chumvichumvi
JF-Expert Member
- May 6, 2010
- 1,207
- 309
Wanajamvini wenzangu kwa yeyote. Mwenye shida na masuala ya sheria za kazi awe huru kuniuliza.
Karibuni!
Karibuni!
Zinazokuwa coverede na Employment and Labour Relation ActFafanua mkuu sheria za kazi zipi?
Kuna suala la taarifa hapo kwenye sheria mama ya ajira taarifa(notice) ni mwezi mmoja kwa anaepokea malipo ya mwezi ambao ni wengi ila bado sheria imeruhusu makubaliano juu ya taarifa kati ya muajiri na muajiriwa kwaiyo ni vyema ukato taarifa kabla kutokana na makubaliano yenuNikitaka kuacha kazi na nikasubiri mkataba uishe kwanza ndio nikamtaarifu mwajiri wangu kutakuwa na tatizo? Eleza
Ni sehemu ya mkatabaAppointment letter ni mkataba?
Pasipo kujua makubaliano ya ukopaji na ulipaji ulivyo. Kwa kawaida Taasisi iliyomkopesha inabidi iwasiliane na mdamini kampuni pamoja na mdaiwa waweze kumlipa mdai kwa mfumo huu wa mdaiwa wa kwanza na wapiliHebu tupe ufafanuzi ,kuna jamaa yangu amaesitishiwa ajira na kampuni moja hapa dar na hiyo kampuni ilimdhamini jamaa kukopa fedha kwenye taasisi moja ya mkopo, swali langu hivi hapo taasisi inayomdai jamaa fedha na jamaa hajapata ajira mpaka sasa,je kisheria imekaaje hiyo?
Anatakiwa kulipa aliyemdhamini akope au taasisi isubiri mpaka jamaa atakapo pata ajira mbadala?
Ukiangalia mabadiliko ya sheria ya hivi Karibuni kwenye ma swala yote ya Employment standards ELRA inakuwa na nguvu juu ya sheria zingine zote za kaziHebu nisaidie huu utofauti wa likizo za ugonjwa: mbona uko tofauti kati ya ELRA, 2014 na ile Public Service Act, 2002 sasa hapo mwajiri atekeleze ipi!
Inatakiwa iombwe ndani ya siku 7 toka mama amejifungua (mke halali) ni siku 3 yenye malipo mtoto akizaliwa salama na ni siku 4 zenye malipo iwapo mtoto atafariki na kadhalika hii ni kwa watumishi woteIle kitu inaitwa Paternity mfanyakazi anatakiwa apewe siku ngapi? Je kuna malipo atapewa? Fafanua kwa watumishi wa umma na binafsi pia je utaratibu ukoje?
Make kwetu unapewa mshahara wa mwexi unaokwenda likizo tu na ukirudi unaanza kuwa omba omba hadi mwezi uishe; hiyo ni moja pili ni kwa unalazimwisho kwenda likizo na hicho kidogo huwepa wanapojisikia ikibidi ukirudi likizo ndio hupewa!OK! Kiutaratibu unapoenda likizo sector binafsi sheria inasemaje?
Tafadhali fafanua swali ili niweze kukujibu ki ufasaha sababu kisheria swala la likizo ni pana sana na inatambua likizo tofauti tofautiOK! Kiutaratibu unapoenda likizo sector binafsi sheria inasemaje?
Likizo ya mwezi ki utaratibu unapaswa kupewa hiyo pesa ya likizo ila sheria haijakataza kuwepo kwa makubaliano ya jinsi ya pesa ya likizo kulipwa waajiri wengi huwa wanatoa nusu ya pesa ya likizo wakati wa kwenda na nusu ukirudi unapewa kama kuanzia nayo maisha baada ya likizo..... kuhusu swala la kulazimishwa sheria imepinga vikali na ili kuepuka ilo mwajiri anapaswa kuwa na orodha yenye mpangilio wa likizo ya mwaka mzima(leave roaster)Make kwetu unapewa mshahara wa mwexi unaokwenda likizo tu na ukirudi unaanza kuwa omba omba hadi mwexi uishe; hiyo ni moja pili ni kwa unalazimwisho kwenda likizo na hicho kidogo huwepa wanapojisikia ikibd ukirudi likizo ndio hupewa!