Kwa yanayoendelea hivi sasa Nchini, sheria ibadilishwe ili watanzania tumiliki silaha kirahisi.

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,288
15,238
Sina sababu ya kuanza kueleza yanayotokea huko Kibiti na maeneo mengine ya karibu.

Hivi sasa hapa nchini kuna ugumu wa kumiliki silaha, yaani nazungumzia mlolongo wa mambo ya kufuatilia ili tu uweze kumilikishwa silaha ki rahisi.

Ukizingatia sisi wakazi wa maeneo ya Kibiti huku jinsi kulivyo, bila shaka tunaona tija kwa sserikali yetu bsikivu, tena pendwa, tena ya "wanyonge" iweze kuhakikisha badiliko la dharura la kisheria ambalo litaondoa masuala ya milolongo mingi ya kufuatilia pale mtu ahitajipo silaha ya kujilinda.

silaha ni haki muhimu ya binadamu, kila binadamu anatakiwa amiliki silaha ili aweze kujilinda katika Dunia yenye watu walio kengeuka.

Ehh Serikali, hebu sikia kilio hiki cha wakazi wako wa Kibiti na maeneo ya karibu.

Cc. @Magufuli @KamandaSirro & co.
 
Silaha siyo watanzania tuenzi amani
Embu nifafanulie amani kwa mtu aliyefuatwa nyumbani kwake, kisha kuwasikia hao baradhuli wakija na kuvunja mlango wake naye kujisunda uvunguni mwa kitanda chake.
Mke akaanza kuhojiwa kuwa tuoneshe huyu mbwa alikojificha.
Mwanamke kaanza kujiumauma na majamaa kuanza kusachi nyumba nzima. Baada ya kugundua kuwa yu mvunguni mwa kitanda chake, wakammiminia shaba za kutosha na huo ukawa ndiyo mwisho wa maisha yake.
Hayo maelezo nimekupa ili uelewe mantiki ya mtoa mada.
Amani ni wimbo usio mashiko sehemu isiyo na amani.
Na huyo muhanga angekuwa na silaha yake binafsi ya kujilinda, hata angelipata umauti kwa kuwa ni jambo lidilozuiliwa likifika, lakini angelikufa akijitathimini aina ya uzembe uliomfikisha kuzimu mapema ghafla, pia angeridhika na kifo chake.
Lakini aina ya kifo alichokipata cha bila kujihami na kuwaacha wauwaji kujichagulia ebeo la kupiga, hakika mabadiliko ya kuondoa ukiritimba wa umiliki wa silaha nchini Tz unahitajika haraka.
 
Mtoa mada, unafikiri raia wa huko kibiti kumiliki Bastola ndio kutapunguza hayo mauaji yanayoshamiri??
 
Solution ni kutatua kibiti,..kuhararisha silaha ni kuchochea mauaji yaendelee,..think twice
 
Back
Top Bottom