Kwani bila pombe sherehe haikamiliki?

Kwani bila pombe sherehe haikamiliki?

Ni kweli uliyoandika!

Ni kweli ili sherehe ifane hasa harusi ni lazima watu washiriki, wale, Wanywe na kucheza.

Lakini kwenye kunywa siyo lazima iwe pombe, kunywa wanaweza kunywa juisi, togwa, maji n.k
Unaweza wewe... yaani wewe kutokunywa bia unaona ndo sawa na wanywa bia wakiona kunywa juisi kwenye sherehe siyo sawa, unawashangaa.
 
Ikulu ni mahapi patakatifu. Pombe ya nini? 🤔🤔
 
Kama kikao cha kwanza usipowapa watu mvinyo basi tegemea dau dogo dogo!Ukishawapa bia kadhaa ndio hata jeuri ya kujinadi kwa dau kubwa kubwa inakuwepo!Kesho yake anaamka na maumivu ya namna ya kufikia lengo aliloahidi!Weka Soda sasa kwenye kikao cha kwanza cha kamati,watu nao watajinadi kwa viwango vya "soda"!

Haya mambo haya nayajua,nilishawahi kujinadi laki 3 wakati kikawaida kama sijapiga mambo ningejibana na kusema laki 1!

Hayo ni kwenye kamati,kwenye ndoa ukifaka kupata washiriki wengi basi hakikisha unaweka mvinyo!Usipoweka Kama wanakupenda sana watakuja wakiwa nyingi na chupa za maji ambazo ndani zina pombe kali zinazofanana na maji!

Mimi harusi hata kama nimechanga wasipoweka mvinyo wala siwezi kukanyaga!Yaani nikae masaa 5 au 6 nakodoa macho tu!!!!Siwezi kwakweli!

Siku ya ndoa yangu nilimuagiza mdada aliyekuwa anatuhudumia meza kuu aende kwa jamaa yangu ambaye nilikuwa nimeshampanga aniwekee nyagi kwenye chupa ndogo ya maji!Wife alimind ila sasa akawa analazimika kutabasamu maana camera mara kwa mara ilikuwa inakuja meza kuu!

Mwisho wa siku nilipokuwa level na yeye akaona nimepiga ya kutolea aibu tu akapotezea na sherehe ikaendelea!
Kama kwenye ndoa yangu nilishindwa kuvumilia,sembuse za wengine!Ujinga sipendi atii!!!!😁😁
 
"inasaidia ondoa aibuuu...nieze kurembua na kudeka deka kwa my beibeee kuonesha uma kuwa hata sie twaishi ndoa/mahusiano ya amani ...ili hali mmmmmm" mwisho wa kunukuu

wengi hujilipua ili kuweza kucheza nyimbo za kisingeliii/taarabuuu etc

Ladha ya reggae inachagizwa na mvinyooo we waulize wachaggaaa....changamoto mzuka wa jani la R-CHUGGA ukipanda awaezii lipata
 
😆😆😆
Jamani acheni na sie wanywa soda tupate mada za kuchangia. Sio kila siku tunaishia kuuliza "Na sisi tuna-comment wapi?"😏😏

Acha soda, epuka kisukari.


Let's meet at the top, cheers 🍻
 
Sasa sherehe bila Pombe uende kufanya nini sasa? Yani uende Kula na kunywa soda seriously mimi hata nichange nikisikia hamna Vyombo napiga chini kwenda unless huyo mtu awe mtu wa karibu sana ndugu au mshikaji napo ntachukua chupa ya maji na kujaza Sprit umo nyeupe inayonekana kama maji tu ndio niende nayo, Vingenevyo siwezi kukaa sehemu masaa mawili na mziki upo bila pombe ni matumizi mabaya ya muda
 
Ili ujue pombe haifai kwa matumizi mtu jiulize:

Ni kwanini wanafunzi wanakatazwa kunywa pombe?

Kwanini makazini ni marufuku kunywa pombe saa za kazi?

Kwanini madaktari wanakataza/kushauri watu kuacha kunywa pombe?

Mfano mama wajawazito, n.k ?

Kila alichokataza Mungu anamaana Nzuri sana kwa faida yetu wenyewe!
 
Baba yangu kama sherehe aina pombe kamwe aendi sasa wewe andaa kijisherehe chako alafu utasikia wana kama wote utasikia shemeji yako anaumwa siwezi kuja kwenye sherehe visababu kibao kumbe hakuna pombe

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kwa uzi huu tutawajua wanywaji na wasiokunywa pombe
 
Ili ujue pombe haifai kwa matumizi mtu jiulize:

Ni kwanini wanafunzi wanakatazwa kunywa pombe?

Kwanini makazini ni marufuku kunywa pombe saa za kazi?

Kwanini madaktari wanakataza/kushauri watu kuacha kunywa pombe?

Mfano mama wajawazito, n.k ?

Kila alichokataza Mungu anamaana Nzuri sana kwa faida yetu wenyewe!
Mungu yupi unaemzungumzia hapa aliyekataza pombe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom