Kwani Morogoro kuna tatizo gani?

Kwani Morogoro kuna tatizo gani?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,097
Reaction score
43,308
Sijui kuna tatizo gani katika Mkoa huo. Imekuwa ni kawaida kiongozi akienda ni lazima alalamikie matatizo ya matumizi ya fedha za Umma. Ameenda Rais, ameenda Waziri Mkuu, ameenda Jafo na hivi sasa kapita Katibu Mkuu wa CCM.

Wote kwa namna tofauti na kuhusiana na mambo tofauti tofauti wanalalamikia au kuibua matumizi mabaya ya fedha au usimamizi mbaya wa fedha. Kuna watu hadi waliondolewa lakini inaonekana kama Moro - Mji Kasoro Bahari - unaonekana kuwashinda au kushindwa!

Kuna tatizo gani Morogoro? Labda hata mikoa mingine hali iko hivyo lakini kutajwa kwa Morogoro mara kwa mara ni lazima kuwafanye watu wajiulize "kunani'?
 
Sijui kuna tatizo gani katika Mkoa huo. Imekuwa ni kawaida kiongozi akienda ni lazima alalamikie matatizo ya matumizi ya fedha za Umma. Ameenda Rais, ameenda Waziri Mkuu, ameenda Jafo na hivi sasa kapita Katibu Mkuu wa CCM. Wote kwa namna tofauti na kuhusiana na mambo tofauti tofauti wanalalamikia au kuibua matumizi mabaya ya fedha au usimamizi mbaya wa fedha. Kuna watu hadi waliondolewa lakini inaonekana kama Moro - Mji Kasoro Bahari - unaonekana kuwashinda au kushindwa!

Kuna tatizo gani Morogoro? Labda hata mikoa mingine hali iko hivyo lakini kutajwa kwa Morogoro mara kwa mara ni lazima kuwafanye watu wajiulize "kunani'?
kuna Watanzania
 
Tuko busy kuwaweka ndani wakuu wa shule waliofelisha. Ile kudili na wakuu wa shule, huku noti zinapigwa usipime!?
 
Kuna makada wengi wapenda kuusudu matumbo yao kwanza arafu kufikilia baadae kupeleka fedha kwenye mambo yaliokuwa yamepangwa kwa ajili ya fedha hizo
 
Usituletee tena habari za huyo vuvuzela Bashiru Ally. Yeye akipita sehemu ni kupiga tu makelele na hanaga data siku zote.
 
Tatizo lipo katika mamlaka ya uteuzi. Ni watu was Aina gani wanateuliwa?
 
Tatizo ni moja tu, CHADEMA wamepenyeza watu wao kwenye hizo halmashauri ndio wanaoiba
 
Hivi suala la katibi mkuu wa CCM kutembea na msafara linakaaje?

Maana jana tumesimamishwa sana foleni kwenye round about fulani hapa moro(siifahamu jina). Kuja kusikia eti katibu mkuu wa CCM anapita.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna siku hapa A twn tumesimamishwa ghafla magari hayaendi, mara tukaona mapikipiki na ma landcruiser...kuulizia ulizia eti ni Mr slow anapita.
 
hujaelewa nini akitoka mwenyekiti anakuja katibu, kama mwenyekiti ni raisi katibu wake ndio msaidizi wa raisi, na msaidizi wa raisi kwanini asiwe na msafar wa wapambe

hivi vitu vipo 2 dunia 3 ambayo bado wapo karne ya 19


Hivi suala la katibi mkuu wa CCM kutembea na msafara linakaaje?

Maana jana tumesimamishwa sana foleni kwenye round about fulani hapa moro(siifahamu jina). Kuja kusikia eti katibu mkuu wa CCM anapita.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku hapa A twn tumesimamishwa ghafla magari hayaendi, mara tukaona mapikipiki na ma landcruiser...kuulizia ulizia eti ni Mr slow anapita.
Mikoani mnaonewa sana ! Polepole si wa kupishwa njia , hana hadhi hiyo
 
Hayo matatizo ya matumizi mabaya yameripotiwa na chombo gani cha kitaalam?

Weka ripot ya CAG hapa.

Hata wao huko ikulu wanasemwa kila siku madudu mengi.

Wawavumilie tu kama na sie tunavyovumilia.

Moro mji kasoro bahari, ndiyo mji wa wajanja ule. Kila kitu mipango.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bwashee unasalimiwa na Cecil Mwambe!
Chadema ilikuwa tayari inayo mipango yote ya fukara Mwambe kabla hata hajaipanga , mimi nilikuwa mtu wa kwanza kuripoti humu jf tarehe ya Kapuku Mwambe kurudi ccm , angalia uone
 
Back
Top Bottom