JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 677
- 1,098
Zoezi la Uandikishaji Wananchi watakaoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024 limekamilika ambapo kwa mujibu wa TAMISEMI, takriban Watu Milioni 32.9 (94%) wamejiandikisha
Kwako Mdau, una mtazamo gani kuhusu zoezi hilo lilivyoendeshwa ikiwa ni takriban mwezi mmoja umesalia kuelekea siku ya Kupiga Kura?
Ungana nasi leo Oktoba 31, 2024 Saa 12:00 Jioni kupitia XSpaces ya JamiiForums ambapo tutapokea maoni ya Wananchi katika Mjadala utakaoangazia Mchakato Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu.
Mwongoza mjadala: Chief Edwin Odemba - Mwandishi wa Habari/Mtangazaji
WAZUNGUMZAJI
1. Idd Mkanza - Katibu Mtendaji Jumuiya ya Vijana CUF
2. Jebra Kambole - Wakili wa Kujitegemea
3. Askofu Maximillian Machumu - CHADEMA
4. Mbarala Maharagande - Katibu wa Haki za Binadamu ACT Wazalendo
5. Bob Chacha Wangwe - Mkurugenzi Mtendaji Jukwaa la Katiba Tanzania (JUKATA)
Kushiriki mjadala Ingia x.com
IDD MKANZA (Katibu Mtendaji Jumuiya ya Vijana CUF):
Mchakato wa Uandikishaji haukwenda vizuri, sisi CUF tumezungumza kuwa hakuna dhamira njema, mfano kule Newala kuna Viongozi wetu walikamatwa na kumekuwa na changamoto inayowahusu Wapigakura
Handeni, Tanga kulikuwa na kupishana kwa idadi ya Wapigakura waliojiandikisha na wale ambao majina yao yalibandikwa, ilikuwa hivyo pia hata Bagamoyo (Pwani)
Ukitazama takwimu za Wapiga Kura zilizotolewa na TAMISEMI na zile Takwimu za Sensa 2022 zinapishana, mbali na hapo kuna Mawakala ambao wamekuwa wakizuiwa kusaini licha ya kuwa Kanuni inaelekeza hivyo, kuwa wanatakiwa kusaini muda wa kufungwa kwa uandikishaji
Kuna Wasimamizi wa Uchaguzi walikuwa wanapokea majina kwenye simu wengine walikuwa wanakwenda nyumbani kuwafuata Watu, hayo yote yanaonesha zoezi la Uandikishaji liliharibika
Ishara ya kilichotokea katika Uandikishaji wa Daftari la Kupiga Kura ni mbaya. Nikumbushe jambo, Mwaka 2014 kulikuwa na mwamko mkubwa wa Watu kujiandikisha tofauti na ilivyo Mwaka huu (2024)
Mwaka huu (2024) vituo vingi vimekuwa vikavu, hakuna Watu lakini baadaye kwenye orodha ya majina inaonekana majina ni mengi, yametoka wapi? Inamaanisha kuna Watendaji waliofanya kinyume cha taratibu kwa kuandikisha Watu ambao hawakidhi vigezo
Mazingira ya Uandikishaji yanaonesha hakukuwa na uhalisia kulikuwa na Watu wengi wasio na sifa wakiwemo wenye umri chini ya Miaka 18, mwamko pia ulikuwa upo chini
Newala Vijijini (Mtwara), nusu ya Wasimamizi wa Uchaguzi hawakuwepo kwenye Vituo vyao
Tulipokuwa tunaulizia Viongozi wao wa juu wakisema wengine wapo katika majukumu mengine lakini ilionekana wazi kuwa Watu hawakuwa na hamu ya kupiga kura
Rais ameleta 4R lakini utendaji wa Watendaji wake hauendani na anachokitaka Rais
Kuna sehemu nilizungumza na Mkurugenzi (siwezi kutaja sehemu) alikuwa hafurahishwi na baadhi ya mambo, nadhani hizi 4R za Rais ambazo amezihutubia akiwa na dhamira ya dhati ikiwezekana kuwe na maelezo ya nini hasa ambacho anakitaka kiongozi wa Nchi
Kuna Watu wa huku chini ndio ambao wameharibu mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, mfano kule Mbeya Viongozi wetu waliambiwa wato ‘copy’, hilo ni jambo dogo lakini linaonesha jinsi ambavyo vitu vingi havipo sawa
WILLIAM (Mdau):
Takwimu zilizotolewa na TAMISEMI zinaonesha kuna ongezeko la Wapigakura waliojiandikisha, ni jambo zuri lakini tunatakiwa kuwa na takwimu sahihi
