Kwani ni lazima serikali iingilie sekta binafsi ya Mafuta?

Ifike sehemu DOLA ijue kuwa USALAMA WA TAIFA hii ndiyo maana yake.Sitaki kuamini kuw DOLA NA WALINZI WA NCHI hawajui nani anacheza mchezo huu.NI VYEMA KUWATAFUTA NYUMBA HATA NYUMBA HATA KAMA YUKO ULAYA ALIYE NA WAJIBU ATAFUTWE,WASHUGHULIKIWE ILI IWE FUNDISHO.

NA MFUMO UONDOE WATU WOTE OVYO OVYO.

ILA ISIJE KUWA UPANDE MWINGINE NI MCHEZO WA KUIGIZA MANAKE WATANZANIA WALIVYOGEUZWA NI JUKWAA LA MAJARIBIO WATU WATAPIGA KELELE KIDUMU CHAMA OYEEEEEEEEEEEE.

NITAAMINI SIO MAIGIZO KWA KUONA KUWA WALE WOTE WALIOCHEZA DRAMA HIYO, WAKIFIKISHA MAHAKAMANI KWA KUHATARISHA USALAMA WA NCHI KIASI KUWA BUNGE KUFANYA NI HATI YA DHARURA BUNGENI.

FIKILIA, TAFAKARI NA KISHA CHUKUA HATUA.

kanuni ya demand na supply inafanya kazi kwenye free market lakini kilichotokea katika soko la mafuta ni wafanyabiashara wameunda catel yani ushirika wa kudhibiti bei na sheria za tume ya ushindani inaipa nguvu serikali kuingilia inapoamini kuna nanma yeyote ya umoja wa wafanyabiashara kudhibiti bei

katika suala la upungufu wa mafuta linatokana na sababu mbili kubwa sasa.

1. kiburi cha wafanyabiashara dhidi ya serikali kwani wanaamini kuwa serikali lazima isalimu amri na haina nguvu na uwezo wa kuwadhibiti

2.kutokana na kushuka kwa bei watumiaji wengi hawaamini kuwa bei itaendelea kubaki chini na wanadhani kuwa ni wakati mfupi tu itabaki kwenye bei hii na ndio maana wamenunua na kuweka stock yao kwa siku za karibuni kwa niliweza kuzungumza na mkandarasi wa barabara anayetarajia kufanya kazi zake muda wa karibuni yeye ameweza kununua zaidi ya lita 700,000 za diesel na kuziweka akiba kwa ajili ya mitambo yake ili pia linaongeza upungufu wa mafuta

imefika wakati ambao serikali haiwezi kukwepa kuunda mfumo wa upatikanaji wa mafuta wa uhakika kwani katika nchi ambayo umeme ni shida na mafuta nayo yakiwa shida basi lazima ife

serikali lazima ifikirie kufufua kiwanda cha kusafisha mafuta cha tipper ili kupunguza bei za mafuta na kuongeza ajira kwa vijana wetu la sivyo haitaweza kusalimika kutoka katika janga la mfumuko wa bei na usalama wake yenyewe

Ni kweli mkuu,kwenye biashara huria ni kosa kwa wafanyabiashara kupanga bei kwa pamoja, ukishafanya hivyo lazima vyombo vya udhibiti viweze kuingilia kati kwani mlaji ataumizwa. tatizo ni timing ya kuchukua hatua, hawa wafanyabiashara hili wamelifanya mara nyingi mno lakini vyombo husika vilikuwa usingizini-wanakuja kushtuka wakati watu wamejijengea nguvu kubwa ambazo zinahitajika pia nguvu kubwa ili kuwadhibiti, na kwa serekali yetu hii tuliyonayo sidhani kama wana uwezo huo, ni sisi walaji tutakaoendelea kuumia

Wananchi wanalalimika kuwa kuna tatizo la mafuta; wafanyabiashara wanasema hawana mafuta, serikali inasema wafanyabiashara wapunguze bei n.k Nimebaki najiuliza kuna uhusiano gani kati ya upungufu wa mafuta jijini na utawala uliopo madarakani? Kwanini tatizo la upungufu wa mafuta halikutokea kwa mfano wakati mmomonyoko wa uchumi duniani umeiva? Kwanini liwe ni tatizo ambalo linaonekana kuhusiana na bei zaidi au ni kweli ugavi wa mafuta ni mdogo hivyo?

Lakini upande mwingine inabidi ujiulize kwenye nchi inayofuata "uchumi wa soko" kwanini serikali ipange bei ya mafuta badala ya kuacha soko liamue kiasi gani kiingizwe na kwa bei gani kumeet demand?

Je Serikali haina reserve ya mafuta kwa ajili ya hali kama hii? Kwa mfano kama tungekuwa tunaenda vitani leo hii tungeweza kuwa na mafuta ya kutosha kuhudumia vikosi vyetu?

Lakini swali linalosumbua mimi kama wengine vile vile je is the a genuine shortage of oil or an artificial one? Kama ni genunie, kwanini serikali basi inafikiria kwa kulazimisha watu washushe bei ndio mafuta yataongezeka? Kwanini serikali isiseme wafanyabiashara wauze katika bei ya awali tuone kama mafuta yatatokea - maana kama mafuta yanatokea bei ikiwa juu na hayapo bei ikiwa chini maana yake ni kuwa kuna mtu anafanya "hoarding"? ni muhimu kujua wapi na kina nani?

Upande mwingine, kama wenye vituo vya mafuta hawataki kuagiza mafuta katika bei ya hasara serikali inaweza vipi kuwalazimisha kuagiza mafuta bila kuonekana inaingilia "sekta binafsi"?

Nadhani haujui Tanzania inatumia mfumo gani wa uchumi..serikali ya Tanzania inatumia mfumo wa "mixed economy" kwa maana ina2mia capitalist economy/market economy ambapo supply n demand ndo zinaweka bei bila ya serikali kuingia lakin kwa wakati huo huo serikali ina2mia socialism kwa maana ya kuingilia bei pale inapoona wananchi wanaumizwa,nadhan nimejibu swali lako la kwann serikali imeingilia.

Wananchi wanalalimika kuwa kuna tatizo la mafuta; wafanyabiashara wanasema hawana mafuta, serikali inasema wafanyabiashara wapunguze bei n.k Nimebaki najiuliza kuna uhusiano gani kati ya upungufu wa mafuta jijini na utawala uliopo madarakani? Kwanini tatizo la upungufu wa mafuta halikutokea kwa mfano wakati mmomonyoko wa uchumi duniani umeiva? Kwanini liwe ni tatizo ambalo linaonekana kuhusiana na bei zaidi au ni kweli ugavi wa mafuta ni mdogo hivyo?

Lakini upande mwingine inabidi ujiulize kwenye nchi inayofuata "uchumi wa soko" kwanini serikali ipange bei ya mafuta badala ya kuacha soko liamue kiasi gani kiingizwe na kwa bei gani kumeet demand?

Je Serikali haina reserve ya mafuta kwa ajili ya hali kama hii? Kwa mfano kama tungekuwa tunaenda vitani leo hii tungeweza kuwa na mafuta ya kutosha kuhudumia vikosi vyetu?

Lakini swali linalosumbua mimi kama wengine vile vile je is the a genuine shortage of oil or an artificial one? Kama ni genunie, kwanini serikali basi inafikiria kwa kulazimisha watu washushe bei ndio mafuta yataongezeka? Kwanini serikali isiseme wafanyabiashara wauze katika bei ya awali tuone kama mafuta yatatokea - maana kama mafuta yanatokea bei ikiwa juu na hayapo bei ikiwa chini maana yake ni kuwa kuna mtu anafanya "hoarding"? ni muhimu kujua wapi na kina nani?

Upande mwingine, kama wenye vituo vya mafuta hawataki kuagiza mafuta katika bei ya hasara serikali inaweza vipi kuwalazimisha kuagiza mafuta bila kuonekana inaingilia "sekta binafsi"?

1. Serikali yetu kingilia sekta binafsi, ni kinyume na misingi ya biashara huria.

2. Serikali yetu kuingilia sekta binafsi unwarranted wakati ambapo inaendesha ubinafsishaji, ni kuchanganya watu, pamoja na kuwapa wawekezaji wakati mgumu kuielewa inaposimama.

3. Serikali haitakiwi kukurupuka kwa sababu tu CC ya CCMs NEC imetoa tamko bei ya mafuta ipunguzwe, tamko ambalo linaweza kuwa limetokana na sababu za political populism zaidi kuliko uchumi sound.

Kwa upande mwingine

1. Searikali ina wajibu wa kuhakikisha bei ya mafuta inafuata nguvu za kweli za "supply and demand" na wafanyabiashara hawapangi bei kwa kutumia monopoly/ oligopoly cartels.

Kwa kuwa serikali imeingilia nguvu za soko zinazopanga bei, inaweza kuhalalisha move hii kwa kuonyesha kwamba kulikuwa na pricefixing? Kama inaweza kutuonyesha hivyo, hatua gani zinachukuliwa kwa wahusika?

Kama hakuna price fixing, kwa nini serikali inaingilia biashara huria?

Wananchi wanalalimika kuwa kuna tatizo la mafuta; wafanyabiashara wanasema hawana mafuta, serikali inasema wafanyabiashara wapunguze bei n.k Nimebaki najiuliza kuna uhusiano gani kati ya upungufu wa mafuta jijini na utawala uliopo madarakani? Kwanini tatizo la upungufu wa mafuta halikutokea kwa mfano wakati mmomonyoko wa uchumi duniani umeiva? Kwanini liwe ni tatizo ambalo linaonekana kuhusiana na bei zaidi au ni kweli ugavi wa mafuta ni mdogo hivyo?

Lakini upande mwingine inabidi ujiulize kwenye nchi inayofuata "uchumi wa soko" kwanini serikali ipange bei ya mafuta badala ya kuacha soko liamue kiasi gani kiingizwe na kwa bei gani kumeet demand?

Je Serikali haina reserve ya mafuta kwa ajili ya hali kama hii? Kwa mfano kama tungekuwa tunaenda vitani leo hii tungeweza kuwa na mafuta ya kutosha kuhudumia vikosi vyetu?

Lakini swali linalosumbua mimi kama wengine vile vile je is the a genuine shortage of oil or an artificial one? Kama ni genunie, kwanini serikali basi inafikiria kwa kulazimisha watu washushe bei ndio mafuta yataongezeka? Kwanini serikali isiseme wafanyabiashara wauze katika bei ya awali tuone kama mafuta yatatokea - maana kama mafuta yanatokea bei ikiwa juu na hayapo bei ikiwa chini maana yake ni kuwa kuna mtu anafanya "hoarding"? ni muhimu kujua wapi na kina nani?

Upande mwingine, kama wenye vituo vya mafuta hawataki kuagiza mafuta katika bei ya hasara serikali inaweza vipi kuwalazimisha kuagiza mafuta bila kuonekana inaingilia "sekta binafsi"?

Mkuu MM,
Ni kweli mafuta kisheria yanatakiwa bei zipangwe na nguvu ya soko, na kwa TZ ilikuwa hivo EWURA alikuwa mtoa leseni na msimamizi tu mpaka nadhani mwaka 2009 alikuja kugundulika kuwa wafanyabiashara wa mafuta hasa wale waagizaji ni wachache mno na kwa taarifa yako hawafiki 10, na hao ilibainika kuwa wana chama chao na wanapanga bei watakavyo. So EWURA ikabidi kuingilia kati maana ni kinyume na maadili ya soko huru kwa wao kupanga bei kwa siri. So EWURA ikapewa mamlaka ya kutoa bei "Elekezi", yahani EWURA inatoa bei ya chini na ya juu ili washindade in between. So mafuta yalitakiwa iwe purely driven by mrkt forces but sellers violeted the rules and EWURA as it is for any Gov was right to interven.

Free Market, Mkuu...

Hakuna nchi ambayo ilifanikiwa kwa kupanga bei, inabidi demand na supply ndio ipange bei.., Nchi nyingi ziligundua hili at a high cost.... Serikali inachoweza kufanya ni kuhakikisha competition inaongezeka na hawa matajiri hawakai pamoja na kupanga bei

Hii ni kutaka kuhalalisha matakwa ya kisiasa katika biashara za watu binafsi.
nafikiri angalieni sheria zenu zinanenaje. hakuna mfanyabiashara aliye tayari kupata hasara kwa sababu za kisiasa.

Mkuu MM,
Ni kweli mafuta kisheria yanatakiwa bei zipangwe na nguvu ya soko, na kwa TZ ilikuwa hivo EWURA alikuwa mtoa leseni na msimamizi tu mpaka nadhani mwaka 2009 alikuja kugundulika kuwa wafanyabiashara wa mafuta hasa wale waagizaji ni wachache mno na kwa taarifa yako hawafiki 10, na hao ilibainika kuwa wana chama chao na wanapanga bei watakavyo. So EWURA ikabidi kuingilia kati maana ni kinyume na maadili ya soko huru kwa wao kupanga bei kwa siri. So EWURA ikapewa mamlaka ya kutoa bei "Elekezi", yahani EWURA inatoa bei ya chini na ya juu ili washindade in between. So mafuta yalitakiwa iwe purely driven by mrkt forces but sellers violeted the rules and EWURA as it is for any Gov was right to interven.

Ndiyo tatizo la kuwa na serikali iliyo "paper tiger". Sasa penalty ukibainika wewe mfanyabiashara uko katika a price fixing oligopoly cartel ni nini?

Na nani kashachukuliwa hatua mpaka leo?

MM.
Kuna vitu viwili hapa.
1. Mafuta yapo ila wafanyabiashara hawataki kuuza sababu serikali imewapangia bei.
tofauti ya maelekezo ya bei ya sasa na yale tuliyoyazoea ni kwamba, kwa kawaida
Ewura upanga bei za mafuta kwa majibu wa mamlaka waliyonayo (naamini huwa
wanaifanya kazi yao vyema) lakini sasa kuna maelekezo maalumu kutoka kwenye
uongozi wa chama cha Mapinduzi, haya ndio yaliyoleta sokomoko

Maelekezo ya CCM yanaashiria kwamba yameingilia mfumo wa upangaji bei katika
namna isiyo ya kawaida, na hapa wananchi tunabaki njia panda kama mfumo wa
kawaida huwa una maslahi kwa watanzania au la!!

Lakini huu ni ushahidi kwamba kwa namna serikali hii ilivyoisha changanya mambo,
sasa haina namna yoyote inaweza ikawaridhisha watanzania, katika namna yoyote
ile serikali itakapojaribu kuleta unafuu kwa watanzania inalazimika kuvunja makubaliano
ya siri, yasiyorasmi, yakifisadi ambayo imekuwa ikiyasimamia kwa muba mrefu kwa kushirikiana
na wafanyabiashara.

Wote tunafahamu kwamba serikali inawafahamu wafanyabiashara ambao uchakachua mafuta,
haijawahi kuwachukulia hatua hata mara moja, majuzi imepandisha kodi ya mafuta ya taa
kama vile haielewi madhara yake kwa wananchi ambao ndio watumiaji wakubwa wa mafuta ya taa.
Hii inaitwa double edged sword.

Tukianzia kwenye maamuzi rasmi ya kupandisha kodi/bei ya mafuta, sababu hapa ndio mwanzo wa matatizo
yote. Kupanda kwa bei ya mafuta ya taa hakuwalipi kabisa wafanyabiashara wa petrol/diesel, hawawezi kuchakachua
kwa faida, hivyo wanalazimika kuuza unchakachured petrol/diesel, maana yake ni kwamba kama with chakachuring
walikuwa wakiuza lita 1000 kama petrol badala ya lita 700, sasa wanalazimia kuuza lita 1000 kama lita 1000 za petrol,
bei lazima ipande, hivyo inawezekana kabisa kwamba bei ya mafuta iliyo sokoni sasa ndio bei halisi na ya ukweli,

2. Mafuta hayapo nchini kabisa.
Hili linahitaji takwimu za ukweli, lakini taarifa nilizonazo ni kwamba, malawi kuna upungufu wa mafuta
kwa kiwango ambacho kama wakisikia malalamiko yetu wanaweza kutuona ni watu tusionashukrani.

Riz1 Mwenyewe ni mfanya biashara wa mafuta. Unategemea serikali itamfanya nini wakati yeye mwenyewe ndiye serikali? Hao kina Masebu wanapoteza muda kama ma-house boy tu!

KAMPUNI ya Commercial Petroleum (COPEC) ambayo imepewa leseni na Serikali kuagiza bidhaa ya petroli, imeahidi kuingiza nchini shehena yake ya kwanza ya mafuta mwishoni mwa mwezi ujao.

Tayari kampuni hiyo tanzu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imetangaza zabuni ikialika wafanyabiashara ambao wako tayari kusambaza bidhaa itakayoagizwa nayo.

Copec ilipewa leseni juzi na Serikali baada ya waagizaji binafsi wa petroli kugoma kutokana na Serikali kutangaza bei elekezi chini ya waliyokuwa wanauzia.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Selengia Mlawi, aliliambia gazeti hili jana, kuwa Serikali imekubali kuipa kampuni hiyo dola milioni 38 za Marekani, kwa ajili ya kuagizia shehena yake ya kwanza.

Imetoa fedha hizo kutokana na dharura iliyopo, baada ya wafanyabiashara binafsi kugoma kusambaza mafuta hayo.

TPDC ilikiri kuwa kwenye mipango yake, suala hilo halikuwamo na ndiyo maana Serikali ikaamua kutoa kiasi hicho cha fedha, ambacho kinatosha kununulia, kusafirishia na kulipia bima shehena yake ya kwanza.

Lengo la Serikali kuruhusu kampuni hiyo inayomilikiwa kwa asilimia 100 na TPDC kujiingiza kwenye biashara ya ushindani, ni kujaribu kupata taarifa sahihi na za uhakika kuhusu uagizaji wa bidhaa hiyo, kutokana na wafanyabiashara binafsi kulalamika kuwa wanapata hasara.

Lingine, ni kuhakikisha kinakuwapo chombo cha uhakika ambacho hakiwezi kupinga wala kutofautiana na maagizo ya Serikali, kama walivyofanya waagizaji binafsi, hadi wakagoma kusambaza bidhaa ya petroli na hivyo kuiingiza nchi kwenye janga la uhaba wa mafuta.

Serikali ina ubia na kampuni ya BP kwa asilimia 50, lakini kampuni hiyo ndiyo inaonekana kushikilia msimamo wa kuendelea na mgomo licha ya agizo la Serikali kukataza mgomo huo.

Hata hivyo, COPEC imeingizwa kwenye biashara hiyo wakati haina watendaji wala bodi, jambo ambalo limeifanya TPDC katika kipindi cha mpito, kuchukua majukumu makubwa ambayo yangeendeshwa na bodi na menejimenti ya Copec.

"Ni kweli, kwa sasa kampuni haina watendaji, kikao cha Bodi cha TPDC kilikaa juzi (Jumanne) na kuamuru wafanyakazi walioko kwenye kitengo cha masoko cha TPDC waendeshe shughuli za kampuni hiyo wakati menejimenti yake ikitafutwa," alisema Mlawi.

Mlawi alisema pia kwamba Bodi ya TPDC chini ya uenyekiti wa Jenerali (mstaafu) Robert Mboma, ndiyo itakayounda bodi ya COPEC na ilikubaliwa kuwa baadhi ya wajumbe wa Bodi ya TPDC waingie kwenye bodi hiyo, ili kuipa uhai na kasi ya kuendesha biashara hiyo.

Ndiyo maana hata tangazo la jana la kukaribisha zabuni ya kusambaza shehena ya COPEC lilitolewa na Bodi ya TPDC kwa niaba ya mpuni hiyo.

Katika tangazo hilo, zabuni inawataka wenye sifa za kusambaza tani 9,000 za petroli, 25,000 za dizeli na tani 1,000 za mafuta ya taa. Mwisho wa kuomba zabuni hiyo ni Septemba 12.

"Shehena ya kwanza kuwasili nchini haitazidi mwisho wa Septemba, hivi sasa tunajiandaa kupeleka zabuni kwenye kampuni kubwa ili zituuzie mafuta kwa bei ndogo zaidi kuliko kununua mafuta kutoka meli zinazoelea baharini.

"Sisi tunaingia kwenye mfumo wa zabuni, si kuagiza kwenye kampuni mama kama wanavyofanya BP na Engen, ambao wanapewa bei kabisa na ndiyo maana inakuwa vigumu kwao kubadilisha bei, kwani ni lazima wapate kibali cha kampuni hizo mama," alisema Mlawi.

Akifafanua kuhusu wafanyakazi, alisema TPDC tangu mwaka 2006 imekuwa na wafanyakazi wenye ujuzi wa hali ya juu katika sekta ya mafuta, kwani tayari Serikali iliwaomba kufanya biashara hiyo na baadaye wakasimamisha suala hilo.

"Tayari tulishaajiri wataalamu kutoka kampuni za mafuta … na uhakikishia kuwa hilo halina shida kwa vile tunao wa kutosha katika kitengo cha masoko," alisema Kaimu Mkurugenzi huyo.

Maghala Mlawi alikiri kuwa kwa sasa hawana maghala ya kuhifadhia shehena watakayoagiza lakini akasema biashara ya mafuta inaruhusu kampuni kutumia maghala ya kampuni nyingine.

"Kwa kipindi hiki ambacho hatuna maghala, tutaomba kampuni nyingine, kwani sheria inaruhusu kampuni shindani kutupa maghala hayo hata kama tuna ugomvi nao. Kwa hivyo hatuna tatizo na suala hilo," alisema Mlawi.

Pia alisema wataangalia uwezekano wa kutumia maghala ya kampuni ya kusafisha mafuta ya Tiper, kwani ina maghala ya kutosha kuhifadhia shehena za mafuta.

Alisema kitendo cha COPEC kuingia kwenye biashara hiyo ya ushindani kutawafanya wafanyabiashara binafsi kutoichezea tena Serikali.

Alisema ana uhakika wataendesha biashara hiyo vizuri, licha ya vita vya kutaka kuwakwamisha ili wasiingie katika biashara hiyo.

Vita serikalini Kampuni hiyo licha ya kuanzishwa mwaka 1999, Serikali iligoma kuipa leseni ya biashara hiyo, hali inayoelezwa na baadhi ya vyanzo vya habari kutoka ndani ya TPDC, kuwa ulikuwa ni mpango uliohusisha baadhi ya maofisa wa Wizara ya Nishati na Madini.

Hali hiyo iliifanya TPDC kushindwa kuunda menejimenti yake. Vita dhidi ya COPEC viliifanya Serikali iiamuru TPDC kuachana na biashara ya mafuta badala yake ijielekeze kwenye kutafuta na kutafiti mafuta.

Mwaka 2006 kampuni hiyo ilifufuliwa baada ya kutokea uhaba wa mafuta, lakini baadaye Serikali ikaitaka isiendelee na mpango wake wa kuagiza mafuta.

Baada ya kutokea tena uhaba wa mafuta juzi kutokana na mgomo wa wafanyabiashara binafsi, Serikali katika kikao chake kilichohusisha watendaji wa Ikulu, Wizara ya Nishati na
Madini, TPDC na Ewura, iliamua COPEC iingie rasmi kwenye biashara ya ushindani wa mafuta.

Mpango wa baadaye Kwa mujibu Mlawi, licha ya kupewa kiasi hicho na Serikali, itaendelea sasa na mpango mkakati wake wa kujiimarisha kibiashara, ikiwa ni pamoja na kukopa fedha kutoka vyanzo vya ndani ili iweze kujiingiza kwenye ushindani zaidi.

Alisema pia fedha watakazopata licha ya kuzitumia kuagizia shehena ya mafuta, watazitumia kujenga vituo ya kusambazia mafuta na maghala.

"Tumefanya biashara hii ya mafuta muda mrefu tunaifahamu nakuhakikishia kuwa pamoja na kuungwa mkono na Serikali, lakini tutatoa ushindani wa kutosha," alisema Mlawi.

Vituoni jana Upatikanaji wa bidhaa ya petroli katika vituo vya mafuta ulikuwa wa kusuasua, kwani vingi havikuwa na bidhaa hiyo, licha ya kampuni kubwa kuruhusu kusambazwa.

Kutokana na mahitaji kuwa makubwa, vituo vingine viliuza nishati hiyo juzi jioni na kujikuta vinaishiwa, hivyo kulazimika kusimamisha huduma na kufanya wananchi waendelee kuhangaika.

Vituo vya BP na Engen pia viliendelea kutotoa huduma hiyo kutokana na maghala ya yake juzi kutoruhusu kusambazwa kwa shehena yake.

Naye Halima Mlacha, anaripoti kwamba wakati hali ya uuzaji mafuta ikiendelea kutengemaa sehemu mbalimbali nchini, bado baadhi ya wasambazaji wa mafuta hayo hasa wa BP walionekana dhahiri kutouza mafuta hayo.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili kwenye maeneo kadhaa ya Dar es Salaam ulishuhudia vituo kadhaa vya mafuta vya BP na CamelOil vikiwa haviuzi mafuta, huku wafanyakazi wao wakionekana kupiga soga.

Vituo vya BP vya Mwenge, Mikocheni, Sinza Kijiweni, Ocean Road na Kinondoni, vilikuwa tupu, bila dalili zozote za biashara.

Hali ilikuwa vivyo hivyo katika vituo vya CamelOil Afrika Sana, Engen Mikocheni na OilCom. Hata hivyo, gazeti hili lilishuhudia baadhi ya vituo vya TSN Oil Bamaga, GBP na Big Bon Afrika Sana, vikiendelea na biashara ya mafuta ambapo kwa jana hakukuwa na foleni kubwa ya magari na watu kama ilivyokuwa juzi.

Vituo vingine vilivyokuwa vikiuza mafuta ni Oil Com Mwananyamala, Gapco na Oryx Posta Mpya.

Mfanyabiashara maarufu nchini na msafirishaji mizigo nje ya nchi, Azim Dewji, alitupia
lawama Ewura na Serikali kwa tatizo hilo la ukosefu wa mafuta na kuhadharisha juu ya kurejea enzi za kupanga mistari kununua bidhaa kama sabuni.

"Wanataka kuturejesha enzi za foleni, hii si sahihi kabisa, nchi ilikuwa inakabiliwa na tatizo la umeme, sasa imeibuka la mafuta, ambalo linatokana na kuchanganya siasa na biashara, tunaomba Serikali iliangalie vizuri suala hilo," alisema Dewji.

Alisema tatizo linaloendelea limetokana na Ewura kulazimisha wafanyabiashara kuuza mafuta chini ya gharama zao za uendeshaji, hali ambayo alidai inatokana na biashara kuchanganywa na siasa.

"Jamani ikumbukwe kuwa bei ya mafuta inadhibitiwa na soko la dunia, hakuna mfanyabiashara mwendawazimu anayenunua mafuta halafu akae nayo," alisema.

Aliitaka Ewura iweke wazi vipengele ambavyo Serikali imefuta ushuru ili vibainike, kwa kuwa sasa jambo hilo bado ni siri, hali inayosababisha shaka kuwa hakuna punguzo lililofanyika.

Akizungumza na HABARILEO, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo, alisema kuhusu baadhi ya vituo kutouza mafuta Bodi ya Mamlaka hiyo inatarajiwa kukutana leo, pamoja na mambo mengine, kujadili suala hilo na hatua za kuchukuliwa.

Kuhusu kutoweka wazi vipengele vya ushuru uliopunguzwa na Serikali, alisema suala hilo si la kweli na kwamba hata katika ukokotoaji wa bei hizo mpya, kila kipengele kilioneshwa na kampuni zote za biashara kupewa nakala

SOURCE: HABARI LEO AUG 12.

My take: Yalishajadiliwa hapa JF. Wanaposema JF inaleta habari kuchafua serikali hawaItendei haki. Wamekiri mpango haukuwepo. Sijui kama walipita pita huku wakadokoa au !

nadhani kitendo cha serikali kuanzisha kampuni ya copec kwa ajiri ya uagizaji wa mafuta ni cha kupongezwa sana nadhani imebaki tu utendaji wake na tuone tija na kama wakifanikiwa nadhani ni wakati wa serikali kuingia kwenye biashara ya madini kwa kuweka sheria ya kila kampuni inayochimba madini tanzania lazima serikali iwe na hisa japo asilimia 30% na kuwa na uwakilishi katika kampuni hii

mwanzo mzuri hongera serikali kwa maamuzi ya kuingia kwenye biashara ya mafuta kazi iliyobaki ni kufufua tipper kiwanda cha kusafisha mafuta ghafi ili kuondoa harakati za kuagiza mafuta yaliyosafishwa na lami toka nchi za nje

Back
Top Bottom