Kwako kuna kura ngapi za Lowassa na UKAWA?

Kwako kuna kura ngapi za Lowassa na UKAWA?

Jamani watanzania hebu kuweni watu wa vitendo zaidi na si maneno mengiiiii!

Mimi hapa kwangu kuna kura NNE safi za lowassa na ukawa! Mimi na wanangu wawili ni tangu mwanzo, kura ya mke wangu ilisumbua sana maaana miaka yote haoni umuhimu wa kupiga kura. Nilimuuzia Sera zote akazipangua.
Mwishoe nikamwambia kuwa sasa atafute pesa za michango ya shule, maana mimi nimechoka kulipa ndiyo maana nimeamua kuwachagua wale wanaotoa elimu bure bila michango.
Wee! mbona aliulizia Siku ya kupiga kura! Sasa ana munkari baraa!
Wewe kwako kuna kura ngapi?

Kwani siku ya kupiga kura wewe ndo unampigia mkeo? Si anapiga mwenyewe? Acha kujitoa ufahamu
 
mimi kama arobaini hivi, ndo raha ya kufundisha tuishieni.
 
Mke wangu,mimi mwenyewe na wadogo zangu wawili.Pia robo tatu ya ukoo wangu ni wahanga wa Sisiem kwa hiyo hizo zote ni za UKAWA.
 
Kwani siku ya kupiga kura wewe ndo unampigia mkeo? Si anapiga mwenyewe? Acha kujitoa ufahamu

Jibu lako rahisi sana hakuna cha kujitoa ufahamu kuna kitu kinaitwa LOYALTY.
 
Back
Top Bottom