Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 876
- 4,101
Magufuli aliamini mapambano dhidi ya rushwa ni kuunda mahakama maalum. Lakini alisahau kwamba wala rushwa na watoa rushwa ni watawala na siyo wananchi. Wakati anatawala watawala waliokuwa wanapelekwa mahakama ya mafisadi ni wale waliokinzana kimtazamo na yeye na utawala wake.
Kwa bahati mbaya baadhi ya mafisadi walioundiwa mahakama walikuwa viongozi wa Mahakama. Kwa kuwa mahakama hiyo haikulenga kupambana na rushwa bali kupambana na wapinzani wa serikali rushwa ilizidi kuwepo na inaendelea kuwepo.
Kwa sasa baada ya utawala wa JPM tulitegemea mafisadi wafikishwe mahakama yao lakini tumeona ukimya wa mahakama hiyo kwa mwaka 2023. Hizi ni tafsiri kwamba muda na uhai wa mahakama hii umeisha hadi pale wanasiasa watakapokorofishana. Wasipokorogishana kifisadi mahakama itakwenda likizo kama ambavyo leo hii tunaona ipo likizo.
Swali, wanaofanya kazi katika mahakama hiyo wanafanya kazi gani? Kwanini wasipangiwe vituo vingine vya kazi? Yale majengo wanaweza wakapewa hata hospitali ya Sinza kupanua huduma za afya.