Kwani Rais Magufuli alitoa ratiba ya kuwapeleka mafisadi mahakamani?

Wapiga zumari wa CCM humu JF tumeshawachoka.Mnapelekwaga tu na upepo utakapo amua wenyewe.
 
HIYO TRACK YENU YA NYUMBA ZA SERIKALI HAIICHUJI TU KWENU , NADHANI MAPAKA SASA UNGEKUA USHAITOA KAMA UNGEKUA UMEMSIKILIZA MWENYEKITI WENU WA CHAMA KANDA YA PWANI ALISHALIELEZA HILO VIZURI TU, AU MWENZETU KIZIWI

Hahaha ....hii video inatembea ile mbaya ...Kila swali juu ya ufisadi Chadema hawana haja ya kuuliza ....wanayo majibu mazuri sana na watoa majibu wako huko huko ....
 
Ulikuwa upande wake wakati wanasema pesa ni za umma?
Au unahoroja tu kufuata upepo unavovuma?
Tafuta posts zangu humu utanielewa....Sijawahi kukaa upande mmoja na mafisadi.

Na Bado ...ule ufisadi wa Ranchi za ufugaji za Taifa.
 
Kweli Magu hatabirikj,sitoshangaa na yeye akipandishwa kizimbani kwa kuuza nyumba za serikali,kununua meli mbovu na kuliingiza taifa hasara.
Tusubiri tutaona na kusikia mengi.
Nyumba serikali kwanini msimuulize kamanda Sumaye, Ninyi ni majasiri na magwiji wa unafiki. Hamna aibu kabisa
 
Muda utaongea...
Kweli nimeamini kuujua ukweli hakumaanishi uwe msomi unaweza kuwa msomi usiweze kuujua au kung'amua ukweli.bado na wasiwasi sana na watu ambao nahisi mna elimu kichwani afu still mnamuelewa huyu mkuu.

Amakweli sijui nimahaba sijui nini? Huwezi ukawa unajua kabisa watu wangu wanauawa na mamba afu wewe unaenda una ua kenge afu una wa aminisha unatatua tatizo.

Jamani kama kweli mkuu kaona wananchi wake tuna uawa na mamba yanini kuua kenge nakutuambia tuvuke mto pako salama? Basi mi nasema tangulieni mvuke vipofu ila mimi nilie na macho atakuyagusa maji ya mto utaniua.
 
Kuna ile sentensi aliyowahi kusema "kuna watanzania wenzetu walikuwa wanaishi kama malaika, sasa wataishi kama.........." ngoja niendelee kuangalia yajayo
 
HIYO TRACK YENU YA NYUMBA ZA SERIKALI HAIICHUJI TU KWENU , NADHANI MAPAKA SASA UNGEKUA USHAITOA KAMA UNGEKUA UMEMSIKILIZA MWENYEKITI WENU WA CHAMA KANDA YA PWANI ALISHALIELEZA HILO VIZURI TU, AU MWENZETU KIZIWI


Track yangu na nani? Kwavile kauza nyumba za serikali haturuhusiwi kuoji?
 
Mwizi ni mwizi tuu ata awe Mbogwe au tundulisu.ila tunachotaka haki itendeke sio kuzugazuga hapa binafsi kinachofanyika sija kikubali.ivi umemuona mwizi wako afu unamuachatu anadunda kitaa eti stahikiwa!!

Aibu iliyoje hii acheni kusifia ujinga nakuleta uzandiki.kwanini kina rugemalila wamefikshwa mahakamani faster kuliko wale mawaziri wa makinikia?tusihoji?nahasila mimi basi tuu kwanza wengine ndugu zetu walifukiwa mashimoni bulyanhulu wakiwa hai.tena mnyamaze kabisa kama hamna pointi za maana sio kuleta upuuzi hapa.
 
Nazungumzia ratiba ya kuwapeleka mafisadi kwenye mahakama ya mafisadi na kuwafungulia mashitaka.

Inawezekana labda aliwahi kuitoa au kuitaja hiyo ratiba lakini mimi ama sikuiona au sikuisikia.

Hivyo, ndo maana nauliza hapa. Kama kuna anayejua nitamshukuru akitufahamisha sie tusiojua.

Aliwahi kuahidi kuwa fulani na fulani atawapeleka kwenye hiyo mahakama na atawapeleka lini?

Kikubwa kilichonifanya niulize ni kile kilichotokea jana kwa wale watu wawili [Harbinder Sing na James Rugemalira] kukamatwa na kupelekwa mahakamani kujibu tuhuma dhidi yao.

Inavyoelekea watu walio wengi hawakuwa wakitegemea kuwa hao jamaa wangekamatwa hiyo jana.

Na ndo maana kitendo cha wao kukamatwa kimepokelewa kwa mshangao, furaha, na wasiwasi.

Sasa, kuna wale ambao wanahoji kuwa kama Lowassa ni fisadi kwa nini hapandishwi kizimbani.

Ndo nami swali linalonijia ni hilo kwenye kichwa cha mada.

Sijui labda watu walitaka kumwona yeye akiwa wa kwanza kupandishwa kizimbani kujibu hizo tuhuma dhidi yake au sijui wanataka kuona kila siku kuna mtu mpya anapandishwa kizimbani!

Muhula wa huyu Ngosha ni bado sana kuisha. Bado ana zaidi ya miaka miwili ndipo amalize muhula wake wa kwanza.

Tayari keshaonyesha kuwa ni mtu ambaye hatabiriki kirahisi wakati mwingine. Hivyo msije shangaa siku moja mnaamka na kumwona [Lowassa] akiwa 'perp walked' nje ya mahakama ya Kisutu.

Hapo naweza hata kutabiri kuwa wengi wenu mnaohoji kwa nini kama yeye ni fisadi hapandishwi kizimbani, mtabadili magoli na si ajabu mkasema kuwa anaonewa kwa sababu za kisiasa.

Vita dhidi ya ufisadi ni vita ndefu na ni endelevu. Mnapokuwa vitani kamanda hawezi ku-telegraph mipango na matendo yake kwani kufanya hivyo kunaweza kumnufaisha adui na akajipanga vizuri ili akushinde.

Siku ya siku ikifika msije kusema sikuwaambia....na msije kulia na kuhamisha magoli hapa!
Hayo mambo sio kipaumbele cha wananchi, tunahitaji na tunasisitiza noah zetu.
 
Hahaha ....hii video inatembea ile mbaya ...Kila swali juu ya ufisadi Chadema hawana haja ya kuuliza ....wanayo majibu mazuri sana na watoa majibu wako huko huko ....

Kwamba Chadema ndiyo walikwapua nyumba za serikali chini ya usimamizi wa Magufuli? Huyo jamaa kwenye video mbona kavaa uniform za kijani? Jenerali Ulimwengu anasema ule wala sio ufisadi bali ni jeuri. Kwamba watu wachache waliamua kugawana nyumba na viwanja vya serikali huku wakitamba kwani mtatufanya nini. Ushabiki hautasaidia na kushabikia kunafanya kiongozi aonekane kana kwamba anapendelea. Mtu akituhumiwa na kufanya makosa, anapaswa kufikishwa mahakamani - bila kujali dini, chama, au kabila la mtuhumiwa. Tabia ya kutumia kesi kisiasa ni tabia ya kishenzi - kwamba watuhumiwa wamefikishwa mahakamani hivyo chama au kabila flani mtaisoma 2. Mwizi ni mwizi hata akiwa JPM anapaswa kuwajibika.

Ni tishio kwa utawala bora kumsifu Rais pale ambapo mtuhumiwa wa wizi anafikishwa mahakamani. Hiyo maana yake ni kwamba watakaofikishwa mahakamani ni wale ambao Rais ametaka wafikishwe mahakamani. Ukiiba na kama Rais hataki ufikishwe mahakamani, hutafikishwa mahakamani. Hatuwezi kushangilia hali hii. Wachunguzi wa makosa ya jinai, uhujumu uchumi, na waendesha mashtaka wanapaswa kuwa na uhuru zaidi - uhuru wa kufanya kazi bila kuingiliwa au kupokea amri kutoka kwa Rais. Kilichofanya kina Rugemalila na Seth wasichunguzwe na kushtakiwa muda wote huo ni kwa kuwa mamlaka za uchunguzi na kuendesha mashtaka si huru. Tunafanya makosa makubwa kushangilia pale ambapo kuna kila dalili kuwa watu wenye madaraka wanaendelea kuingilia uhuru wa mamlaka za uchunguzi na waendesha mashtaka. Hatupaswi kusema JPM si wa mchezo, ona Rugemalila na Seth wamefikishwa mahakamani. Tunapaswa kusema TAKUKURU, Police, Usalama wa Taifa, na Waendesha mashtaka wa Serikali ni moto wa kuotea mbali, ukijihusisha na rushwa na rushwa huchomoki, hata kama mhusika ni mke wa Rais. Natamani tuwe na waendesha mashtaka kama wale wa Scorpions ya SA: Scorpions (South Africa) - Wikipedia - ambao hata JPM ashiriki matukio ya rushwa, hawatapepesa macho na kumumunya maneno - watamchunguza na kuweka mambo hadharani.
 
Lowassa anawaumiza vichwa sana, mbona alikwishasema kuwa yeye alikuwa anatekeleza amri kutoka juu, juu yake kulikuwa na makamu wa raisi na raisi
Sasa siku wakimkamata Lowassa na akatoa ushahidi wa maagizo toka kwa mkubwa wake sijui mahakama itaamua nini na wakati tumeshasema tusiwasumbue wazee wetu.
 
Mkuu Ngabu, kuna report ya TICTS bado haijatoka, ila ipo kwenye michakato ya mwisho mwisho.

Kama ulivyosema mwishoni mwa andiko, watu wanaweza kabisa kuhamisha goli na kuanza kuongea maongezi ya kutia huruma.
 
Back
Top Bottom