Muhimu zaidi tunachotakiwa kufanyika ni kuwapa elimu Wananchi ili waweze kushiriki kwa kuwa wao ndio wanaofanya maamuzi kupitia Kura wanazopiga
Licha ya upungufu uliojitokeza kwenye mchakato wa Uandikishaji bado tunatakiwa kutoa wito kwa Wananchi kujitokeza na kufanya maamuzi kupitia Kura
Askofu Maximillian Machumu (CHADEMA)
Uandikishaji ulivyoanza sisi kama Chama tulipinga ikiwemo kufanya maandamano Nchi nzima, lengo lilikuwa ni kutaka TAMISEMI wasisimamie uchaguzi huo kwa kuwa kusingekuwa na Haki
Baada ya yote yaliyotokea tukakubaliana kuwa hatuwezi kususia kushiriki kwa kuwa kwa Katiba hii na TAMISEMI hii tuliwahi kushinda katika chaguzi zilizopita
Tumeshuhudia Daftari la Kupiga Kura limekuwa na mizengwe mingi ambayo inaonesha Uchaguzi hautakuwa salama
Jambo zuri katika maandalizi haya ni kuwa wametangaza na kuweka mabango sehemu nyingi kama Kanuni zinavyoelekeza lakini wanachokiuka ni kuandikisha Watu wasio na vigezo vya kupiga Kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
Kuna watu wamejiandikisha zaidi ya mara moja kwa kuwa Daftari lilikuwa halina nafasi ya kuonesha huwezi kujiandikisha katika zaidi ya Kituo kimoja
Kuna Kituo waliandikisha Watu zaidi ya 200 lakini majina yaliyoandikishwa yalikuwa zaidi ya 600 hadi Watu wa Mtaa husika wanajiuliza hao watu wengine wametoka wapi
Kuna sehemu walikuwa wanachukua daftari la majina ya Wanafunzi na kwenda kuhamisha kwenye Daftari la Kupiga Kura
ISIHAKA MCHINJITA (Makamu Mwenyekiti ACT Wazalendo - Bara)
Kuna matukio ambayo sio ya bahati mbaya kwenye Uandikishaji na hatukuona kama TAMISEMI wakionesha mwitikio, kitu ambacho kinaonesha hawana dhamira ya kweli
Kuna maeneo ambayo Msimamizi ameandikisha Mtu ambaye amefariki na Msimamizi Msaidizi akakiri, unajiuliza hilo jina liliandikishwaje?
Inawezekana Waandikishaji walikuwa wanaorodhesha tu Watu, hali kama hiyo ndio iliyotufanya kuaminia TAMISEMI sio sehemu sahihi au Watu sahihi wa kusimamia zoezi hilo la Uandikishaji wa Daftari la kupiga Kura Serikali za Mtaa
Mwaka 2014 kulikuwa na mwamko mkubwa wa Kisiasa, Haki za Kidemokrasia zilikuwa zinapatikana kuliko ilivyo leo, hakukuwa na vitisho kwa Watu, mambo ya Watu wasiojulikana hayakuwepo
Hivyo, kusema leo watu wanamwamko mkubwa wa kujiandikisha ni kujidanganya
TAMISEMI haina uwezo wa kusimamia uchaguzi huu kwa kuwa wanaonesha wana upande mmoja
Jambo lingine kuna upungufu wa makosa ya kudhamiria na sio ya Kibinadamu, mfano Newala kuna Watendaji wanaosimamia hawakuwepo vituoni, mwingine walimkuta Msimamizi akasema subiri narudi, baada ya hapo hakurudi tena na simu hapokei
Mahakama kuipa TAMISEMI kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni kukatisha tamaa Demokrasia
Ujio wa Tume Huru ya Uchaguzi ilimaanisha lazima kuwe na chombo huru cha kusimamia uchaguzi, hivyo kilichofanywa na Mahakama ni sawa na kupiga rungu Demokrasia na tunaingia kwenye wakati mgumu sana, tunalazimika kuongea na TAMISEMI kuhusu matatizo ambayo tuliyatabiri yatatokea
NTEGHENJWA HOSSEAH (TAMISEMI):
Tumepokea maoni na ushauri wa Wadau, huko siku za nyuma Uchaguzi ulikuwa unafanyika lakini Uandikishaji ulikuwa chini, mfano Mwaka 2014 waliijiandikisha walikuwa Milioni 11, Mwaka 2019 waliojiandikisha walikuwa wengi hadi siku zikaongezwa baada ya ile za awali kukamilika
TAMISEMI haiwezi kuwa na takwimu ambazo sio sahihi, kwa namna ambavyo ofisi hii ina majukumu makubwa haiwezi kutengeneza takwimu
Takwimu ambazo zinapatikana TAMISEMI ndio zile ambazo zinapatika katika Mamlaka nyingine za Takwimu za Serikali
Kuhusu madai kuwa kuna Watu wameandikishwa wasiokuwa na sifa, Kanuni zipo wazi kuwa kuna muda wa mapingamizi baada ya mchakato wa Uandikishwaji wa Wapiga Kura ambapo wanaweza kuwasilisha vielelezo vyao kwa ajili ya kuweka pingamizi
TAMISEMI: Kuhusu suala la TAMISEMI kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni kuwa Sheria inatupa mamlaka ya kusimamia uchaguzi huo
Wadau wanatoa maoni na wanaendelea kutoa mapendekezo yao, inawezekana miaka ijayo mambo yanaweza kubadilika lakini kwa sasa hatuwezi kusema tusisimamie wakati Sheria na Kanuni zinatutaka kusimamia Uchaguzi
Jukumu la kusimamia Uchaguzi sio kwamba tunajipa wenyewe bali ni miongozo iliyopo kwenye Sheria
Uandikishaji wa Daftari la Wapiga Kura wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulikuwa unafanywa katika levo ya chini ya Mamlaka ya Serikali za Mtaa, kwenye Mitaa na Vijiji vingi tunavyoishi tunafahamiana
Inapotokea mtu ana shaka ndipo linapokuja suala la kitambulisho ambalo linatakiwa kuendana na lile lililoandikwa
Kuhusu kufuata Waandikishaji nyumbani wahusika waliafikiana kufanya hivyo baada ya majadiliano lakini baada ya malalamiko na maoni ya Wadau hilo likafanyiwa kazi na ikaelekezwa wanaotakiwa kujiandikisha waende kwenye vituo na sio kuwafuata
Jina na utambulisho wa Mpiga Kura linapotiliwa shaka wakati wa Uandikishaji, Msimamizi anayo nafasi ya kutumia nafasi yake kuhitaji utambulisho wa Mhusika kwa maana ya vitambulisho ambavyo vinatakiwa kuendana na majina na utambulisho wake alioandika kwenye daftari
Wanaolalamika kuhusu Uandikishaji wa Daftari la Kupiga Kura Serikali za Mitaa ni wachache na wanajulikana wanatokea upande gani lakini haina maana maoni na mapendekezo yanayotolewa tunayachukulia poa, tunayazingatia na ndio maana baadhi yanafanyiwa kazi
Maoni ya kuwa Uandikishaji unatakiwa kuhamia Kidigitali tunaupokea, inawezekana Chaguzi zinazofuata tunaweza kuhamia huko kwa kuwa tunaweza kuwa katika nafasi nzuri ya Teknolojia zaidi
SHANGWE AYO (Naibu Katibu wa Habari na Uenezi wa ACT):
Mchakato huu wa uchaguzi hautoi njia ya kuwa kuna uhuru na haki, kuna matikio mengi ambayo yanafanyika ndivyo sivyo, kuna baadhi ya Shule zimetumia daftari la mahudhurio kwa ajili ya kuandikisha majina
ACT tutashiriki Uchaguzi lakini kuna makandokando mengi, TAMISEMI haikuwa na uhalali wa kushiriki kusimamia Uchaguzi huu
Mimi nipo Arumeru Mashariki huku kwetu fomu zinatolewa kwa kutoa ‘copy’, kuna baadhi ya Watendaji wanatueleza kuwa kama Wapinzani wakionekana kutawala Jimbo tunaweza kukosa misaada na vitu kama hivyo
ACT Wazalendo tumejiandaa kutoa Wagombea kila Kijiji na kila eneo katika Uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa japokuwa kuna viashiria kuwa kuna chama fulani kimeandaliwa kushinda
Safari hii hatutakuwa lelemama kama ilivyokuwa siku za nyuma
SHASHI JOHN: MDAU
Zoezi la Uandikishaji liliwa la wazi, majina yamebandikwa na kila kitu kipo wazi, kitu kizuri ni kuwa mchakato ulifanyika kwa ngazi ya Kitongoji ambacho Wananchi wanajuana
Waliokuwa na pingamizi walikuwa na nafasi ya kuweka mapingamizi, kila kitu kilikuwa kinaonekana kwa uwazi japokuwa watu wengi wanazungumza wakiegemea upande mmoja