lakini hakuna juhudi zozote za kukomesha au kupunguza ufisadi huo. Report ya CAG imetoka na ufisadi mkubwa wa matrilioni ya shillingi lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kwa waliotajwa ktatika report ya CAG.

Kutokana na hali hiyo ni wazi kuwa ile mahakama haina sababu ya kuwepo kama mafisadi hawapo.

kigogo200014_168167265020969.jpg
geraldhando_1680756005605831.jpg
JamiiForums-671446292.jpg
mwananchi_official_1680809993051833.jpg
mwananchi_official_1680881942184440.jpg
 
Mkuu Tanzania wapo mafisadi maalum ambao hawawezi kushtakiwa kutokana mfumo uliopo. Ndiyo maana utasizikia kauli kuwa watu fulani wakiguswa nchi itatikisika.
 
Katika vitu vinavyomdhalilisha Harisson Mwakyembe aliyekuwa Waziri wa Sheria na Katiba kwenye Baraza la kwanza la mawaziri la Magufuli ni kutomshauri vizuri Bosi wake kuhusu kutohitajika kwa Mahakama hii.

Hii Mahakama haikupaswa kuwapo kwa vile mfumo uliopo wa Mahakama unakidhi haja ya kila kosa la jinai
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom