Kwa wazazi: soma hapa tafadhali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wazazi: soma hapa tafadhali

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kapwani, Aug 10, 2011.

 1. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa waliotazama taarifa ya habari ya saa 2 usiku ITV waliona taarifa ya binti wa miaka kumi na tatu kujinyonga hadi kufa kwa kamba ya pasi. Ilikuwa ni habari ya kusikitisha sana sana hasa kwa sie wenye watoto/ambao tunalea kwa sasa...mbali ya uchungu wa mwana lakini pia gharama kubwa tunazotumia kuwalisha, kuwavisha, kuwasomesha nk lakini zaidi ya yote future iliyokuwa mbele ya binti mdogo Mariam iliishia jana asubuhi alipoamua kuyakatisha maisha yake mwenyewe.

  Nikiwa bado katika mshtuko wa taarifa hii, mwandishi alijipenyeza kutaka kujua kisa cha jambo lile...majirani wengine walisema binti alionekana toka juzi hana raha, wengine walidai kulikuwa na hali ya kutoelewana na mzazi wake LAKINI MAMA YAKE ALIYEKUWA ANALIA KWA UCHUNGU ALISISITIZA KWAMBA HAJUI LOLOTE. Hili jibu la Mama mariam ndio sabau ya mie kuweka uzi huu hapa jamii forums.


  Ningependa kuwaasa wazazi wenzangu juu ya malezi ya watoto hasa watoto wetu wa utandawazi kujitahidi kuwa karibu na mabinti na vijana kwa karibu sana. Kuwa na tabia mzazi/rafiki at the sametime ili kuepusha sintofahamu kama hizi. Simaanishi kuwa msiba huu unasababishwa na distance kati ya mama na binti yake kwani siwajui wala sijapata taarifa zaidi ya ile ya ITV.

  Ila kwa majibu ya haraka haraka yaliyojitokeza pale na reflection yangu ya maisha ya sasa na watoto wetu ambao wako katika ulimwengu uliojaa mambo maovu, EXPOSED NA INFORMATION KILA KONA nina kila sababu ya kuwaasa wazazi wenzangu juu ya umuhimu huu.....UKARIBU NA WATOTO WETU/

  Nitaandika maana yangu kwa mfumo wa maswali 2;
  1) kwanini kuna umuhimu wa kuwa na rafiki na mtoto wako Ambao tulilelewa tukiwa watoto miaka ya 80 na 90 wengi wetu tunajua ukoloni wa wazazi wetu ulivyokuwa.

  Ilikuwa ngumu sana kushare na mama au baba yako mambo fulani fulani (uzazi) hasa ukizingatia kuwa culture yetu hairuhusu.....nakumbuka binafsi hata nilipofika hatua ya kuingia usichana  nilitamani mama asijue....hata leo hii naandika mada hii bado distance kubwa ipo kati ya ngu na mama yangu ( baba yangu alifariki), nikipata shida ni heri kumtafuta rafiki yangu kwa simu na kuomba ushauri juu ya mambo yangu lakini sio mzazi wangu.

  Kwa vyovyote mahusiano ya mtoto na mzazi yakijaa VITISHO, KUPEANA TAARIFA ZA UONGO, UBABE NA MIPAKA ISIYOYALAZIMA lazima utajikuta humfahamu mtoto wako, hujui anapita kwenye stress zipi, hujui ana mahitaji gani ya kiroho na kimwili.


  Ukaribu unasabisha kuzisoma hisia za mwanao kirahizi, kuweza kulinganisha mapito anayopitia sambamba na umri wake na peer pressure inayomzunguka.....ukiwa mkweli na muwazi kwa mtoto toka yupo mdogo ATAKUAMINI, ATAJUA MAMA AU BABA ANA SULUHISHO LA MAMBO YANGU....atategemea peers kwa kiasi fulani na sio 100%.

  WAZAZI WENZANGU TUSOME ALAMA ZA NYAKATI...TUWAJENGEE WATOTO WETU CONFIDENSI, WASITUOGOPE SANA, WAWE HURU KUJIELEZA, MZAZI UWE MKWELI AKIKUULIZA ISHU FULANI hata kama ngumu kimila haizungumziki.

  KWANI UKIMDANGANYA ATAHAMISHA IMANI YAKE KWA MARAFIKI ZAKE AMBAO WATAMWAMBIA KWELI KWA MFANO 'MTOTO HANUNULIWI HOSPITALINI ILA ANAZALIWA wakati wewe ulimpa desa refu la uongo. Akikusoma katika taarifa nne tano za uongo hata kuamini tena.

