EWURA kuwa mpangaji wa bei ya mafuta katika soko huria itazamwe upya

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,623
46,269
Kwa nini serikali inapanga bei za mafuta katika uchumi wa soko huria kupitia taasisi yake ya EWURA?

Hili wazo la kuipa taasisi ya kiserikali jukumu la kibiashara kuwapangia bei wafanyabiashara binafsi lilitokana na sababu zipi za msingi na limekuwa na manufaa gani mpaka sasa kwa walaji wa mafuta?

Katika soko huria kama hakuna mapungufu ya kisoko katika ushindani katika biashara husika katika sekta binafsi, uingiliaji wa serikali kwa mtindo huu huwa ni hasara zaidi kuliko faida na ni chanzo cha matatizo mengi zaidi kama uhaba usio wa lazima na "rent seeking".
 
Wanaohujumu mafuta ya Petroli ni serikali wenyewe,CCM ni mafisadi👇
 
Nakuunga mkono, iachwe soko liamue make kuna wengine wanayo mtaji wa kuagiza mafuta kwa wingi na kuuza kwa bei rafiki lakini wanasubiri EWURA wapandishe bei.
EWURA ni wahujumu uchumi namba moja.
 
Kwa mara ya kwanza tangu uhuru mafuta yanauzwa kwa bei juu zaidi!

Mamaenu anaupiga mwingi!

Sisi team Magu tuwazoom tu jinsi mnavyolia kwa uchungu wa vidonge vinavyowaingia.

Na bado
 
Kwa mara ya kwanza tangu uhuru mafuta yanauzwa kwa bei juu zaidi!

Mamaenu anaupiga mwingi!

Sisi team Magu tuwazoom tu jinsi mnavyolia kwa uchungu wa vidonge vinavyowaingia.

Na bado
Jikite kwenye mada, acha taarabu kama za mtalikiwa.
 
tuilaumu serikali au tuwalaumu mababu walioachwa na bogey lililomigrate huko Sauzi nk. katika nchi zote kweli waliona TZ ndio pazuri?
 
Kwa nini serikali inapanga bei za mafuta katika uchumi wa soko huria kupitia taasisi yake ya EWURA?

Hili wazo la kuipa taasisi ya kiserikali jukumu la kibiashara kuwapangia bei wafanyabiashara binafsi lilitokana na sababu zipi za msingi na limekuwa na manufaa gani mpaka sasa kwa walaji wa mafuta?

Katika soko huria kama hakuna mapungufu ya kisoko katika ushindani katika biashara husika katika sekta binafsi, uingiliaji wa serikali kwa mtindo huu huwa ni hasara zaidi kuliko faida na ni chanzo cha matatizo mengi zaidi kama uhaba usio wa lazima na "rent seeking".

Kazi na Majukumu ya EWURA

Kwa mujibu wa Kifungu cha 7 cha Sheria ya EWURA, majukumu ya Mamlaka niajukumu hayo ni:-

Kutekeleza kazi zote zilizoanishwa kwenye sheria ya EWURA na Sheria za Kisekta;

Kutoa, kuhuisha na kufuta leseni;
Kuweka na kusimamia viwango vya ubora wa huduma;

Kudurusu na kusimamia bei za huduma,

Kutunga sheria ndogo na kanuni;

Kufuatilia maendeleo ya sekta zinazodhibitiwa kwa kuzingatia upatikanaji, ubora wa huduma, gharama ya huduma, ufanisi wa uzalishaji, uwekezaji na usambazaji wa huduma;

Kusimamia utatuzi wa malalamiko na migogoro;

Kutoa taarifa kuhusu kazi za udhibiti;

Kupata maoni ya mamlaka zingine za kiudhibiti;
na
Kusimamia utekelezaji wa Sura Na 414 ilyoianzisha EWURA.

Katika kutekeleza kazi zake, EWURA ina wajibu wa kukuza ustawi wa Watanzania kwa kuzingatia yafuatayo:-

Kuhimiza ushindani wenye tija na ufanisi kiuchumi;

Kulinda maslahi ya walaji;

Kulinda mitaji ya kifedha ya watoa huduma;

Kuhimiza upatikanaji wa huduma zinazodhibitiwa kwa makundi yote ikiwamo wenye vipato vya chini,makundi maalumu na vijijini;

Kuimarisha utoaji wa elimu kwa umma na kujenga uelewa kuhusu sekta zinazodhibitiwa, ikiwamo haki na wajibu wa watumiaji na watoa huduma zinazodhibitiwa, namna ya kupokea na kutatua malalamiko na migogoro na kazi, wajibu na shughuli za Mamlaka;

Kulinda na kutunza mazingira.
 
Back
Top Bottom