Ethical Ninja CEH
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 3,695
- 5,038
- Na alaaniwe amdharauye baba yake au mama yake. Na watu wote waseme, Na iwe.
- Na alaaniwe ampotezaye kipofu akakosa njia. Na watu wote waseme, Na iwe.
- Na alaaniwe apotoaye hukumu ya mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe. Na watu wote waseme, Na iwe.
- Na alaaniwe alalaye na mke wa baba yake, kwa kuwa amefunua mavazi ya babaye. Na watu wote waseme, Na iwe.
- Na alaaniwe alalaye na mnyama wa aina yo yote. Na watu wote waseme, Na iwe.
- Na alaaniwe alalaye na umbu lake, binti ya babaye, au binti ya mamaye. Na watu wote waseme, Na iwe.
- Na alaaniwe alalaye na mkwewe, mamaye mkewe. Na watu wote waseme, Na iwe.
- Na alaaniwe ampigaye mwenzake kwa siri. Na watu wote waseme Na iwe.
- Na alaaniwe atwaaye ujira wa kumwua asiye makosa. Na watu wote waseme, Na iwe.