Kwa wataalam wa sheria masaada unahitajika

Habari wadau, natumai mko vizuri....

Iko hivi, kuna mshkaji wangu mmoja hivi yeye yuko mwanza huko.

Juzi jumaatatu alitangaza kuuza simu yake kwenye mtandao flani wa hapa bongo.
Sasa anasema ni watu wengi waliipenda Ile simu Ila kikwazo ni kwamba walikuwa wakiuliza kama ana risiti ya simu pamoja na box lake na pia emai ya risiti ifanane na ya kwenye simu ndiyo watainunua bila shida lakini kwa bahati mbaya jamaa yangu risiti na box la simu alishavipoteza kitambo kidogo Ila simu alinunua kwenye Duka kubwa tu la muuzaji mkubwa Sana wa simu pale mwanza na siku ananunua tulikuwa nae Ila Mimi kwa sasa sipo mwanza.

Jamaa anasema akatokea dada mmoja akaonesha uhitaji Sana wa hiyo simu kwa bei waliyokubaliana ilikuwa ni simu Aina ya REDMI NOTE 10pro ambapo walikubaliana wakutane jana na huyo dada kwajili ya mauziano rasmi.

Jamaa anasema mida ya asubuhi wakawasiliana na yule dada ili waonane kumbe Yule dada baada ya kuusoma mchezo kuwa mwamba Hana risiti demu akawahi kituo cha polisi Pale mwanza na kuripoti kuwa Kaibiwa simu akaitaja Ile Ile ya mshkaji na mwizi wa hiyo simu yake aka mtaja mshkaji pia na mpaka rangi ya simu aliitaja ileile maana aliona picha za simu jamaa alizopost wakati ananainadi bidhaa yake.

Sasa kumbe wakati yule demu anaenda kuonana na jamaa kwajili ya makabishiano aliongozana na polisi kama wanne hivi wamevaa kiraia mshkaji akatiwa mikononi mwa polisi na kubebwa juu juu mbele za watu maana walikubaliana waonane barabarani kisha watulie sehemu demu aikague simu ili kama ataridhika nayo basi aichukue.

Mchizi anasema alisombwa juujuu hadi kituoni akituhumiwa kumwibia huyo dada hiyo simu na kama simu ni yake alinunua basi aoneshe risiti ya hiyo simu kama anayo na wakati huo jamaa anasema demu alikuja na karisiti
kake mchizi hajui demu amekatoa wapi hako karisiti na akawapa wale Askari kale karisiti.

Lakini cha ajabu mshkaji Kila akiomba risiti ya huyo demu aiangalie kama ni ya hiyo simu kweli polisi waligoma kumuonesha wakabaki wameishikilia wenyewe na kumwambia mchizi aende Duka aliponunua hiyo simu huwa wanabaki na kopi za risiti pindi unapoinunua ikiwa mpya na wanaandika kwenye kompyuta watampa ili aipeleke hapo central police waangalie emai za risiti na simu na pia wajue Nani tapeli Kati ya mchizi na huyo demu wa mjini

Na demu kakomaa kwamba simu ni yake na mchizi ndo aliyemwibia huku akaonesha yeye anarisiti yake ambako ni karisiti uchwara sasa na mchizi hajui huyo demu kachongesha wapi hako karisiti.

Sasa wadau kama kuna aliyewahi kukutana na kesi ya kubambikiwa na kutaka kutapeliwa namna hii je hili swala linasoviwa vipi!!?

Je mchizi akienda pale tuliponunua simu kweli atapewa hiyo kopi ya risiti yake ama hizo kopi zinakuwaga hazipo. Maana sasa mchizi anatuhumiwa kuiba simu yake mwenyewe kisa hana risiti.

Kisheria hii ikoje wadau. Na je ikibainika kwamba demu ni muhuni jamaa anaweza akamfungulia mashtaka huyo demu?

