Kwani ni lazima serikali iingilie sekta binafsi ya Mafuta? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwani ni lazima serikali iingilie sekta binafsi ya Mafuta?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 9, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 9, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Wananchi wanalalimika kuwa kuna tatizo la mafuta; wafanyabiashara wanasema hawana mafuta, serikali inasema wafanyabiashara wapunguze bei n.k Nimebaki najiuliza kuna uhusiano gani kati ya upungufu wa mafuta jijini na utawala uliopo madarakani? Kwanini tatizo la upungufu wa mafuta halikutokea kwa mfano wakati mmomonyoko wa uchumi duniani umeiva? Kwanini liwe ni tatizo ambalo linaonekana kuhusiana na bei zaidi au ni kweli ugavi wa mafuta ni mdogo hivyo?

  Lakini upande mwingine inabidi ujiulize kwenye nchi inayofuata "uchumi wa soko" kwanini serikali ipange bei ya mafuta badala ya kuacha soko liamue kiasi gani kiingizwe na kwa bei gani kumeet demand?

  Je Serikali haina reserve ya mafuta kwa ajili ya hali kama hii? Kwa mfano kama tungekuwa tunaenda vitani leo hii tungeweza kuwa na mafuta ya kutosha kuhudumia vikosi vyetu?

  Lakini swali linalosumbua mimi kama wengine vile vile je is the a genuine shortage of oil or an artificial one? Kama ni genunie, kwanini serikali basi inafikiria kwa kulazimisha watu washushe bei ndio mafuta yataongezeka? Kwanini serikali isiseme wafanyabiashara wauze katika bei ya awali tuone kama mafuta yatatokea - maana kama mafuta yanatokea bei ikiwa juu na hayapo bei ikiwa chini maana yake ni kuwa kuna mtu anafanya "hoarding"? ni muhimu kujua wapi na kina nani?

  Upande mwingine, kama wenye vituo vya mafuta hawataki kuagiza mafuta katika bei ya hasara serikali inaweza vipi kuwalazimisha kuagiza mafuta bila kuonekana inaingilia "sekta binafsi"?
   
 2. MANI

  MANI Platinum Member

  #2
  Aug 9, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Mkuu serekali imeshindwa kumfukuza kazi katibu mkuu iliemwajiri itakuwa kuwasimamia wafabiashara mbona hilo ni gumu sana.
   
 3. m

  majege Senior Member

  #3
  Aug 9, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 117
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu hawa jamaa watoa pesa nyingi sana kwaajili ya kampeni ya sisiem kwa uhakika wa kuvuna baada ya uchaguzi, kilichotokea sasa ni kwamba mpaka sasa pesa zao hazijarudi na kama ilivyo kawaida selikali nayo imewageuka. ndiyo maana unashindwa kuelewa ni nani mwanye nguvu nchi hii. Ni siku nne tu zimepita Masebu alikua akijigamba kuwa Reserve ya mafuta aina zote ya siku zisizopungua 40. sasa unashangaa siku mbili baadaye hakuna mafuta. Kuna tatizo kubwa sana la viongozi wa taasisi zetu hizi za serikali kwani hawajui hata wanachokiongea.
   
 4. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2011
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nafikiri serekali imejichanganya, kwenye soko huria huwezi kuagiza kwa kupayuka barabarani na "kuagiza". Ynanahitajika mazungumzo kati ya wafanyabiashara na serekali. Serekali itoe ruzuku kwa wafanyabiashara, kama kupunguza kodi, ili nao washushe bei. Tofauti na hapo serikali inaweza kuingia kwenye competition, kwa kufungua viwanda vyake vya mafuta.
  Ila kuna swali gumu wenye hisa kwenye hayo makampuni si ndo haohao wanaotuongoza? Au ni akina nani waliisaidia ccm kwenye kampeni za uchaguzi?
   
 5. Nyota Ndogo

  Nyota Ndogo Senior Member

  #5
  Aug 9, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania ina genge la wasanii wanaojiita serikali.
   
 6. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu unaongelea serikali ipi?

  Mimi naona hii drama ina 2 visible players (wafanyabiashara na wananchi) na 1 invisible player (hiyo inayoitwa serikali)!!

  Katika mazingira kama hayo, invisible na wale visible wanaweza kufanya kazi pamoja???
   
 7. G

  Godwine JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  kanuni ya demand na supply inafanya kazi kwenye free market lakini kilichotokea katika soko la mafuta ni wafanyabiashara wameunda catel yani ushirika wa kudhibiti bei na sheria za tume ya ushindani inaipa nguvu serikali kuingilia inapoamini kuna nanma yeyote ya umoja wa wafanyabiashara kudhibiti bei

  katika suala la upungufu wa mafuta linatokana na sababu mbili kubwa sasa.

