Kwako kipimo cha mke bora ni kipi?

Gily

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
1,090
2,000
mlikutana wapi na x wako?
mahusiano yenu yalianzaje?
kipi kizuri unakikumbuka kutoka kwake?
naomba majibu plz Mr Gily

Sent using Jamii Forums mobile app
Nilikutana na ex nikiwa chuo mwaka wa kwanza, siku ya kwanza kumuona nilitamani sana kuzungumza nae. Mie usione navyojieleza hapa ukazani ni mashuuri kwenye kutongoza hapana, nilikuwa zege kweli kweli. Mbali na hivyo mie sio mtu wa kuhangaika na wanawake. Basi nikajisogeza akiwa na rafiki yake, ila nilikuja jua hawakuwa friends nao wamekutana tu, basi wakati tunapiga story hizi na zile yule rafiki akawa amenichangamkia sana. Yeye alikuwa form six na pale mwenge alikuwa amekuja tution kusoma, basi tuakajikuta na story za hapa na pale na ushahuri mwingi tu. Kilichonipa sifa ni kuwa form six nilipiga PCB so akawa anavutiwa sana na jinsi nilivyosoma hivyo na yeye alikuwa anasoma PCB, na alishangazwa kwa nini chuo nimekimbilia biashara, Bachelor degree in Accountancy

Niliomba number zake, na nikawa namtumia message, kila message ikiingia iliyotoka kwake basi moyo wangu ulikuwa unadunda, kwa shauku ya kutaka tu kujua anachkisema ni kitu gani. Mungu ni wa ajabu sana, kumbe wakati mimi nimemzimia kumbe na yeye alikuwa kama kanipenda vile. Tukajikuta tumekuwa kwa mahusiano. Mahusiano yanapokuwa machanga unakuwa na hamu sana ya kutaka kujua cha ziada kutoka kwa mwenzako na yalivutia sana, ilibidi arudi shule. Basi akawa anarudi likizo na mapenzi yanakuwa matamu zaidi, shule nilikuwa napigiwa simu na number za walimu anadanganya anampigia mama yake, nilikuwa najisikia ananipenda sana sana sana na likizo nilikuwa natamani sana kuwa nae, na nilifurahi sana.

Nakumbuka yeye ndiye mtu wa kwanza kabisa kuninunulia keki kwa birthday yangu. Hakuna ambaye alishawahi kuninunulia kabla ya wengine wote na ilikuwa ni faraja sana. Baba yake Muislam mama yake Mkristo, nakumbuka sana alivyokuwa ananipigia simu usiku tu saa kumi mfano, na kunambia tusali, sala nishaisahau ila ilikuwa napenda sana kwa kuwa yeye si Mkristu. Ile sala ya ya kulala ya kikatoliki dah siamini nimeisahau. Nitakwambia imenitoka tu coz umeniuliza ghafla
Nachokumbuka pia ni kuwa alinipa usichana wake, ila mapenzi yalikuwa kama movie kipindi kile, baada ya miaka miwili alibadilika sana

Nimekosa hata mood ya kuandika kwa kusahau ile sala
 

google helper

JF-Expert Member
Jun 11, 2013
8,131
2,000
Hahaha kwa sababu nimependa sana au? To love is not a crime, if someone leaves me for loving them definitely shame on them. .

Ina maana google helper wewe hujawahi kupenda????? Ila ulichosema ni sahihi hutakiwi kumpenda mtu ambaye hakupendi. Hawezi na haiwezi tokea mtu akaamka asubuhi akakutamkia hakupendi, lazima kutakuwa na jambo tu, unless hakukupenda toka mwanzo. .
Mkuu neno langu la busara ni kwamba ishi nao kwa akili pia. Usije lia huku jamvini boss

Sent using Jamii Forums mobile app
 

dottoz

JF-Expert Member
Jan 29, 2012
1,520
2,000
Mwanaume kukonda kukonda na mwanamke kunenepa wakiwa katika ndoa je shida ipo kwa nani????
Na kuna usemi mmoja unasema kuwa ,ukiona mwanamke ananenepa akiwa kwenye ndoa na mwanaume wake kukonda jua kuna shida kwa mwanamke,je wewe unachukuliaje hilo?
Gily,
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom