Thread haijauliza za ccm, soma uelewe
Kwangu ziko tatu japokuwa mbili za wazazi wangu ziliingia matatani baada ya slaa lakini nimefanya kazi kubwa kuwaelimisha juu ya ulaghai wa CCM kwamba hawapaswi kutoa ahadi wanapaswa kutoa majibu ya kero za wananchi na wanaposhindwa kuzitatua katika ustaarabu wa kawaida wanapaswa watoe sababu lakini hawafanyi hivyo badala yake wanajazia ahadi juu ya ahadi kitu ambacho wamenielewa ila shida nyingine ambayo imenipata tena "LATEST"ni kwamba MUUZA NYUMBA amewatishia vita sasa na kazi tena kuwaelimisha ya kuwa kubadilisha chama katika sanduku la kura hakuna cha vita ni utamaduni tu wa kawaida katika demokrasia na duniani nchi nyingi zimefanya hivyo bila vita project ambayo naendelea nayo hata sasa wanahofu hata ya kupiga kura ila nitahakikisha nashinda mtihani huu mgumu alioniletea MUUZA NYUMBA na amezidisha hasira zangu dhidi ya hilo lichama.
Kwangu na nyumba yote zipo 8 ila ya wife ina mashaka ila nitamuazima kwa lazima kichinjio chake. hakuna namna nitamuibia kwa tarehe 25 tu.nitarudisha kesho yake.
Jamani watanzania hebu kuweni watu wa vitendo zaidi na si maneno mengiiiii!
Mimi hapa kwangu kuna kura NNE safi za lowassa na ukawa! Mimi na wanangu wawili ni tangu mwanzo, kura ya mke wangu ilisumbua sana maaana miaka yote haoni umuhimu wa kupiga kura. Nilimuuzia Sera zote akazipangua.
Mwishoe nikamwambia kuwa sasa atafute pesa za michango ya shule, maana mimi nimechoka kulipa ndiyo maana nimeamua kuwachagua wale wanaotoa elimu bure bila michango.
Wee! mbona aliulizia Siku ya kupiga kura! Sasa ana munkari baraa!
Wewe kwako kuna kura ngapi?
Wizi tena