  1. kiburi cha wafanyabiashara dhidi ya serikali kwani wanaamini kuwa serikali lazima isalimu amri na haina nguvu na uwezo wa kuwadhibiti

  2.kutokana na kushuka kwa bei watumiaji wengi hawaamini kuwa bei itaendelea kubaki chini na wanadhani kuwa ni wakati mfupi tu itabaki kwenye bei hii na ndio maana wamenunua na kuweka stock yao kwa siku za karibuni kwa niliweza kuzungumza na mkandarasi wa barabara anayetarajia kufanya kazi zake muda wa karibuni yeye ameweza kununua zaidi ya lita 700,000 za diesel na kuziweka akiba kwa ajili ya mitambo yake ili pia linaongeza upungufu wa mafuta

  imefika wakati ambao serikali haiwezi kukwepa kuunda mfumo wa upatikanaji wa mafuta wa uhakika kwani katika nchi ambayo umeme ni shida na mafuta nayo yakiwa shida basi lazima ife

  serikali lazima ifikirie kufufua kiwanda cha kusafisha mafuta cha tipper ili kupunguza bei za mafuta na kuongeza ajira kwa vijana wetu la sivyo haitaweza kusalimika kutoka katika janga la mfumuko wa bei na usalama wake yenyewe
   
 8. The Stig

  The Stig JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 882
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80  EWURA imefanya kosa kubwa sana kuingilia bei ya mafuta kama ilivyofanya. Katika soko huria, hauwezi ukapanga bei. Ukipanga bei unazalisha ARTIFICIAL SHORTAGE (kuhadimika bidhaa) kutokana na wauzaji kutokuwa tayari kuuza kwa bei ya hasara. Hii nayo inatengeza BLACK MARKET (ulanguzi) na mwisho kabisa INASAMBARATISHA UCHUMI.

  EWURA wa swallow their pride na kuondoa agizo lao la bei ya 2004/=.

  Inabidi Tanzania ifike mahali ambako watu wanafikiria kwa kutumia akili zao zaidi ya mioyo yao.
   
 9. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  nchi yetu haina mwelekeo hatujui tunaelekea lakini pia tusisahau hawa wafanyabiashara ndio walipelekewa vimemo kwa ajili ya kutoa chcchote kwenye uchanguzi kwa njia nyingine ndio waliopatia hela ya kampeni Jk kwa hiyo ni vingumu kukemea hata kuwaajibisha hao wafanyabiashara.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Aug 9, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  serikali ikiamua kukaa pembeni kutakuwa na athari gani? Maana bei ikipanda sana watu hawatanunua! Hapa ndio suala la UDA linapokuja!!
   
 11. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  MKuu mimi nadhani Mungu anataka kutufundisha kitu na pengine kama kuna watu wake Tanzania waliokuwa wanaomba basi huenda ndo ukawa ukombozi wa nchi hii. Haiwezekani kwa hali yakawaida balaa juu ya balaa lingine. Balaa la mafuta juu ya balaa la umeme! Mapigo juu ya mapigo kama wana kipindi cha wanawaiziraieli walipokuwa wa kiokolewa toka Utumwani misiri?

  Kitendo cha serikali kutunishiana misuri na wafanyabiashara wa mafuta na serikali kushindwa hii inadhihirisha ulegelege wa serikali. Naamini serikali hawana ujasiri wa kutekeleza maamuzi wanayoyasema kwa sababu vituo vya mafuta ni vya mafisadi walewale na pengine familiya za wakubwa!

  Kuna thread moja humu ilikuwa inaongelea ingridients za kodi ya mafuta na kulikuwepowapo na tetesi juu ya kuwepo kwa ingridient za sirisiri ndani ya kodi hiyo. Watu wanasema pengine wafanyabiashara hawa kuna wakati wanatoa michango mingine zaidi ya hizi kodi za mafuta na kuahidiwa mavuno baadaye. Sasa mambo yamebadilika na wao walishatoa michango hiyo. Serikali imejitutumua kusema kujiosha mbele ya wananchi huku wakijua ukweli wa mambo nyuma ya pazia.


  Tusubiri tuone ila inaonekana mambo ni bandika bandua na mengi tu yatakuja na nadhani litakalofuatia ni njaa kubwa tena!
   
 12. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #12
  Aug 9, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Tatizo la mafuta ni 'artificial' na ni la wafanyabiashara. Kumbuka wakati mafuta yanapanda bei katika soko la dunia hatukuwahi kuona upungufu hata sku moja. Kitu cha kushangaza mafuta yalikuwa yanapanda bei kila siku utadhani ni maji yanayonunuliwa ruvu na kuuzwa siku hiyo hiyo. Nina maana kuwa kama kuna shehena imenunuliwa mwezi wa 3 na bado ipo kwanini bei ikibadilika usiku mmoja iathiri shehena hiyo?

  Wapo watakaosema ni soko huria, lakini soko huria na bei za mafuta linaathiri sana nchi zinazoagiza mafuta kila siku na matumizi yake ni makubwa. Huko nyuma ilishawahi kutokea TPDC walipandisha bei miezi 3 baada ya bei kupanda soko la dunia kwasababu walishagiza kwa bei ya wakati huo.

  Soko huria ni zuri likiachiwa kufanya kazi kwa maana hiyo, lakini wafanyabiashara wameamua kufanya ushirika kinyume na taratibu za soko hilo popote duniani. Kwa hivyo, kuachia huria ni kuhalalisha maumivu zaidi kwasababu watakaa vikao na kusema tuuze lita 7,000. Ni kwa msingi huu ndipo EWURA iliundwa si kuthibiti bei bali kumlinda mtumiaji 'consumer'.

  Hata nchi zilizoendelea zina consumers organizations, sio kudhibiti bei bali kuhakikisha kuwa soko linakuwa huru kwa maana hiyo na kuwa mtumiaji hakamuliwi mpaka tone la mwaisho la damu kwa ushirika wa wafanyabiashara, bali bei zinapangwa na soko lenyewe.

  Kama TPDC ingekuwa katika ushindani wafanyabiashara wasingefika hapa walipo kwasababu soko lingekuwa huru na si la ushirika. Hatujajifunza kuwa kuweka sekta muhimu kama hii mikononi mwa watu wawili au watatu ni hatari, na kwamba ikitokea dharura sijui tutafanya nini.

  Wafanyabiashara hawa wana nguvu sana na wanatumia umoja to creat demand, na wanajua serikali haina pa kutokea. Ndio manaa hadi leo suala nyeti na la hatari kama hili linashughulikiwa na EWURA inayoonekana kutokuwa na uwezo kukabiliana nao. Serikali ipo kimya na sijui ni kwanini inawaogopa.

  Marekani ina stategic reserve na ndio wenye soko huria, sasa tujiulize kwanini wana reserve. Kuna wakati waliachia mapipa milion 30 na yaka stabilize bei kiasi, na ile psychology tu kuwa uwezekano wa kutumia strategic reserve upo ulishusha bei sana. Sisi ya kwetu ipo wapi?

  Hili ni tatizo la kutokuwa na mkakati, nguvu kubwa ya waagizaji inayoizidi serikali na madudu mengine ambayo tutayafahamu tu huko mbeleni. Sitashangaa nikisikia wanahisa ni viongozi, nani alijua Kapuya ana hisa Simon au mwenyekiti wa bodi ni consultant pia !!
   
 13. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #13
  Aug 9, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  nchi hii haijawahi kua na serikali tangu 2005!!!
   
 14. Lord

  Lord Member

  #14
  Aug 9, 2011
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 91
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  MM, Hivi nchi hii ina serikali au genge la wezi?? Si umesikia juzi wanaambiana wanafikiri kwa makalio. Sasa mtu anayefikiri kwa vifaa vya kukalia unategemea anafikiria nini hasa zaidi ya kushibisha tumbo ili makalio yakue.
   
 15. G

  Godwine JF-Expert Member

  #15
  Aug 9, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  tetesi: rais kikwete amewapa maagizo wanajeshi kuingilia shell binafsi kuzikagua na kuwalazimisha na ikibidi MPs wa jeshi wauze kwa nguvu

  note:bado sijaweza kuzithibitisha habari hizi   
 16. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #16
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Unamaanisha 2005 au 1985???
   
 17. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #17
  Aug 9, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Mkuu I beg to differ. Hakuna serekali makini duniani isiyomlinda mwnanchi wa kawaida (mlaji) kwa kisingizio chochote kikiwemo cha Free Market. Kilichofanyika hapa kwetu ni muendelezo wa chama lege lege kilichozaa serekali legelege ndio maana hata TIPPER ikapelekwa kuzimu na hao wafanyabiashara wa mafuta. Ilikuwa ni kosa kubwa kwa serekali kujiondoa kwenye hiyo biashara kwa asilimia 100 na ndio maana wafanyabiashara wamehamua kuichezea kama wanavyotaka na kwakuwa wanajua serekali haijui A wala B ya biashara hiyo at the end watasalimu amri na kuwaacha wauze kama wanavyotaka wao na kuendelea kuneemeka huku walalahoi wakikamuliwa zaidi. Najiuliza kama ni kweli walikuwqa na akiba ya mafuta iliyooagizwa kabla ya bajeti mbona mafuta ya taa yalipopandishwa bei hawakusema wana akiba wakaendelea kuuza kwa bei ya zamani hadi walipoagiza shehena mpya? Huu ni uhuni wa wafanya biashara na ni nafasi ya serekali kuachana na ulege lege na kuonesha makucha. Kama wanapata hasara hawa wachache wanaouza wanafanya kazi msikitini/kanisani? hawataki hasara? Big Born kila siku anauza yanaisha anainweka na kuuza tena yeye ndo hataki faida? Narudia huu ni uhuni lazima serekali makini ichukue hatua na ilinde watu wake.
   
 18. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #18
  Aug 9, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,081
  Likes Received: 6,544
  Trophy Points: 280
  Serikali gani??????????? naungana na aliyesema nchi haijawahi kuwa na serikali since 2005.
   
 19. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #19
  Aug 9, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Wauza mafuta ndio walioiweka serikali madarakani kw michango mikubwa aliyoifanyisha MAKAMBA SR......jeuri yao ipo hapo
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Aug 9, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwanini hawakuboresha UDA? kwani watu wote DAR wanahitaji kuwa na magari na pikipiki?
   
Loading...