  HII INAMAANISHA KUMPA MTOTO MAJIBU YA UKWELI KULINGANA HA UMRI WAKE NA SIO MAJIBU YA UONGO. HII INAWEZEKANA NITAFAFANUA NEXT TIME.

  ANGALIZO:

  Hii haimaanishi kuwadekeza na kuwaendeka kwa kila kitu hapana......UKARIBU, IMANI YA MTOTO WAKO KWAKO NA CONFIDENSI UTAKAYOMJENGEA INAWEZEKAMA PASIPO KUDEKEZANA
  . NAKIRI HII SIO NJIA PEKEEE YA KUMALIZA ATHARI ZA MATUKIO MABAYA KWA WATOTO HASA KIPINDI CHA EARLY ADOLESENSI ( AGE between 10-13) NA ADOLESENSI YA BAADAE (14 and above) ILA KWA MTAZAMO WANGU HUENDA IKAPUNGUZA MATUKIO HAYA KWA KIASI FULANI IKICHANGIWA NA JITIHADA NYINGINE.

  INAWEZEKA MZAZI TIMIZA WAJIBU WAKO MTOTO ASIPOKUELEWA AKAPINDA HYO ITAKUWA JUU YAKE LAKINI WEWE ULI PLAY VEMA YOUR PATI

  Swali la 2 ni: How to balance! kuwa mzazi/rafiki/mshauri kwa watoto wetu? hii siku nyingine wapendwa.
  Nakubali kukosolewa ili nijifunze zaidi
  Mix with yours
   
 2. I

  Igangilonga Senior Member

  #2
  Aug 10, 2011
  Joined: Mar 11, 2006
  Messages: 121
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kapwani nakukubali kwa maelezo yako mazuri na ushauri mzuri. Mimi ni mzazi na huwa najitahidi kuwa karibu na wanangu, nitaendelea kuboresha zaidi na zaidi urafiki na ukaribu kwa wanangu. Hujatuambia imetokea wapi hiyo ya mtoto kujinyonga?

  Halafu nikuulize swali la kizushi, wewe ni mwandshi by profession? Maana umeandika vizuri mno na imeeleweka.... all da best
   
 3. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii imetokea jana dar es salaam maeneo ya mwananyamala...

  mie sio mwandishi kaka yangu ni mtafiti ( Human geographer). nikiwa mtoto nilipenda sana kuwa mwandishi lakini nikaishia kusoma sociology na human geography

  mix with yours
   
 4. M

  Majala Kimolo JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 344
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Inasikitisha, na jana Naibu katibu mkuu wa UN Dr Asha Rose Migiro alizindua taarifa ya survey ya ukatili kwa watoto. Kwa kweli tunahitaji kujipanga, mazoea yetu yanhaitaji kudhibitiwa. Hebu angalia maeneo waliyofanyia uchunguzi
  awali, Unyanyasaji kijinsia, udhalilishaji na ubakaji, Pili, lugha ya manyanyaso, matusi na kashfa na tatu vipigo kwa watoto.
  Hebu tufikiri ni lipi hatujalifanya aidha kwa hasira au bila kukusudia?
  Wanangu najipanga kurudisha heshima yenu, maana hata kindumbwendumbwe hakifai kwa watoto vikojozi wapelekwe hospitali, na haya magazeti ya udaku watafakari wanachoandika

  shime tutafute report hii tuisome, au wasiliana na Wizara ya maendleo ya Jamii Jinsia na Watoto au UNICEF Tanzania waliofadhili
   
 5. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Thanks for sharing, ni vema kujibidisha katika masuala ya watoto wetu .....leiziafeaness haifai. Kama ulivyosema kindumbwendumbwe kinajenga picha mbaya sana kwa mtoto....unamuaibisha hadharani hii inaleta self esteem kuwa low, confidensi inadondoka akiwa na watoto wenzie nk
  By the way baadhi ya sababu zinazoweza kuchangia mtoto kujikojolea usiku ni bulingi/ kuonewa .....imagine anaonewa na marafki zake, mzazi hujui nawe bila kuelewa una muadhibu kwa kindumbwendumbwe....inaumiza sana lol

  mix with yours
   
 6. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #6
  Aug 10, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Kusema ukweli ile habari ilinivunja moyo halafu binti mwenyewe alivyokuwa anafanana na mamake!! Mh hata sijui tufanyeje hapo usikute alionywa kidogo tu akaona anaonewa. Nadhani kwa staili hii itabidi tuwe tunawaonya watoto wetu kwa kuwalia timing kama tunavyofanyaga kwa spouses wetu!! unasubiria kwenye good mood ndo unaanza lakini mwanangu, siku ile kusema ukweli sikufurahia...........
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Aug 10, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Ni vizuri kumsoma mwanao na kujua jinsi ya kukabiliana na hisia zake.
   
 8. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Asante sana Kapwani kwa mada yako.
  Mara nyingi mtu anapozungumza dhana ya "kwenda na wakati", wahafidhina wanakuja na kejeli eti ni "kufuata uzungu". Walichokuwa hawaelewi au pengine wanaelewa lakini hawazingatii, ni kuwa sasa dunia haina tena mipaka, hakuna uzunguni wala uswahilini. Kwani hata huko uzunguni, kuna wahafidhina pia, wana malezi yale yale ya kizamani ambapo "mzazi yuko juu, anajua kila kitu, ana suluhisho kwa kila tatizo, kauli yake ni sheria...na mtoto yuko chini, ni wa kusikiliza, wa kutii, haja komaa, wa kuogopa...". Hata huko kwa wazungu, bado kuna watoto wanaangukia kwenye madawa ya kulevya, wanapata ukimwi, wanakuwa na mkonomkono, wanapata mimba zisizotarajiwa, wanajinyonga kwa kamba za pasi, sababu kubwa ni uhafidhina katika malezi na wazazi kukosa wakati na watoto wao.


  Kwa aina hiyo hapo juu ya mahusiano kati ya wazazi na watoto, ndio maana watoto kwa kujua kuwa atakemewa, atatishwa, atapigwa, atanyimwa taarifa... hukimbilia kwa marafiki ambako atasikilizwa na kushauriwa. Tatizo ni ushauri gani atapewa. Kwa hivyo ninakubaliana kabisa na Kapwani kuwa wakati umefika wa kuondosha mipaka na pazia baina yetu na watoto wetu. Kimaumbile, mtoto mchanga anamwona mzazi wake kama kimbilio na kinga kwa usalama wake. Mtoto mchanga anapokuwa mbele ya mzazi wake hujiamini na kujisikia analindwa. Kwa nini baadaye watoto wetu wanapokuwa wakubwa wanpoteza imani hii? Pamoja na sababu nyingine, wazazi tunakuwa hatuko karibu na watoto wetu.

  Nikisema karibu sikusudii ukaribu wamasafa tu, bali, na zaidi, hata ukaribu wa mawazo. Ukaribu wa masafa mara nyengine hauepukiki. Fikiria baba na mama mnatoka asubuhi kuenda kazini. Watoto wanarudi shule kabla na wazazi wanaingia masaa kadhaa baadaye, pengine usiku. Si baba wala mama mwenye nafasi (dhamira) angalau ya kumwuliza mwanawe "leo imekuwaje?, amesoma nini?, amefikwa na nini?, ana tatizo gani? Ikiwa haiwezekani haya ndani ya siku za wiki, basi angalau mwishoni mwa wiki? Mara ngapi kwa wiki mnakuwa nyote mko pamoja nyumbani, mnaka meza moja? unachungulia kwenye madaftari yao kujua wamesoma nini? Hapa mtoto hafaidi tena ule ukaribu aliokuwanao alipokuwa mchanga.

  Kuwa wazazi na wakati huohuo kuwa marafiki kwa kwa watoto wetu inawezekana na wala haimaanishi kuwa mzazi utajivunjia heshima kwa mtoto wako. Kubwa ni kuhakikisha kuwa unamjenga mtoto wako kukuamini na kuwa wewe si tishio kwake, si chanzo cha karipio, si kisago, si kukosolewa, si kutokusikilizwa, si HAPANA isiyo sababu bali "HAPANA KWA SABABU HAPANA; NIMESHASEMA HAPANA". Tukiwa wazazi wa aina hii tunasababisha watoto wetu kutotuamini na kutojiamini wao wenyewe. Na ndio maana, wanakimbilia kwa marafiki.

  Pengine nyote, wewe mzazi na marafiki, mnaweza kuwa sahihi au la katika kumshauri, tafauti ni kuwa "mzazi hachaguliwi na rafiki huchaguliwa, katu mzazi hawezi kwa makusudi kumpotosha mtoto wake lakini rafiki mbaya anaweza". Cha kufanya ni kufungua mlango wa uwazi na ukweli kwa watoto wetu. Tuzungumze, tuwasilikilize, tujadiliane nao kwa uwazi na ukweli. Tutetee HAPANA zetu kwa kutoa sababu. Tusikilize NDIO zao kwa kuuliza sababu baadaye kuzijadili. Tuwafanye watoto wawe na uwezo wa kutafakari kwa uhuri kabisa katika matendo yao.

  Tujitahidi kuwalea na kuwafunza watoto wetu sisi wenyewe na wala sio kuwawacha wafunzwe na ulimwengu, wasije kuangukia katika lile kundi la "Asofunzwa na mamae/babae".
   
 9. Jomse

  Jomse JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli ni muhimu sana wazazi wa sasa kuwa karibu na watoto wetu kwani hatari ambazo zinawazunguka watoti wetu ni nyingi,hasa kwa wenye watoto wa kike hatari pale nyumbani ,hatari barabarani na hata huko shuleni.Ni muhimu kuwa karibu na watoto wetu ili waweze kutuuliza na sisi ndio tuwe watu wa kuwapa majibu ya maswali mengi waliyonayo kuliko wapate majibu hayo kutoka kwa watu wengine ambao wanaweza kumpotosha.
   
 10. A

  Aine JF-Expert Member

  #10
  Aug 10, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ahsante sana mpendwa kwa hilo, huu ni ukweli usipingika,mimi niliona taarifa hiyo ilisikitisha sana, ila kinachonishangaza sana ni kuona damu, hivi kweli mtu akijinyonga anatoka damu au kuna kitu kimejificha hapo!!!!!
   
 11. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #11
  Aug 10, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mhhhh,

  Wazazi kazi tunayo...Tena watoto wenyewe wamzungukwa na misitu ya habari...chafu na safi...Lazima tutaonja joto la jiwe!!
   
 12. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #12
  Aug 10, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nikimkuta mtu anataka kujinyonga namuengezea kamba ili ajinyonge haraka kwa sababu amechoka kuishi!
   
 13. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #13
  Aug 10, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  mie na mwanangu ana miaka saba kavulana kazuri naenda nako bar tunakula bia kinoma nimekafanya kanione rafiki sana kakipata glass moja ya bia kananieleza kila kitu bila kificho
   
 14. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #14
  Aug 10, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Mie niko karibu sanasana kwa kweli, kitu chochote lazima aniambie yaaani, na ninamweleza wazi mambo ya dunia yalivyo, tangu hivi na umri mdogo, kwa hiyo hata akikua nitaendelea hivihvi, sasa mie nina ndugu zangu ni wakali hatar, utakuta watoto wao wanakuwa karibu na mie na kunieleza mambo mengi kuliko hao wandugu, na mie natumia nafasi hiyohiyo kuwapa mafunzo ya dunia inavoenda na kuwa kama mwongozo bila kuwasemea au kuwakaripia

  Kwa huyo mtoto itakuwa tu mambo ya wanaume tu, mtoto akiingia uteenager usipokuwa na busara unaweza ua, sababu wanakuwa wanafikiri wanajua kuliko wewe, yaani wanaweza mwona mzazi kama mshamba fulani hv, inabidi uwe na zaidi ya busara kuweza kuwa handle hawa watoto
   
 15. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #15
  Aug 10, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kunakitu hapo sijakuelewa kama hayo ndio maadili mtoa maada alikuwa analenga ushauri wangu acha kwenda na mtoto miaka 7 bar unamfundisha vitu vya ajabu sana atakuja afanye vitu amabavyo hukutegemea
   
 16. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #16
  Aug 11, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Tuwaonyeshe upendo watoto wetu, hata wakiwa wamekosa, tuwakanye kwa mipaka, hasa wakifika umri wa kupevuka
   
 17. Domo Kaya

  Domo Kaya JF-Expert Member

  #17
  Aug 11, 2011
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mijitu mingine bwana kama punguwani vile, wenzio wanaongea vitu vya maana wewe unaleta kejeli..... unajua sio kila mada lazima uchangine kama huna soma uondoke ukachangine siasa sio kuandika pumba zako kwenye mada ya maana. "Nyambafu"
   
 18. A

  Aine JF-Expert Member

  #18
  Aug 11, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ebu tuambie hapo unamfundisha nini huyo mtoto wako unachoweza kujisifia?
   
 19. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #19
  Aug 11, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Asante sana Kapwani..
  Kwa hii Post yako nakumbuka machungu yaliyonipata nikiwa na umri mdogo sana13-15 lakini kwa sababu wazazi wetu enzi zile hawakutuweka karibu sana ..walijenga mazingira ya sisi kuwaogopa hata ukiwa na jambo kumuanza unaona issue sana unajihoji mara mia
  Sitasahau ...sitasahau
  Kabinti kangu sasa kanasoma baby class najitahidi kuwa karibu nae nimwelewe hatua kwa hatua katika ukuaji wake hata sasa akitoka shule ananipa vituko na viugomvi vyao vya kitoto nafarijika.Pale napoona kakosea namwambia tu hapa sio hivi mwanangu ...
  Nitajitahidi kuwa karibu nae siku zote za maisha yangu.

  Inasikitisha
   
 20. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #20
  Aug 11, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Naimani hauko serious na hili kama mzazi…
   
Loading...