Mods tafadhali naomba mnirekebishie spelling za tittle hapo juu ni msaada na sio masaada kama nilivyoandika.

Ahsante.......
Mtafute wakili mpe laki moja akishinda kesi yule demu atalipa compensation na remidies zote
 
Hiyo simu niya wizi Mkuu!

Mwambie jamaa yako aseme ukweli, aidha alinunua simu ya iliyoibiwa, au yeye ndiye kaiba,
Yani nashindwa kusema kwamba jamaa kaiba sababu siku anaenda kuinunua nilikuwa nae Mimi mwenyewe na alikabidhiwa Kila kitu yaani full box kitu kiipyaaaa. Naona demu kapata upenyo baada ya kusoma komenti za watu wakiuliza risiti kama anayo ili wanunue na jamaa akakomenti kwamba risiti alipoteza sasa nahisi demu anataka kupitia humohumo na inaonekana ndo michezo yake.
 
Basi Sawa Mkuu.

Mpo pole Ila hongera Kwa kututahadharisha wengine
 
Sasa jomba sinaende hapo dukani ili ajue kama kuna copy ya risiti au la ndioo aanze machakato wa kupata mwanasheria au dolari za kutosha.
Asubuhi hii ndo kasema anaenda pale dukani hata Mimi nasubiri anipe feedback.
 
Hapo kuna njia nzuuli sana, aende kwa mkuu wa kituo aeleze shida yake , kisha aombe kitengo cha mtandao cha polic kuangalia ile cm toka ilenunuliwa ilitumia line ngapi? Hapo ndio utakuwa mwisho wa picha
 
Habari wadau, natumai mko vizuri....

Iko hivi, kuna mshkaji wangu mmoja hivi yeye yuko mwanza huko.

Juzi jumaatatu alitangaza kuuza simu yake kwenye mtandao flani wa hapa bongo.
Sasa anasema ni watu wengi waliipenda Ile simu Ila kikwazo ni kwamba walikuwa wakiuliza kama ana risiti ya simu pamoja na box lake na pia emai ya risiti ifanane na ya kwenye simu ndiyo watainunua bila shida lakini kwa bahati mbaya jamaa yangu risiti na box la simu alishavipoteza kitambo kidogo Ila simu alinunua kwenye Duka kubwa tu la muuzaji mkubwa Sana wa simu pale mwanza na siku ananunua tulikuwa nae Ila Mimi kwa sasa sipo mwanza.

Jamaa anasema akatokea dada mmoja akaonesha uhitaji Sana wa hiyo simu kwa bei waliyokubaliana ilikuwa ni simu Aina ya REDMI NOTE 10pro ambapo walikubaliana wakutane jana na huyo dada kwajili ya mauziano rasmi.

Jamaa anasema mida ya asubuhi wakawasiliana na yule dada ili waonane kumbe Yule dada baada ya kuusoma mchezo kuwa mwamba Hana risiti demu akawahi kituo cha polisi Pale mwanza na kuripoti kuwa Kaibiwa simu akaitaja Ile Ile ya mshkaji na mwizi wa hiyo simu yake aka mtaja mshkaji pia na mpaka rangi ya simu aliitaja ileile maana aliona picha za simu jamaa alizopost wakati ananainadi bidhaa yake.

Sasa kumbe wakati yule demu anaenda kuonana na jamaa kwajili ya makabishiano aliongozana na polisi kama wanne hivi wamevaa kiraia mshkaji akatiwa mikononi mwa polisi na kubebwa juu juu mbele za watu maana walikubaliana waonane barabarani kisha watulie sehemu demu aikague simu ili kama ataridhika nayo basi aichukue.

Mchizi anasema alisombwa juujuu hadi kituoni akituhumiwa kumwibia huyo dada hiyo simu na kama simu ni yake alinunua basi aoneshe risiti ya hiyo simu kama anayo na wakati huo jamaa anasema demu alikuja na karisiti
kake mchizi hajui demu amekatoa wapi hako karisiti na akawapa wale Askari kale karisiti.

Lakini cha ajabu mshkaji Kila akiomba risiti ya huyo demu aiangalie kama ni ya hiyo simu kweli polisi waligoma kumuonesha wakabaki wameishikilia wenyewe na kumwambia mchizi aende Duka aliponunua hiyo simu huwa wanabaki na kopi za risiti pindi unapoinunua ikiwa mpya na wanaandika kwenye kompyuta watampa ili aipeleke hapo central police waangalie emai za risiti na simu na pia wajue Nani tapeli Kati ya mchizi na huyo demu wa mjini

Na demu kakomaa kwamba simu ni yake na mchizi ndo aliyemwibia huku akaonesha yeye anarisiti yake ambako ni karisiti uchwara sasa na mchizi hajui huyo demu kachongesha wapi hako karisiti.

Sasa wadau kama kuna aliyewahi kukutana na kesi ya kubambikiwa na kutaka kutapeliwa namna hii je hili swala linasoviwa vipi!!?

Je mchizi akienda pale tuliponunua simu kweli atapewa hiyo kopi ya risiti yake ama hizo kopi zinakuwaga hazipo. Maana sasa mchizi anatuhumiwa kuiba simu yake mwenyewe kisa hana risiti.

Kisheria hii ikoje wadau. Na je ikibainika kwamba demu ni muhuni jamaa anaweza akamfungulia mashtaka huyo demu?

Mods tafadhali naomba mnirekebishie spelling za tittle hapo juu ni msaada na sio masaada kama nilivyoandika.

Ahsante.......
Ulaji wa police tena ana bahati police wataongeza na kosa lingine la hiyo simu ilikua kwenye pochi na kwenye pochi kulikua na hela na cheni ya dhahabu mahabusu wapo wengi sana huko wamerundikwa mwisho unaambiwa huna ndugu wenye hela wake wakutoe
 
Hapo kuna njia nzuuli sana, aende kwa mkuu wa kituo aeleze shida yake , kisha aombe kitengo cha mtandao cha polic kuangalia ile cm toka ilenunuliwa ilitumia line ngapi? Hapo ndio utakuwa mwisho wa picha
Nitamweleza aende kwa mkuu wakituo maana anasema wale polisi wengine hawakumpa hata chansi ya kuongea muda wote walikuwa upande wa demu, pia nahisi kuna afande anamega hiyo manzi.
 
hamna njama wala kuna tatizo hapo huyo demu sio chzi kaa muangalie inawezekana demu kaibiwa simu kama hyo aliiona mtandaoni inapigwa bei

mkikosa risit ajiandae na jela ana kesi ya kuiba kwa kunyang'anya atajuta kuzaliwa miaka ya kutosha
 
Mchizi anasema hawakutaka hata kumsikiliza Ila Tu walimwambia aende aliponunua simu na apewe kopi ya risiti sasa wasiwasi wake ni kwamba je hizo kopi za risiti ni kweli zinabaki madukani maana like ni duka kubwa Sana la simu na mwenye duka ni muuzaji maarufu.
...kama ni Duka kubwa la Simu hio Risiti lazima ipo, Hata kama imeishapelekwa Store huko, lakini Lazima ipo !
 
hamna njama wala kuna tatizo hapo huyo demu sio chzi kaa muangalie inawezekana demu kaibiwa simu kama hyo aliiona mtandaoni inapigwa bei

mkikosa risit ajiandae na jela ana kesi ya kuiba kwa kunyang'anya atajuta kuzaliwa miaka ya kutosha
Mimi sasa nasema huyu demu ni chizi sababu jamaa anasema demu aliulizwa toka ameibiwa simu ni muda gani umepita demu akasema ni wiki mbili zimepita, na wakati hii simu tulienda kuinunua na jamaa mwezi wa pili tarehe za mwanzoni sasa hapo huoni kwamba huyu demu akili zimeyumba!!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom