sblandes
JF-Expert Member
- Apr 25, 2010
- 6,153
- 4,271
Kuna ukweli kwamba Waafrika au African Diospora hawafanyi vizuri katika kustawisha uchumi katika mataifa waliopo Na wakifanya vizuri ni mara chache ukilinganisha na watu wengine.Lakini background ya mtu mweusi yawezekana imechangia kutofanya vizuri kutokana na matatizo ya muda mrefu yaliokumba vizazi hadi vizazi zaidi ya karne 5.Hii imedumaza fikra na kumjengea hofu,hivyo kupungukiwa na umakini ,wepesi wa kuamua na kutenda kwa kujiamini.
Tukija upande wetu wa Tanzania.Si tofauti sana na nchi za kiafrika katika ustawishaji wa jamii na uchumi.
Maamuzi ya mtu mmoja mmoja hayana tofauti sana na maamuzi ya serikali,kwani serikali inaponunua ndege ya raisi,au waziri kusafiri business class,au kutumia mabilioni ya maela kwenye campaign ya ubunge Igunga na ikaacha wanafuzi wanakaa chini,zahanati hazina hata bandage,ina tofauti gani tunapofanya harusi ya kifahari kwa kuchangishana wenyewe kwa sherehe ya siku mmoja,lakini hatuchangii watoto kwenda kusoma elimu bora kwenye shule bora ?
Hatuna haja ya kuongeza maazimio mengi bila kutekeleza yalio ndani ya maazimio,inaonekana makongamano mengi yanayofanyika nchini hayaboreshi makusudio ya kongamano bali yamegeuka matumizi mabovu ya hazina.
Kujitambua kwawezekana lakini kutenda ndio kitendawili.