Kwa wenzangu wote, siku yetu hii

Kwa wenzangu wote, siku yetu hii

Nilikua na kula na mkono wa kushoto utotoni niliambulia ukatili wa kutosha kutoka kwenye familia hadi nikanyooka mpaka leo hii nikipata tatizo mkono wakulia hua nakula kwa shida sana mkono wa kushoto
All in all watu wanaamini tunaakili sana napenda nithibitishie kwa mimi binafsi yangu sina akili kabisa na sijawahi kua nazo
But trust me normal is boring hakuna kitu kizuri kama kua tofauti na majority , happy leftists day [emoji23] kama ni kweli hii siku ipo
Kipindi napata ufahamu utotoni, sikuwahi kuwaza kuwa huu mkono nnaotumia unatatizo (kumbe wazazi walipambana mapema lkn ilishindikana) mpaka hiyo siku nikiwa kama darasa la tano hivi bro alikua na desturi ya kurudi usiku na vitumbua vitamu toka uswazi huko kwenye zile biznes za usiku, siku hiyo alirudi mapema nikamganda kwamba twende wote kwenye vitumbua kweli mida ya saa moja jioni akanibeba kwenye baiskeli ya Phonex mapaka kwenye vitumbua, wamama wamejipanga wengi kaenda kwa mama muuza kampa pesa mm nikachukua spoku haraka kwa kono langu la kushoto nikaenda kwenye sanduku la mbao lina kioo mbele nakuanza kuchukua vitumbua vya idadi ya pesa, asee yule mama alibadilika ghafla akasema "ndio umetumwa uje kuharibu biashara yangu mshenzi we mtoto subiri nikufundishe" anaongea hayo huku ananyanyuka kaacha kuchoma vitumbua ananifuta kwa kasi naamini alikua anakuja kunipiga ndio bro kuingilia kati na kuninyang'anya ilespoku wakawashiana moto (bro akinitetea nakuambia yule mama aache imani za kishirikina) binfsi nilibaki kwenye sito fahamu, yule mama akatufukuza na kurudisha ile hela yetu, tukahamia kwa jirani na kuchukua mzigo lkn bro ndio alichagua, si njiani wala home hatukuzungumza kilichotokea binafsi ilinifanya nitafakari mno na kujua tatizo ilikua nini, baada ya hapo nimeshuhudia mengi mno, mazuri na yaabu kuhusiana na huu mkono lkn mpaka sasa si mkono wala mguu natumia shoto.

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Kono la baraka hili 😀😀
 
Kutumia mkono wa Kushoto ni Ulemavu kama ilivyo watu waliozaliwa na Ulemavu mwingine au kasoro za Uumbaji mfano wa makengeza, albinism nk.
Hao wanaojiita MASHOTO wanakasoro za Uumbaji kwenye mkao wa Ubongo kwenye Vichwa vyao. Nendeni Hospital kwa wataalam wawambie ukweli acheni kujisifia Ulemavu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom