Kwa watumiaji wa kinywaji cha Serengeti Lite

chimwanga

Member
Apr 15, 2020
8
1
Mimi ni mmoja wa watumiaji wa kinywaji hiki pendwa cha Serengeti Lite

Mwanzoni kilipoanza kusambazwa kwa watumiaji chupa zake zilikuwa na maandishi madogo kwenye chupa yanayooeleza tarehe ya kutengezwa na tarehe ya mwisho wa matumizi ya kinywaji hicho na zilikuwa na ladha nzuri sana.

Baadaye kidogo maandishi hayo kwenye chupa yakaonekana kuwa ni makubwa. Juzi kati maandishi hayo hayo yakawa yanaonekana kwenye karatasi iliyobandikwa (ile iliyoandikwa no sugar added) kwa chini.

Mie kama mteja naomba kuwauliza wazalishaji ikiwa line of production ni moja iweje kuwepo na tofauti hizo?

Pili chupa hizo za kinywaji zenye maandishi makubwa ya tarehe hizo, na zile zenye maandishi ya tarehe hizo kwenye karatasi hazina ladha nzuri na zina kaharufu flani ikilinganishwa na kinywaji kwenye zile chupa zenye viandishi vidogo kwenye chupa,ambazo kinwaji kina ladha nzuri.

Kinachoshangaza zaidi unapata aina zote hizo tatu katika baa moja na zipo ktk. crate moja.

Serengeti Breweries tujuzeni kunani hapo?
 
Ulipoanza kunywa uliona maandishi madogo kwa juu.

Ulipoanza kulewa ukaona maandishi yamekuwa makubwa.

Umezidi kulewa maandishi yakahamia chini ya chupa. UKIENDELEA KULEWA MAANDISHI YATAINGIA NDANI YA BEER KABISA.

Ila safari kubwa haina mpinzani bado. Siyo ndogo, KUBWA.
 
Back
Top Bottom