Kwako kaka Mpina

IsayaMwita

JF-Expert Member
Mar 9, 2008
1,127
140
Mheshimiwa mbunge Mpina, ile budget uliyoipinga magamba wenzako wameipitisha, je unawaambia nini watanzania? utaendelea kuwa mchumia tumbo ili maisha ya wanao yasonge? je ni uwamuzi gani utauchukua kwa sasa mami? wamekupuuza, wamekudharau....,wanajua hauna pa kwenda, watanzania wanasubiri kauli yako....TAFAKARI
 
Mpina hakuna kitu, hayawezi maamuzi magumu kama ya lyatonga mrema! Mchumia tumbo tu huyo! Kwa nini anakimbia kura ya maamuzi?
 
mimi naona naa kupinga kwake hiyo bajeti ameonesha dhamira ya dhati ya kuwatetea wananchi wake hata akitoa kauli kama bajeti imepita haita saidia lolote
 
Mnafiki aki zeeka anabadalika kuwa mchawi leo tumeyaona wenyewe jinsi nchi hii wachawi walivyo wengi. Ccm wote ni wanga waTz angalieni sana sasa wamebakiza kutula nyama tu.
 
Nashangaa sana wabongo tunapowakejeli wabunge wanaotetea maslahi ya taifa kisa tumeweka uchama mbele. Akili itakapotukaa vizuri itakuwa too late!
 
Wakuu Mpina hana lolote huyo, mchumia tumbo tu huyo. Tungemsifu kama angebaki MJENGONI na kusema HAPANA! Tena kwa sauti kubwa. Yaani kwa kitendo hiki kajidhalilisha mwenyewe mbele ya Umma. Jimboni tunamsubiri tuje tumhoji kulikoni. Ila kwa vile asilimia kubwa ya wapiga kura jimboni kwake ni bongo lala watamwona shujaa kwa jinsi alivyojitutumua! Chezea kitu ingine siyo posho bwana, watu huwa wanalia ati! Kumbuka yaliyomkuta KAFULIA! Eti mpaka anaitisha na waandishi wa habari kumbe ovyooooo!!
 
Kati ya wabunge wote wa ccm ktk awamu hii,mpina amewazidi wote kwani ameonesha uzalendo kwa wapiga kura wake
 
Mheshimiwa mbunge Mpina, ile budget uliyoipinga magamba wenzako wameipitisha, je unawaambia nini watanzania? utaendelea kuwa mchumia tumbo ili maisha ya wanao yasonge? je ni uwamuzi gani utauchukua kwa sasa mami? wamekupuuza, wamekudharau....,wanajua hauna pa kwenda, watanzania wanasubiri kauli yako....TAFAKARI

Ilikuwa siasa tu. Mpina hana tatizo na serikali yake. Anaipenda ccm
 
Hebu hawa wabunge wetu ni kwa nini hawajiamini? ni kwa nini wanatuhadahaa! hebu kwele Mpina alikuwa na sababu ya kukimbia? kweli tutafika? siamini, Mpina sasa tukueleweje ndg yetu? kweli ndani ya CCM Hakuna mzima... nilidhani Mpina amekula unga wa rutuba... kutishiwa tu.... uharo huo....
 
Mpina na Bulaya wote hawana msimamo! bulaya alichimba mkwara lakini alipoitwa ndiyooooooooooooooo! Mpina aliweka bayana atapinga hata ijapobidi kufukuzwa ccm ulipotimia wakati wa kupinga kakimbia! ******! kama huna guts kwa nn usiwe unakaa kimya kama magamba wenzio??
 
Hawa wabunge wanajua kuwa wanazidanganya nafsi zao na siyo watanzania, kweli wanatufake sisi...., mpina ajitafakari... aone kama kuna sababu ya kuendelea kuwa mbunge... hata zile bilion 500 hazijaingizwa..
 
Mnafiki aki zeeka anabadalika kuwa mchawi leo tumeyaona wenyewe jinsi nchi hii wachawi walivyo wengi. Ccm wote ni wanga waTz angalieni sana sasa wamebakiza kutula nyama tu.

Ukiona kundi kubwa la watu kila kitu ambacho wanakipanga wanakubaliana basi ujue wengi wao hawafikiri
 
Hebu hawa wabunge wetu ni kwa nini hawajiamini? ni kwa nini wanatuhadahaa! hebu kwele Mpina alikuwa na sababu ya kukimbia? kweli tutafika? siamini, Mpina sasa tukueleweje ndg yetu? kweli ndani ya CCM Hakuna mzima... nilidhani Mpina amekula unga wa rutuba... kutishiwa tu.... uharo huo....

Siasa ni usanii, zamani definition ya siasa ilikuwa ni uongo ulikomaa sijui siku hizi ni nini, hapo nadhani serikali ilinusa dalili ya baadhi ya wabunge kupinga budget ikabidi ilete utaratibu wa kupiga kura kwa face to face hali serikali ikijua kuwa watz wengi including wabunge hawajiamini. Hapo ingekuwa kura ya sauti ya ndio au kikaratasi ungeona hata baadhi ya CCM wangekuwepo
 
Nadhani ifike mahali kura zipigwe kwa siri, kwa sasa CCM Wanachofanya ni kiini macho
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom