Kwakuwa kizazi chetu kimeshindwa... Tuwekeze katika kizazi kijacho!

IsangulaKG

JF-Expert Member
Oct 14, 2010
706
386
Umewahi kujiuliza kwa nini nchi za Ulaya zinaendelea kutajirika kila kukicha huku za kwetu zikiendelea Kumasikinika?
Umewahi kujiuliza kwa nini wakati Life Expectancy kwao Ikiongezeka kwetu ndiyo inapungua zaidi?
Umewahi kujiuliza kwa nini idadi ya watu kwao inapungua wakati kwetu ndo kwanza tunazaliana?
Umewahi kujiuliza kwa nini 'vijiji' vyao vinakua kwa kasi wakati vya kwetu ndo Vinachakaa?

Kwa miaka mingi sana nimekuwa na fikra tofauti na wengine kuhusu umasikini na hali duni ya maisha na afya katika nchi zetu za bara la tatu. Japo hadi sasa bado ni mwanafunzi wa HUMAN MIND lakini maarifa ambayo nimejikusanyia hadi sasa yananitosha kuandika makala hii.

Acha tuanze kutafakari hivi:

Kukata tamaa kwa Haraka

Kwa muda mrefu nimesoma na kufanya kazi na wajapan. Kimsingi wengi wao nilikuwa nawazidi katika ufaulu na hata katika kufikiria mambo kwa haraka. Baada ya kupitia baadhi ya vitabu vya historia ya ujapan na life style yao , nimetambua kuwa hawa jamaa wanaendelea kwa kuwa wako PERSISTENT, hapa namaanisha si watu wa kukata tamaa kirahisi.

Mifumo ya familia za kijapan na maisha yao toka utotoni yanamjenga mtoto wa kijapani kutokukubali kushindwa hasa kunapokuwa na imani kuwa lile jambo analolifanya lina manufaa kwake na kwa taifa kwa ujumla, hata kama imani hiyo ni ndogo. Wajapan na rafiki zao wachina, kwa mfano wako radhi kufanya kazi hadi usiku wa manane pasipo kulalamika kwa sababu hali hiyo imejengeka toka utotoni, ni kama mila kwao, kuwajibika!

Nakumbuka wakati wanajenga daraja la mto Mara pale 'Kirumi' inaaminika walikuwa wakijenga usiku wa manane na wenyeji wa maeneo yale wakaishia kufikiria kuwa pengine ni washirikina. Kwa nchi zetu mfano Tanzania sisi ni wepesi wa kukata tamaa hasa unapoona kuwa manufaa ya jambo unalolifanya yako mbali. Mara nyingi tunahangaika na manufaa ya muda mfupi ambayo siyo sustainable badala ya kuhangaika na manufaa yanayochelewa kuja lakini ni sustainable.

Tunataka tuanze biashara leo kesho tupate faida, Tupande leo kesho tuvune. Tunataka tuajiriwe leo kesho tupate nyumba na gari na pale unapoona kuna kuchelewa kiasi basi unakata tamaa na kuanza kutafuta shortcuts. Hali hii imetuathiri sana kwani shortcut hizi tunazotafuta ndizo zinazozaa roho za Rushwa na Ufisadi. Matokeo yake yako dhahiri.

Fikra Finyu

Miaka ya Nyuma kidogo nchi kama Marekani ilipoteza watu wengi sana kutokana na Vita ya pili ya dunia. Uingereza ilipoteza watu wengi sana kutokana na magonjwa kama tauni, kipindupindu n.k, Spanish flu miaka ya karne iliyopita ilifyeka idadi kubwa ya watu huko Ulaya. Mbali na matukio haya makubwa ya kiafya, bado nchi za Ulaya zinaongoza kwa kuwa na huduma nzuri za afya...kwa nini? Kwa sasa wao manonjwa yao yamehama toka kwenye 'Infectious disease' kwenda kwenye 'Chronic Disease' na 'Uzee'. Kitaalamu Chronic disease kama Hypertension na magonjwa ya moyo yanatokana na lifestyle hasa kwa watu wenye uchumi mkubwa. Life expectancy yao imeongezeka na wazee wanaishi umri mrefu kutokana na kuboreka kwa huduma ya Afya. Wakati nchi zetu 'infectious disease' kama Ukimwi, Malaria n.k. ndo 'store' yake.

Mfano mwingine Marekani, ina disparity kubwa sana kwa weusi na weupe. Weusi wamewekewa misingi mingi sana ya kuboresha afya zao, wamepewa nafasi nyingi sana za kimasomo , lakini je wanazitumia? Hadi leo hii bado weusi wa marekani wana viwango vibovu vya afya Ukilinganisha na weupe japo wana nafasi kubwa ya Kuboresha afya zao japo kuwa hali zao bado haziwezi kulinganishwa na nchi zetu hizi zisizo makao ya 'malaika'. Baada ya kuishi Marekani kwa Muda niliweza kuona Kuwa tatizo kubwa linalotusumbu sisi ni fikra finyu. Tunapenda kila kitu tufanyiwe na tufurahie mafanikio. In short tunapenda kufurahia mafanikio ambayo hatujachangia kuyatafuta.

Ni mara ngapi umepanda katika gari na kufikiria lilivyotengenezwa na kufikiria unawezaje kutumia rasilimali zilizo katika mazingira yako ukatengeneza lenye matairi matatu tofauti na hilo ulilopanda? WE LACK CREATIVE THINKING! Tunafikiri kama maboya tu! Unakula chakula pasipo kujiuliza kimepikwaje, Unavaa nguo pasipo kujiuliza imetengenezwaje. Kila jambo jipya tunaloliona 'WE IGNORE'

Unatumia Kijiko pasipo kujiuliza Kimetengenezwaje. Mfano mzuri ni yule Mwanasayansi aliyegundua law of gravitation. Alikuwa kanisani akaona taa inayoning'inia darini inacheza wakati hakuna upepo, akatoka nje akakaa chini ya mwembe, embe likamponda kichwani wakati hakuna upepo., hapo akaanza mfululizo wa fikra mpaka akagundua law of gravity.
Au mfano wa yule daktari aliyegundua kile kifaa cha Madaktari 'Stethoscope' Alikuja mgonjwa mnene sana na kwa kuwa wakati huo walikuwa wanasikiliza mapigo ya myo kwa kuweka sikio kifuani kwa mgonjwa, akapata wazo kukunja karatasi ili kutengeneza kama 'tube' iliyomwezesha kusikia mapigo ya moyo wa yule mgonjwa mnene. Je sisi wataalamu wetu wanapokosa vifaa hospitalini wanakuwa na akili ya kufikiria njia mbadala au ndo hukumu ya kifo inatolewa kwa mgonjwa hapo hapo?

Ni Mambo au matukio mangapi yanayotutokea na kushindwa kuyafikiria kisayansi na kuwa wagunduzi? Bahati mbaya kabisa twatanguliza ushirikina au kwa anayesali saana huishia kusema ni mpango wa Mungu! Ili tuwe ni wagunduzi twahitaji kuhoji kila kitu kinachotutokea maishani.

Mfumo huu wa kutokuhoji kila kitu umetufanya tuwe wana mapokeo. Mfano hatuwezi hata kuhoji kwa nini hospitalini hakuna dawa, kwa nini serikali haitekelezi huduma muhimu kwa wananchi badala yake tunaishi kwa kuwa tunaishi.

Moja wapo ya kitu kinachochangia kuboresha afya katika nchi za wenzetu ni kitu kinachoitwa 'Service Demand" Kwetu huku twaishia kulalamika tu kuwa hakuna vifaa na dawa hospitalini pasipo kudai kwa nguvu zote. Kwa mfano mtu mwenye Medicaid Insurance aliyopewa na serikali kule Marekani ana haki ya kuishitaki serikali au kituo cha afya kama hakupata huduma fulani ambayo ni haki yake. Ni mara ngapi ndugu zetu wanafariki mahospitalini kwa uzembe au kukosa huduma za msingi na tunaishia kusema 'ni mpango wa Mungu? Ni mara ngapi watoto wetu wanakosa chanjo kwa kuwa dawa zimeisha na tunajiendea nyumbani kwa Amani?

Ili afya zetu ziimarike tunahitaji kudai Huduma ambazo ni Haki yetu. Kwa nini ukose umeme na Unalipa Kodi? Kwa nini ukose dawa Hospitali na Umekatwa zaidi ya Asilimia 20 ya Mshahara? Mambo haya yanajitokeza pia hasa katika mifuko yetu ya Bima, una Bima ya afya, unaenda hospitalini hakuna dawa, kwa nini usidai na kwenda mahakamani? Kwa nini wanakijiji wanakubali shule isiyo na Madawati? Kwa nini wasidai?Kwa nini? Kwa nini?

Tuna matatizo katika fikra, hatujajikomboa, si wagunduzi, twaishi kwa kudra za mwenyezi Mungu na mambo ya 'hewala'

Moyo hafifu wa kujituma

Ni mara ngapi umeenda dukani ukakuta limefunguliwa na Muuzaji hayumo? This how we are! We are not serous in whatever we are doing! Mfanyakazi serikali hakai ofisini, Mwendesha mitambo kiwandani anatega, Daktari hospitalini hayupo, Mwalimu shuleni hayupo, Mkulima hayuko shambani, Mwanafunzi hayuko Darasani. Hebu tembelea sehemu za wengine kama Taiwan, Engineer yuko barabarani au juu ya Magorofa anajenga kila siku. Daktari yuko hospitalini anatibu kila siku, Mfanya biashara yupo katika eneo lake kila siku...Kila mtu anawajibika, Kila mtu anajituma ,kwa nini sisi pia tusijitume?

Mtu pekee atakewasaidia watanzania kujiuondoa katika maisha ya sasa ni yule atakayegundua jinsi ya kuwakomboa kifikra. Kuwabadili fikra za uzembe, kutokuwajibika, kutokuhoji ili kuwajengea fikra madhubuti. Tofauti na hapo hatutapata maendeleo kamwe!

Pengine kizazi hiki kimeshindwa, basi naamini ni vema angalau tutimize wajibu wa kuwekeza katika wanetu:
  • Tuhakikishe Mimba za kuwazaa zinapatikana kwa haki, wapate malezi yanayowajenga fikra (siyo kutegemea tuisheni kufaulu)
  • Tuwatengenezee mifumo ya elimu 'competitive' inayowafundisha kufikiri siyo 'kulishwa' kila kitu. Tuwe na waalimu wanaochochea ufikiri siyo wanaochochea 'ukariri'
  • Tuwe na jamii inayowajibika kila mtu na nafasi yake , siyo jamii inayotafuta shortcuts na mafanikio ya haraka. Tukiwekeza katika mafanikio ya muda mrefu, tunaongelea mafanikio ya wanetu, kizazi kijacho...
  • Serikali ianze kuwekeza katika miradi mikubwa si kama sasa ambapo hakuna Miradi yoyote mikubwa, japo itachukua muda mrefu lakini kizazi kijacho kitafaidi..
  • Ili kufanikisha haya naamini tunahitaji kukubali kuwa TUMESHINDWA ili tufumue mifumo yetu ya KISIASA, KIUCHUMI, KIELIMU, KIAFYA isukwe upya si kwa ajili yetu (Tuna miaka michache ya Kuishi) bali kwa Kizazi kijacho.
  • Na kadhalika na kadhalika
Kwa leo naishia hapa, nitaendeleza Makala hii, Kumbuka, Japo Mti mmoja hautengenezi msitu, msitu ulianza na mti MMOJA.

Anza kubadili maisha yako sasa!
 
Nimeielewa makala yako. Kwa ufupi ni kwamba nchi zetu zote za kiafrika kuna step fulani za kimaendeleo tumeruka. Huwa kuna msemo fulani wa kuruka step katika ukuaji wa mwanadamu.

Mfano, kama mtoto mdogo hakucheza ile michezo ya kitoto kwa sababu ya kubanwa na mazingira ya kimalezi, akikua tu akawa na uhuru atajitahidi kurudia yale mambo ya kitoto na hapo ndo unakutana na mtu mzima wa miaka kama 40 lakini anawakonyeza watoto wadogo wa shule ya msingi.

Sasa sisi kuna mambo ya kitoto kama taifa tunayafanya ambayo kwa kweli ni mambo ya kijinga wenzetu wanatuangalia wanaona tumeruka step. Mfano mzuri ni pale mtu anapopata madaraka hapa kwetu. Basi kwa vile tumekuwa masikini wa muda mrefu ukipata tu hiyo chance unaanza kufanya mambo ya ajabu.

Kiongozi wa umma kama waziri kusafiri business class wakati wa safari za nje wakati mwenzake wa Norway au Sweden anasafiri economy class, serikali kununua magari ya kifahari, flamboyant dress code kama wale wabunge mjengoni unawaona wamevaa makoti makubwa yanawazidi uzito hadi wanalala usingizi, kula mavyakula mengi kupita kiasi hadi kuoteana vitambi typical ya viongozi karibu wote wa umma; n.k

Haya japo yanaonekana ni mambo madogo lakini si ya kupuuza maana viashiria vya nje kuonyesha mfumo mbovu wa kufikiri kwa mtu binafsi au taifa kwa ujumla. Ukiona mtu anaanza maisha lakini anakimbilia kununua gari ya starehe kabla ya kununua kiwanja na ujenzi wa nyumba ujue huyo mtu anaruka step ya maisha.

Na ukiona taifa linanunua ndege ya rais na viongozi wake kutembelea business class wakati nyumbani kwao hawana umeme wala dawa hospitalini, hiyo si ni hatari zaidi?
 
Du! kazi kweli! Katika swala la utambuzi wa haki zako za msingi bado kuna kazi tena kubwa.
Kama bima ya afya pesa tunakatwa ukienda mahospital ndio balaa tena wewe mwenye kadi ndio haupati dawa kabisa,
Na mazingira tuliyonayo utaenda kumshitakia nani, jibu ni dawa hamna ukanunue.
 
Hongera kwa makala nzuri. Kwa historia ndogo ninayofahamu, sisi weusi tulikuwa mbele kimaendeleo dhidi ya mataifa ya weupe kabla ya Biashara ya pembe tatu ya antlatika(Trans Atlantic Slave/Triangular Trade) tangu biashara hii ilipoanza tumerudi nyuma sana kimaendeleo kulinganisha na nchi nyingine, kwa sababu tumeshindwa kubadilika kulingana na sayansi na teknolojia.

Hii biashara ya atlantiki ilianza muda ambao kulikuwa na vuguvugu la mapinduzi ya kiviwanda huko ulaya lakini sisi hatukubadilika tukabaki na teknolojia ileile ya kizamani hivyo pindi ilipoharibiwa na wazungu tukabaki hatuna chetu.

Pia naona Hali ya tabia nchi ya Afrika imetufanya tukkose changamoto mbalimbali za kimaisha ambazo watu wa ulaya walizipata hivyo ikabidi kupambana nazo waweze kustahimili maisha yao.

Kwa upande mwingine bado tunasumbuliwa na unafiki, uroho, upumbavu, ujinga, uoga na kutopenda kufikiri kwa kina. Nadhani mpaka hapo tutakapoadibishwa kutokana na tabia zetu ndipo tutabadilika
 
Du! kazi kweli! Katika swala la utambuzi wa haki zako za msingi bado kuna kazi tena kubwa.
Kama bima ya afya pesa tunakatwa ukienda mahospital ndio balaa tena wewe mwenye kadi ndio haupati dawa kabisa,
Na mazingira tuliyonayo utaenda kumshitakia nani, jibu ni dawa hamna ukanunue.
Hapo ndo tatizo liapoanza...Lack of Service Demand. Katika mfumo huu wa Kibepari, nguvu pekee aliyonayo mnyonge ni kumpigia kelele bepari hadi masikio yamuume ni lazima tu atatekeleza.

Hilo linakosekana kwetu, KUKOSA HAKI ZETU ZA MSINGI TAYARI IMEKUWA HAKI PIA! Yaani ukikosa dawa hospitalini unaona kama ni haki yako kukosa! Katika mfumo huu, Viongozi wataendelea kubweteka kwa kuwa wananchi tumebweteka. Ni kama darasani ukiwafundisha wanafunzi mbumbumbu wasioelewa kitu nawe mwalimu utalazimika tu kuwa mbumbumbu!

Ni viongozi wangapi wameingia madarakani na nyota ya matumaini lakini ghafla vitendo vyao vikaizima nyota ya Matumaini? Kwa kuwa sisi hatuwezi kudai kilicho haki yetu, viongozi hawawezi kutekeleza.

Siku tutakapoamua kudai, kila kona ya Tanzania...viogozi wataamka na wallah nchi hii itakuwa na neema, otherwise wataendelea kusinzia kwa kuwa sisi tuko usingizini!
 
Mkuu Tatizo kubwa tulilonalo Watanzania tulio wengi ni ubinafsi na hiki ndo kiini kikuu cha umasikini wetu. Ukifuatilia vizuri watu wengi wana tafsiri maendeleo kama ni kitu cha mtu mmoja mmoja na siyo jamii nzima, hii imetokana na ukweli kwamba watu wamekata tamaa na kadri miaka inavyokwenda watu wanapigania kujikomboa kimaisha "individually" ndiyo maana hata katika ofisi za umma utakutana na misemo ya kukata tama kama vile

1. "Nchii hii ilishajifia wee chukua chako mapema anza mbele"

2. "Matatizo haya yalikuwepo hata enzi za baba wa Taifa sembuse mimi/sisi?"

Kwenye namba moja hapo utagundua kutokana na roho ya ubinafsi, kweli mtu anaacha kufanya kazi kwa bidii na kwa uadirifu akiamini yeye kama yeye hawezi kuleta mabadiliko na hata kama anaweza kufanya hivyo basi hatanufaika nayo.

Kwenye namba mbili hapo ni mara nyingi sana viongozi tunaowachagua hupenda kutumia huo msemo kama defensive mechanism kwa kushindwa kututatulia matatizo tuliyonayo.

Ninaichukia sana roho ya kibinafsi, maana ndo chanzo kikubwa cha hali hii tuliyonayo,

Ni ubinafsi unaowafanya watu wafumbie macho maovu yanayotendeka serikalini kwasababu ya kuogopa kupoteza nafasi zao,

Ni ubinafsi ndiyo unao pelekea watu kuchakachua kura ili waendelee kuwepo madarakani hata kama uwezo wao ni mdogo na hawahitajiki tena na wananchi.

Ni ubinafsi ndiyo unaopelekea watu kukwepa kodi ili wao kama wao wapate maendeleo wakiyapuuzia maendeleo ya jamii nzima.

Ni ubinfsi ndiyo unaopelekea wizi wa rasilimali za nchi, kila kitu ni ubinafsi tu
 
Pia naona Hali ya tabia nchi ya Afrika imetufanya tukkose changamoto mbalimbali za kimaisha ambazo watu wa ulaya walizipata hivyo ikabidi kupambana nazo waweze kustahimili maisha yao.
Hapa kidogo nakubaliana na wewe, japo niseme changamoto tunazo, Mfano mzuri ni gonjwa la Ukimwi linalotafuna mataifa yetu.

Miaka fulani baada ya Vita ya Pili ya dunia, idadi ya watu Marekani iliongezeka sana kwa kuwa maaskari waliokuwa wamerudi toka vitani walanza kuzaliana, hii inaitwa 'Baby boom' .Serikali ya wakati huo kwa kutabiri ongezeko la watu ikaanza kupanua Infrastructure kwa kushirikiana na watu ili kuaccomodate generation itakayozaliwa. Upande wetu je?

Birth rate inaongezeka kila siku! Je kuna kiongozi anayetabiri ongezeko la watu tukapanua shule ,mahospitali, mfumo wa uzalishaji umeme, maji n.k?

Fikra zetu ni kusubiri tatizo lijitokeze ndo tuanze kutapatapa. Magari yanazidi ndo tunatapa tapa kuweka viraka vya barabara, ukame kutuchapa ndo tuanze kutapatapa kutafuta umeme wa ziada...........LACK OF VISION!

Si Viongozi si Wananchi wote Tumekosa Vision! Macho yetu huishia kuona Leo badala ya kesho,keshokutwa na mtondogoo. Katika ngazi ya familia, baba anazaa watoto pasipo kupanua nyumba au shamba, pasipo kujua kuwa kama ni mkulima kwa kila mtoto mmoja unayemuongeza unahitaji kuongeza zaidi ya hekari 2, Watu wangapi vijijini wameoa wake zaidi ya mmoja but akiwa na nyumba moja?

Nimeyaona hayo! Shule, Vyuo vinaongeza intake ya wanafunzi kabla ya kupanua miundo mbinu, Chuo cha Muhimbili mfano kilijengwa kuaccomodate wanafunzi 50 sasa kina Maelfu kwa miundombinu ileile na kujikongoja kupanua miundo mbinu taratibu.

Kwa Sababu tumekosa vision na kubaki kuwa responders after the Problems, Tumejikuta hata response zetu haziwezi kumeet mahitaji yetu. Kwa mfano tatizo la mikopo kwa wanafunzi ni kutokana na serikali kuongeza idadi ya wanafunzi pasipo kupanua bajeti ya board.

Acha niongelee indicators, Juzi raisi wa CCM alikuwa anajitap kuwa tumepunguza idadi ya vifo vya akina mama...Yes kwa target yetu ni ni performance INDICATORS na siyo process indicators. Je unadhani kuwa idadi ya vifa vya akina mama imepungua AU Tumeongeza ubovu wa kutorepoti Vifo vya akina mama?

Mimi kama mtaalamu wa afya ya Binadamu na ya Jamii najua kuwa ili useme umepunguza vifo ni lazima uwe na mfumo bora wa kurepoti taarifa. Kwa sasa Manesi na Madaktari wetu wamechoka na Maisha na kelele, si ajabu kuona mama kafariki na hawajadocument. Kwa kuwa tuna Poor documentation basi yaonekana vifo vimepungua.

Sababu nyingine ni idadi kubwa ya wamama wasiozalia hospitalini! Uliona response ya watu kwenda Loliondo..Its because people has no faith withour hospitals. Kwa kuwa huduma imekuwa mbovu na ukosefu wa dawa ktk dispensary za vijijini, kuzalia nyumbani ni bora kuliko kuzalia hospitalini. Yet tunajisifu kuwa tumepunguza idadi ya vifo vya akina mama..uhuni mtupu.

Kwa ufupi ni kwamba we need visionary people. Sisi wenyewe tuanze kuwa na Vision kabla ya kuwataka viongozi wawe na vision na pengine kwa kuwa sisi tumeshindwa , labda ni vema tuwafundishe wanetu kuwa na vision!

Kwamba tuinvest katika kizazi kijacho....
 
nakubaliana na makala yako! Nasikia huwa kuna msemo miongoni mwa wahindi wekundu(native American) eti wazungu walikuja na biblia na kuwapa hao wahindu wakati wakipeluzi kwenye biblia kutahamaki walikuta ardhi nzuri imekwapuliwa na wazungu. The same stituation pia kwetu: biblia na korani zimepukutisha uwezo wetu wa kutumia mind, unaona jiafrika zima linatamani kuwa mwarabu au mzungu. Fikra pana huanzia jinsi unavyojitazama! Kama unajiona mwarabu au mzungu wakati sivyo hata wembe hutaweza kuutengeneza
 
Umeandika article nzuri. Sema kuna issue moja ambayo inabidi uifanunue zaidi. Umesema watu weusi wa Marekani hawatumii benefit ambazo wanazipata kutoka serikali yao, je una argue kwamba besides other factors, race ya kuwa black pia ni issue inayosababisha umaskini?
 
Umesahau kuwa dunia hii inaendeshwa na mfumo wa NWO (new world order)

Kitu unavyokiona (appearance) ni tofauti na Reality (ukweli) ulivyo???

Mfano uchumi (resources) wa nchi za Afrika na Middle east unatakiwa usaidie hao (NWO) vinginevyo utapewa jina baya sana mkuu..

Ili kufanikisha wanakuleteeni Policy (WB, IMF, etc) ambazo lazima mzifuate au upate kichapo (Sadam, Qadafi, Mugabe etc) are examples..

Ili kufanikisha wanakuletea siasa na vyama vya jamii (hiyo kitu inasaidia sana kuwagawanya wananchi forever!)

Kizazi hiki kimeshikwa pabaya..hawaruhusiwi kutengeneza gari mkuu toyota hawatakubali alijaribu nyerere unajua mwisho wake..
 
Mtulutumbi article yako ni nzuri sana, umeainisha karibu kila kitu kilichofanya tuwe mafukara wa kupindukia. Ni kweli tatizo ni kubwa sana maana halihitaji kufahamu tu yanayo tusibu, inahitajika kuyafanyia kazi, wewe mwenyewe umekiri kuwa wajapani wasifa ya kutokata tamaa lakini wewe mwenyewe umeanza na heading ya kukata tamaa kuwa sisi tumeshindwa kwahiyo tuandae kizazi kijacho hii inathibitisha tatizo ni kubwa sana.
 
Mtulutumbi article yako ni nzuri sana, umeainisha karibu kila kitu kilichofanya tuwe mafukara wa kupindukia. Ni kweli tatizo ni kubwa sana maana halihitaji kufahamu tu yanayo tusibu, inahitajika kuyafanyia kazi, wewe mwenyewe umekiri kuwa wajapani wasifa ya kutokata tamaa lakini wewe mwenyewe umeanza na heading ya kukata tamaa kuwa sisi tumeshindwa kwahiyo tuandae kizazi kijacho hii inathibitisha tatizo ni kubwa sana.

Yap, Buza, Tatizo ni kubwa kuliko watu wanavyofikiria. Kwa hatua tulofikia ya usugu wa tatizo ni vigumu kupata Tiba. Yani Tanzania inahitaji KUBATIZWA na Kuzaliwa UPYA, tena ule Ubatizo wa Kisabato wa Kuzamishwa kwenye maji! Hope pekee tuliyonayo ni kuwekeza katika kizazi kijacho, watoto wetu! Wafundishwe tulipotoka! Wafundishwe tulipokosea! Wafundishwe wajue kwa nini sisi hatuwezi kuchukua hatua kuifanya Tanzania nchi ya Neema!Wafanye Mapinduzi ya Fikra na actions katika minds zao. SisI Tumeshindwa, Hatuwezi kuibadili system inayotuongezea umasikini kila siku.............Tumeshindwa!
 
Mtulutumbi, Nakubaliana na wewe;
Tatizo la msingi ni mfumo wetu wa fikra- thinking paradigm imekaa vibaya. Mbaya zaidi, mfumo wetu wa elimu kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu unahitaji mabadiliko makubwa sana. Hakuna somo la uzalendo ambayo ni muhimu sana kuondoa ufisadi, uvivu nk. Ufisadi unafilisi nchi na kurudisha ukoloni mambo leo kwa kasi. Kizazi kinashindwa kweli. Hakuna somo la ujasiriamali ili hata hao watanzania wachache walioajiriwa au wanaojiari wajue jinsi ya kutumia hizo fedha zao vizuri waachane na umasikini. Badala yake waajiriwa wanasubiri kustaafu, na mwenye duka lake moja ( aliyejiajiri) hasogei mblele.
Ikumbukwe kuwa walioajiriwa na ambao ni wahitimu wa chuo kikuu walipaswa wawe wanaacha ajira mapema ili wajitegemee baada ya kupata uzoefu- ndiyo maana ya degree ya pili ya masters - Unajiajiri ktk kile unachomaster na kuajiri wengine. Tanzania yetu masters inasomwa kwa lengo la kuongeza mishahara. Je, ikiwa wahitimu wenye degree moja, mbili ( masters) na tatu ( PHD) nao wanatafuta ajira nani wa kuwa ajiri? Kama wenyewe hawawezi kutumia rasimali zilizopo kujiajiri na kuwaajiri watz wengine ina maana kwamba lazima wazungu waje waanzishe biashara zao ( vodacom, TIGO, wanunue TBL na kuchukua ardhi yetu) ili hao wasomi waajiriwe na wazungu hao. Hili nalo ni tatizo lingine - chanzo cha umaskini. Tatizo ambalo chanzo chake kimejikita ktk mfumo wa elimu usiomkomboa mwanadamu kifikra.
Nahitimisha kwa kusema ili tuanze upya na kizazi kipya tuanze kubadilisha maudhui ya elimu yetu.
 
Tz Kila mtu analalamika.
Viongozi wanalalamika, wabunge wanalalamika, wanazuani wanalalamika, wanafunzi wanalalamika, wafanyakazi wanalalamika, wakulima wanalalamika, wafanyabiashara wanalalamika, wanasiasa wanalalamika.

Sasa nani atamsikiliza mwenzake?
 
Mtulutumbi, Nakubaliana na wewe;
Tatizo la msingi ni mfumo wetu wa fikra- thinking paradigm imekaa vibaya. Mbaya zaidi, mfumo wetu wa elimu kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu unahitaji mabadiliko makubwa sana. Hakuna somo la uzalendo ambayo ni muhimu sana kuondoa ufisadi, uvivu nk. Ufisadi unafilisi nchi na kurudisha ukoloni mambo leo kwa kasi. Kizazi kinashindwa kweli. Hakuna somo la ujasiriamali ili hata hao watanzania wachache walioajiriwa au wanaojiari wajue jinsi ya kutumia hizo fedha zao vizuri waachane na umasikini. Badala yake waajiriwa wanasubiri kustaafu, na mwenye duka lake moja ( aliyejiajiri) hasogei mblele.
Ikumbukwe kuwa walioajiriwa na ambao ni wahitimu wa chuo kikuu walipaswa wawe wanaacha ajira mapema ili wajitegemee baada ya kupata uzoefu- ndiyo maana ya degree ya pili ya masters - Unajiajiri ktk kile unachomaster na kuajiri wengine. Tanzania yetu masters inasomwa kwa lengo la kuongeza mishahara. Je, ikiwa wahitimu wenye degree moja, mbili ( masters) na tatu ( PHD) nao wanatafuta ajira nani wa kuwa ajiri? Kama wenyewe hawawezi kutumia rasimali zilizopo kujiajiri na kuwaajiri watz wengine ina maana kwamba lazima wazungu waje waanzishe biashara zao ( vodacom, TIGO, wanunue TBL na kuchukua ardhi yetu) ili hao wasomi waajiriwe na wazungu hao. Hili nalo ni tatizo lingine - chanzo cha umaskini. Tatizo ambalo chanzo chake kimejikita ktk mfumo wa elimu usiomkomboa mwanadamu kifikra.
Nahitimisha kwa kusema ili tuanze upya na kizazi kipya tuanze kubadilisha maudhui ya elimu yetu.

Uko Sahihi Mkubwa Aweda
Pengine tuna Tatizo la Kimsingi zaidi kuliko Mfumo wa Elimu. Hata kama tukiubadili Mfumo leo hatutapata mafanikio kwa kuwa hata kama tkiubadili mfumo na wahitimu wanaenda kufanya kazi katika mfumo uliocollapse ni lazima nia zao njema zitakuwa Transformed kuwa za Kifisadi. Ni vigumu kuwa mwadili wakati mfumo wetu wa kimamlaka unakusukuma upokee au kutoa Rushwa ili ufanikiwe.
Thats why nikasema thinking yetu ina matatizo lakini pia mfumo wetu wa kiutawala una Matatizo. Tanzania hii tunaishi kitumwa pasipo kujijua. Tunahitaji Kuibatiza nchi hii, tena ubatizo wa kuzamishwa katika maji izaliwe upya. Izaliwe upya katika kwa kubadili system ya Utawala, Kustructure upya kila kitu, sera za uchumi, afya, elimu, mahakama, ulinzi..kila kitu. Vitu vyote hivi vinategemeana na kila kimoja kinaathiri kingine. Iwapo tunahitaji mabadiliko ya kweli lazima tukae chini na kuisuka upya system ya nchi hii from zero. Ili kumwezesha daktari atibu kwa uhakika, engineer ajenge kwa moyo na akili thabiti, hakimu ahukumu kwa haki, polisi alinde usalama na haki mkulima alime kwa bidii, mfanyakazi afanye kazi kwa uhakika............. Kwa sababu hata tukibadili katika lakini mfumo wa utekelezaji wake ukawa ni huu huu wa sasa....Tunaendelea hivi hivi!
 
Tz Kila mtu analalamika.
Viongozi wanalalamika, wabunge wanalalamika, wanazuani wanalalamika, wanafunzi wanalalamika, wafanyakazi wanalalamika, wakulima wanalalamika, wafanyabiashara wanalalamika, wanasiasa wanalalamika.

Sasa nani atamsikiliza mwenzake?

Mkubwa Barubaru..Kulalamika ndo mwanzo wa Mabadiliko, It means watu wanaelewa matatizo yaliyopo.
 
Nani kakwambia tumeshindwa? ukweli ni kwamba imechukua muda mrefu kujitambua.Kwa sasa watanzania wamehamasika sana na ndiyo maana sasa hata idadi ya activists (wanaharakati) imeongezeka.Swala ni kwamba viongozi wetu walitanguliza ubinafsi kwa kufanya ufisadi mkubwa hata kufanya rasilimali za nchi hii kuchotwa na watu wachache.Ieleweke kwamba kwa sasa watanzania wameamka na wanachukua hatua za kusimamia rasilimali za watanzania.Chukua mfano mdogo tu kwa watanzania kuchoka wale wanaoibua maovu au ubadhirifu wa rasilimali za nchi ni wale walio maofisini wanakotokea vigogo mafisadi,hii ni commitment kubwa yenye risk ndani yake,lakini wanajitoa kufichua maovu haya.
 
Nani kakwambia tumeshindwa? ukweli ni kwamba imechukua muda mrefu kujitambua.Kwa sasa watanzania wamehamasika sana na ndiyo maana sasa hata idadi ya activists (wanaharakati) imeongezeka.Swala ni kwamba viongozi wetu walitanguliza ubinafsi kwa kufanya ufisadi mkubwa hata kufanya rasilimali za nchi hii kuchotwa na watu wachache.Ieleweke kwamba kwa sasa watanzania wameamka na wanachukua hatua za kusimamia rasilimali za watanzania.Chukua mfano mdogo tu kwa watanzania kuchoka wale wanaoibua maovu au ubadhirifu wa rasilimali za nchi ni wale walio maofisini wanakotokea vigogo mafisadi,hii ni commitment kubwa yenye risk ndani yake,lakini wanajitoa kufichua maovu haya.

Uko Sahihi, huu ni mwanzo Mzuri,lakini tunahitaji zaidi ya kujitambua..Bado sis kwa sisi tunabishana, hatuna Umoja,hatuaminiani, Inapofikia kuchukua maamuzi hao hao waliotoa data wnarudi nyuma, in that case we can't make a 'significant' Change. Mabadiliko ya kweli yako mbele saana mkuu, si leo, si kesho, ni kizazi kijacho iwapo tutawekeza katika kupandikiza hisia za kweli za uzalendo na uoga wa kuwasaliti walio wengi katika mioyo ya wanetu..
 
Mkubwa Barubaru..Kulalamika ndo mwanzo wa Mabadiliko, It means watu wanaelewa matatizo yaliyopo.

nafikiri ujanifahamu.

Suala langu hapo ni nani atamsikiliza mwenzake?

Yaani kama wote mnalalamika na kupiga kelele nani atamsikiliza mwenzake.

Njia sahihi sio kulalama bali ni kuangalia mmejikwaa wapi kisha kusonga mbele kwani siku zote in order to build something strong it helps to start with BEST and POSSIBLE materials. Na vyote mnavyo sasa mmepotea wapi?


 
Back
Top Bottom