kwa wapenzi wa Ulanzi WANYALUKOLO

kwa wapenzi wa Ulanzi WANYALUKOLO

Kipindi nipo sekondary nilikuwa nakaa na at least lita kumi gheto kwangu kwani debe ilikuwa 250. Nilikuwa siendi shule bila kupiga kidogo. Walimu walinifahamu ila sema kwa kuwa nilikuwa mzuri darasani walikuwa hawanigusi. Na mwisho wa siku nikapiga wani yangu na kuoodoka. Shule za day zina ubaya wake ukiwa hujui nini unalotakiwa kufanya kwani nikikumbuka naona ulikuwa upuuzi tu.
Mkuu ilikua mwembetogwa nn?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
aisee nimekumbuka idete kwenye mapera na ulanzi,lupalama B, na ipamba kwa manesi...those time are gone now....ulanzi uliwafanya wazungu wasahau wine wahamie kwenye ulanzi...kwa waliokuwepo tosa wanamkumbuka Mr. Simon na Mr. Jonathan? (kama sijakosea) hawa jamaa walikuwa wakiwa zamu tu then wakakukamata na kosa wanaomba jiti kwa ajili ya ulanzi kama adhabu.
Lupalama B Kama kawa last Sunday nlikua kule it was much funny japo nlkw nmeenda kwa msiba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
vipi unakumbuka kina -niangushage mwenyewe! hizi zitakuwa dhambi zako mwenyewe

maisha yalikuwa ni matamu iringa tanangozi na basili la milango miwili na nyota basi servise jioni linatoka tanangozi linaingia mjini na wanywaji kibao. hii ya leo ni inside iringa kama mtu wa iringa hakuyaona haya alikosa vitu vikali sana bado hujapita nyumba ya mtu ukasikia amepiga mziki wa kidamali yaani miziki ya jaluo
Mziki wa jaluo wnyw walikua wanaita katitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baadhi ya interesting words/terms za wabena in connection kinakotokea kinywaji hiki ambazo yawezekana wabena wengi nao hawazojui: nimezipata kwenye vitabu vya dini vya kijerumani

Baba kwa kibena ni dada, kama unataka kusema baba yetu basi utasema dadisu au dadesu, baba yako ni dado

Mama anaitwa yuva, mama yako anaitwa yuvo au nyoho na mama yake anaitwa ng'ina

Bibi anaitwa papa, babu anaitwa kuhu

Dada (sister) anaitwa mhadza na kaka anaitwa mama, kaka yako anaitwa mamo

Mjomba anaitwa yaya, mjomba wako anaitwa yayo

Monday - Jumatatu - shaulembela
Tuesday - Jumanne - hivili
Wednesday - Jumatano - hidatu
Thursday - Alhamisi - hitayi
Friday - Ijumaa - hihanu
Saturday - Jumamosi - shauviluha
Sunday - Jumapili - mulungu
 
Kuna siku nimetoka zangu mkimbizi na baskeli mpaka tosa wakati wa kurudi nikanunua ulanzi wangu lita 5 nikakamua, dah ile baskeli niiona nzito kama jiwe gangilonga...nitatafuta siku nikatembelee ndugu na jamaa aisee
 
Niliishi ipogolo mpakani na kibwabwa jirani kabisa na korongoni hope enzi hizo zilikua za kina chonya na mzee makala pale ruaha

Sent using Jamii Forums mobile app
1989 to 1995 nilikuwa Iringa. Niliishi kibwabwa kutoka barabara ya lami tunaingilia pale mbele ya cotex mbele kidogo kuna bakery ya mikate then shule ya msingi kibwawa unaenda kulia mpaka sehemu moja kulikuwa na kilabu ya pombe ya myovela.
 
1989 to 1995 nilikuwa Iringa. Niliishi kibwabwa kutoka barabara ya lami tunaingilia pale mbele ya cotex mbele kidogo kuna bakery ya mikate then shule ya msingi kibwawa unaenda kulia mpaka sehemu moja kulikuwa na kilabu ya pombe ya myovela.
It means primary ulisoma kibwabwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom