Kwa yeyote mwenye shida ya sheria za kazi

Ukiwa na tuhuma fulani kazini, na ukasimamishwa kazi kupisha uchunguzi, je uchunguzi huo unachukua mda gani kisheria? Na je mda huo ukipata bila tume ya uchunguzi kufanya chochote wala kutoa maamuzi yoyote nini kifanyike au sheria inasemaje kuhusu hilo?
Kisheria pale unapopewa barua ya kusimamishwa kazi inapaswa iandikwe na muda ambao unasimamishwa kazi of which it has to be reasonable kwa hiyo reasonable time itategemea na tuhuma yenyewe pamoja na muda wa uchunguzi kwa vigezo hivyo ndipo hesabu ya reasonable time hupatikana. Na iwapo muda ukipita unaweza kuwaandikia barua waajiri wako kujua hadhi ya ajira yako japo.
 
Shukrani mkuu
 
Nisaidie hili , Mtumishi mmoja wa idara ya Elimu , "alitoroka" kituo cha Kazi kwa kupata barua FEKI ya Uhamisho toka Kituo /Shule mmoja mjini Mwanza na kwenda Kufundisha Shule fulani moani Morogoro , Ulipokuja uhakiki wa watumishi ilibidi arudi Mwanza ambako alipewa charge sheet na TSD kwa kuwa amesimamisha na atapokea Nusu Mshahara , akapewa siku14 kuwa amejitetea kwa nini asifukuzwe kazi ,
Likajazuka la uhakiki wa watumishi , akapelekwa TAKUKURU ambako aliamriwa kurejesha pesa alizopokea akiwa nje ya kituo chake cha Kazi ambako anahesabiwa "MTORO" , akiwa anafanya hivyo , ile nusu Mshahara pamoja na Account yake ya Bank ZIKAFUNGWA hivyo pesa ya nusu mshahara ikio bank Marejesho ya pesa alizotakiwa kurejesha alisha maliza kurejesha Mpaka leo hajapata majibu ya TSD na Pia mkurugenzi wa Mji haja mpatia barua kutamka kuwa amefukuzwa kazi hivyo yupo ana "hang" bila kujua hatima yake , akienda kwa HR aanambiwa hilo ni agizo toka ngazi za juu
IPI FATE YA MWALIMU HUYU KIUTUMISHI
Asante
Walimu na nyie mnatia aibu!.

We umepewa barua feki ya uhamisho na ukaenda. Mwanza to Moro umbali wa kilomita 960. (Ni safari ya kuanzia saa 12 asbihi hadi saa 3 usiku kwa usimamizi wa sasa) swali;-

1. Je ulikuwa ni uhamisho wa malipo ama bila malipo??

2. Kama ni wa malipo (ni lazm uwe wa malipo coz yy ndo alipewa barua kuwa amehamishwa na mwajiri wke) je kwa nini asingeenda kwa mwajiri wke kudai/kufuatilia malipo yake yahakikiwe kabla hajaenda si hapo ndo mwajiri angeshangaa na kumuuliza kwan umehamishwa, then angegundua kuwa ni FAKE????

3. Mtumishi wa umma akihamishwa (tena mkoa had mkoa) taarifa hutolewa kwa mwajiri mpya (kituo kipya cha kazi) je alikuta kumbukumbu zake huko moro???

WALIMU..!!!!WALIMU....!!!mmhh....Aah...maana kuna mwingine huku nae kaenda BAYPORT kuulizia mashart ya mkopo kumbe kasainishwa form za mkopo bila hiari yake/bila kujua! Na cha ajabu kila mwezi anaona salary slip amekatwa marejesho ya mkopo hadi anakuja kwangu tyr ameshakatwa miezi 35 kwa RATE ya >170,000/= kila mwezi.

Nilishindwa hata kutumia LITIGATIONS badala yake nikakomaa na ADR.
 
Wakuu msaada wenu,
Mtumishi wa serikali akiacha kazi kwa hiari yake huku anadaiwa mkopo benki itakuwaje?
 
Wakuu msaada wenu,
Mtumishi wa serikali akiacha kazi kwa hiari yake huku anadaiwa mkopo benki itakuwaje?
Kisheria yajue haya

1. Kuna liability (kuwajibika)
2. Na Security (amana/dhamana)

So ukikopa pesa lets say 1,000/= kwa kujinadi kuwa wewe unamiliki mti wa maembe dodo na ukasema kwamb endapo utashindwa kulipa mkopo huo basi mkopeshaji achuke mti huo (wa maembe dodo) kurudisha hela yake, basi;-

Kisheria hapo ni kwamba 1,000 ni LIABILITY yko (i.e You are liable to repay it whatsover)
Mti wa mwembe hapo ni Security tu ya hyo 1,000.

Then, LIABILITY & SECURITY are independent from each other in relation to the process of repay. Iwapo SECURITY itatoka (....is destructed) LIABILITY itabaki palepale i.e YOU ARE LIABLE TO REPAY....

Kuisha kwa SECURITY adhari zake ni kwamba INAMPUNGUZIA UWEZEKANO MKOPESHAJI KULIPWA PESA YAKE.....ila haimwondolei mkopaji kulipa pesa anayodaiwa!.

Kwa kesi yko.
Kama mwajiri aliingia km mdhamini (GUARANTOR) basi atawajibika kulipa mkopo huo bank then yy atadili na aliyekuwa mfanyakazi wake (hata kwa kumshitaki mahakamani) ili awe refunded pesa yake aliyolipia mkopo maana mnufaika wa mkopo ni yy ex-employee. (Ref. Kifungu cha 92 cha sheria ya mikataba sura Na. 345 toleo la mwaka 2002)
 
Naombeni msaada wa kisheria mimi ni mtumishi nilienda kukopa pesa kwenye taasisi moja ya kifedha hizi ndogondogo ambazo wanakupa pesa alafu unawaachia kadi yako ya benki na tulijaza mkataba na kutia saini. Ila nimeshindwa kulipa deni lao kwa wakati ivyo wamenitishia kunishitaki sasa je nifanyaje na je ninaweza kufungwa?
 
Kuna mwenyewe swali juu ya maswala ya kazi
chumvichumvi heshima kwakwo,
Ninahitaji kufahamu boss anakupa mkataba usign kuwa anakulipa elfu anakuambia sign usijari lAkin mwisho wa mwez mshahara anakulipa elfu 3.je hapa mimi kama mfanyakazi nilishasign lakini pengine mbele nitafukuzwa Kazi nifanyanye napofukuzwa Kazi ili bos anilipe 3 yangu baada ya ile elfu iliyomo kwenye mkataba
 
Naombeni msaada wa kisheria mimi ni mtumishi nilienda kukopa pesa kwenye taasisi moja ya kifedha hizi ndogondogo ambazo wanakupa pesa alafu unawaachia kadi yako ya benki na tulijaza mkataba na kutia saini. Ila nimeshindwa kulipa deni lao kwa wakati ivyo wamenitishia kunishitaki sasa je nifanyaje na je ninaweza kufungwa?
Sio kufungwa tu, utafungwa endapo hautakuwa na uwezo wa kulipa hilo deni, lakini kama mlisaini na mkataba wa kimaandishi basi utalazimika kisheria kulipa hilo den, kwa sababu utakuwa unabanwa na mkataba mliosainiana, hapo huwezi kukwepa hilo deni cha msingi kama watakupeleka mahakamani uiombe mahakama mkamalizane nyumban basi
 
Ninahitaji kufahamu boss anakupa mkataba usign kuwa anakulipa elfu anakuambia sign usijari lAkin mwisho wa mwez mshahara anakulipa elfu 3.je hapa mimi kama mfanyakazi nilishasign lakini pengine mbele nitafukuzwa Kazi nifanyanye napofukuzwa Kazi ili bos anilipe 3 yangu baada ya ile elfu iliyomo kwenye mkataba
Kama mlichosainiana kwenye mkataba ni tofauti na unachopewa, basi cha kwanza kabla haujafuata hatua ya kisheria mwandikie barua ya kumwomba atekeleze kutoka na mkataba na umpe siku 5 ndan ya kaz awe ameshakujibu. Siku 5 zikipita andika barua ya pili ukimwambia kwamba rejea barua yangu ya tareh fulani yenye kichwa cha habari fulani, nakumbushia juu ya utekelezaji mpe limitation time. Asipokujibu sasa ruksa kwenda mahakamani ukiwa na ushahidi wa barua
 
Mkuu nashukuru kwa majibu mazuri. Tatizo muda huu haupo tena maana kuna mfuko flani wa jamii hutoa huduma za bure za matibabu kwa wanachama wake.wanakupa form upeleke kwa muajiri wako kuna mahali anatakiwa ajaze Mara tatu za mwisho yeye kukuingizia michango.nikampa form akanizungusha zungusha kwa kuwa tangia mwaka ulopita hajaingiza mchango.nimemsitiza sana zikawa ni kalenda.

Juma lilopita arinirudisha nyumbani,jumamosi akatuma meseji niende jana nikamuone kufika akanipa barua ya kuhudhuria kesho kikao cha nidhamu. Makosa ni kutofuata ratiba za kazi na n.k.nafahamu kwa kuwa unajua mimi najifahamu unataka kuniondoa. Sikatai kuondoka je ntapataje kifuta jasho?
 
Back
Top Bottom