Kwako Waziri Bashe: Je, mpango wa kuwakopesha wakulima fedha za kuendeshea shughuli za kilimo kupitia Mfuko wa Pembejeo upo kama ulivyotuaminisha?

VYEMELO

JF-Expert Member
Jul 21, 2020
348
459
Salaam aleikum!

Nitumie fursa hii kukupongeza kwa kazi nzuri unayoifanya. Nikiri kwamba Wizara ya Kilimo imekuwa na mawaziri wengi, lakini wewe, umekuwa tofauti kwa uchapakazi wako. Maono na mipango ya Wizara unayosimamia unawagusa wakulima wa ngazi zote hususan wa ngazi ya chini na kati.

Wizara ya Kilimo ni ngumu kuiongoza na hasa ukitilia maanani ndiyo iliyobeba mzigo mzito wa kuhakikisha usalama wa chakula nchini, kusapoti uchumi wa Nchi kwa takriban 40%, kutoa ajira kwa zaidi ya 70% ya Watanzania, na kadhalika.

Serikali imekuwa ikijitahidi kuhakikisha sekta ya kilimo inaimarika kwa kuweka ruzuku na kuimarisha huduma za ugani kote Nchini. Hata hivyo, pamoja na jitihada nzuri hizi, zipo changamoto zinazozorotesha maendeleo ya Kilimo Nchini; na, mojawapo ya changamoto muhimu ni watendaji ktk Wizara hii pamoja na Taasisi nyingine muhimu ktk kusapoti kilimo kama zile za kifedha zilizo na wajibu wa kuhakikisha upatikanaji wa mitaji hasa kwa wakulima wadogo na wale wa kati ambao kwa kweli ndio wanaoibeba sekta kwa zaidi ya 85%.

Waziri mhe: Bashe, tangu kuteuliwa kwako umeonesha nia ya dhati ya kukabiliana na changamoto hii ya ukosefu/upungufu wa mtaji kwa wakulima. Nakumbuka 2021 ktk ziara yako mkoani Rukwa uliwahakikishia wakulima juu ya upatikanaji wa mikopo yenye riba nafuu ili wawe na uwezo wa kuzalisha kwa tija kubwa. Tunashukuru Mheshimiwa Rais Samia aliunga mkono maono yako kwa kuziagiza benki kutoa mikopo kwa wakulima na wafugaji wadogo na wale wa kati yenye masharti na riba nafuu, kwamba, riba kwa makundi haya ishushwe kutoka zaidi ya digiti moja, iwe digiti 1.0 tu. Benki zilitii.

Nimehakikisha hili ktk benki ya NMB na hata kwenye mifuko kama Mfuko wa Pembejeo.

Changamoto kubwa ni upatikanaji wa mikopo hii Mheshimiwa. Hali ni kinyume kabisa na mlivyopanga, haiyumkiniki. Kuna urasimu wa hali ya juu mno ktk utoaji wa mikopo hii. Ukifuatilia sana, kuna harufu ya wazi ya utoaji wa mikopo hii.

Serikali ilikuwa wazi wakati ikitujulisha wakulima na wafugaji juu ya mikopo hii. Tunachokutana nacho sasa tunapokwenda kuomba mikopo hiyo, utashangaa!
Kama ndiyo huo Mfuko wa Pembejeo, utachanganyikiwa majibu unayokutana nayo. Wenye Mfuko huko Dar sijui Dodoma wanatujibu kuwa, .... Hakuna mpango kama huo; hizo ni siasa tu. Ati Ni kauli zenu Wanasiasa. Je, ni kweli Mheshimiwa Bashe?

Uwe na tahadhari mheshimiwa, Wizara hii kama nilivyotangulia kusema, Ni ngumu kuliko unavyoweza kufikiri. Usiichukulie poa. Je, unakumbuka sakata la Pembejeo za Ruzuku mwaka 2015 kurudi nyuma? Serikali inaweka mabilioni ya pesa kuruzuku kilimo kwa ajili ya wakulima wadogo vijijini, wataalam wachache "wajanja" (wezi) wanatengeneza masharti yenye utata utakaosababisha wanufaika (wakulima); kushindwa kunufaika, Kwa lengo wachote pesa hizo za wanyonge. Na walizichota kweli kabla marehemu JPM hajawashtukia.

Mfuko wa Pembejeo; unaandika Andiko la mradi, unajaza fomu ya Mkopo, na kila kitu kwa kadiri ya maelekezo na kutuma kwa anwani zilizo kwenye kipeperushi chao wenyewe; Hakuna majibu. Unawapigia simu, majibu ndiyo hayo.

Waziri Bashe, kwa waraka huu wakulima tunaomba utujulishe, Je, mpango wa kuwakopesha wakulima fedha za kuendeshea shughuli za shamba (kilimo) kupitia Mfuko wa Pembejeo upo kama ulivyotuaminisha wakulima wako? Nasikitika niliwasiliana nawe kupitia akaunti yako ya Instagram, hukunijibu. Nilishangaa pia kwani kwa ninavyokuelewa Mheshimiwa, kamwe hauko hivyo.

Kuna wakulima walijaza fomu za mkopo kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji 2018 mkoa flani,,,toka zile fomu ziende mpaka leo wale wakulima wanasubiri majibu.
 
Back
Top Bottom