kwa wapenzi wa Ulanzi WANYALUKOLO

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
270
Ulanzi
Ulanzi ni kinywaji kinachotokana na mmea ambao huota kwa wingi sehemu moja na hukua sana kwenda juu. Mimea hii ikiwa bado michanga hukatwa juu na ikishakatwa hutoa maji na kitu mithili ya povu hujaa juu ya pale palipokatwa. Maji hayo yanayotoka hukingwa kwenye kitu kiitwacho “mbeta”: halina kiswahili sahihi. Maji hayo yanayotoka ni matamu sana na tena yana uwezo wa kulewesha.Historia yake.
Inasemekana ulanzi uligunduliwa na mnyama mdogo aitwaye panya ambaye kwa mara ya kwanza waling’ata ule mmea mchanga wa ulanzi na maji yakaanza kutoka. Kila siku panya walionekana kupenda kulamba ile sehemu walioing’ata. Binadamu, baada ya kugundua hilo, walifuatilia na wakajaribu kulamba na wao, ndipo walipogundua kuwa yale maji yaliyotoka ni matamu.
Basi wakakata ile mimea michanga ya mianzi na kuona maji mengi yakitoka na kitu mithili ya povu juu yake.
Baadaye wakatumia mianzi iliyokomaa kwa kutengenezea kitu cha kukingia yale maji yanayotoka. Zinaitwa “mbeta”Maelezo
Ulanzi ni kinywaji cha asili kinachopendwa sana na watu wa mikoa ya Iringa, Mbeya na Songea, Kanda za Juu ya nchi ya Tanzania.
Ni kinywaji cha asili ambacho hakitengenezwi bali kinatokana na mti unaoitwa mwanzi.
Ulanzi unagemwa mara tatu kwa siku:
¨ Asubuhi: hugema na kutoa ulanzi kutoka kwenye vile vyombo vya kukingia (mbeta). Ulanzi huu wa asubuhi daima ni mtamu na togwa sana.
¨ Mchana huenda kugema kusudi kuweza kutoa sehemu iliyokauka ili ulanzi uendelee kutoka.
¨ Jioni: hugemwa tena na kutoa ulanzi uliomo kwenye vyombo vya kukingia. Ulanzi huu wa jioni ni mkali kidogo kwa sababu unakuwa umewakiwa na jua.
Ili kupata ulanzi ulio mzuri, wagemaji huchanganya ulanzi wa asubuhi na wa jioni ili uwe bora zaidi na kwa hiyo upendwe na wengi zaidi.
Utomvu:
Ni kitu kama uji unaotuama juu ya ile sehemu iliyokatwa kwenye kitindi kichanga kwa ajili ya kutoa ulanzi.
Kitindi
Ni mti ule unaotoa ulanzi. Kitindi ni umoja, vikiwa vingi huitwa vitindi na daima huwa vingi ili kupata vitindi vichanga vingi. Kitindi kikiwa kimoja huwezi kugema ulanzi kwa sababu kitindi kichanga hakiwezi kupatikana.
Hugemwa lini?
Ulanzi huu hugemwa kwa kipindi, kwa sehemu zilizo nyingi hasa kipindi cha kifuku (masika) ulanzi huwa mwingi sana na unazidi kupungua kadiri kipindi cha masika kinavyoisha. Lakini kuna baadhi ya sehemu ambazo zina baridi sana na hali ya ubichi kwa mwaka mzima, kwa mfano katika mbuga ya Kitulo, wilaya ya Makete (Tanzania).
Hunyweka kwa siku ngapi?
Ulanzi hunyweka kwa siku moja kimsingi hapo huwa mtamu wa ladha safi. Lakini ukishalala, ulanzi hupoteza ubora wake na hivi hauwi mtamu sana. Lakini ukichanganya na uliogemwa siku hiyo, hurudi katika hali njema tena, ingawa siyo safi sana.
 
enzi zetu tulikiita kitete! Acha bana tunatoka kibwabwa mpaka mseke au njia panda ya tosa debe sh 500 mnaogelea kabsaa! Kijombelo sh 20. Hiyo ni early 90s mpaka 95. Vijana wengi wameharibika sana Iringa sababu ya ulasi be! Tunywe ludodo be segito!
 
mwayeriko uvanzile amaligo pe kwelu?
ILIGA AMALIGO SIKWELEWA UKUTA UMU NA VAKWIVETU VALIMUMU.kama akelwike tigile pajumamosi adze kukaye nene kila wiki vakundetela mulibotolo vayilagila mu basi ya nyagawa
 
mkuu kilimasera nashukuru kwa kunikumbusha ulanzi...nshazoea mnazi xaxa....but naomba nikusahihishe kidogo. mimea ya mianzi, vitindi huwa havikui sana kwenda juu....hurefuka yapata mita tano hivi then inapinda kwenda down, na pia mbeta hazitokani na mianzi (vitindi) vya ulanzi but hutokana na mianzi mingine ambayo haitoi ulanzi bali hutumiak kwa kutengenezea mbeta na bidhaa zingine kama vitanda, nyungo, vikapu nk.
ulanzi uliokomaa sana unaitwa kilama, huu ulanzi ni full spirit kwani ukimwagia kwenye majani yanaungua,na ukiunywa bila kuchanganya na togwa afya yako ni hatihati.
 
Kipindi nipo sekondary nilikuwa nakaa na at least lita kumi gheto kwangu kwani debe ilikuwa 250. Nilikuwa siendi shule bila kupiga kidogo. Walimu walinifahamu ila sema kwa kuwa nilikuwa mzuri darasani walikuwa hawanigusi. Na mwisho wa siku nikapiga wani yangu na kuoodoka. Shule za day zina ubaya wake ukiwa hujui nini unalotakiwa kufanya kwani nikikumbuka naona ulikuwa upuuzi tu.
 
juzi nilikua nyumbani makete, nilichanganya ulanzi na safari, stimu zizotoka hapo hata baridi sikuiona...
 
mwayeriko uvanzile amaligo pe kwelu?

mwe ndekhelwikhe otolanzi na matsebele ghakhonyianya! Kitu kikipatiwa na mahindi mabichi hupati stimu ya kulewa lakini ukifika home ndo utasikilizia mziki wake. Aafu usinywe ile kitu na jua linawaka, utajuta kuufahamu.
 
juzi nilikua nyumbani makete, nilichanganya ulanzi na safari, stimu zizotoka hapo hata baridi sikuiona...

khulongu binamu! Ndinoghwa ndevuje khonyumba vatye isitsebele sidolwikhe no volanzi wolosu nhiiii!
 
Sahihi.
Addition;Yale mapovu yanaitwa "maboso". Ulanzi uliopita umri wa masaa 24 unaitwa "mkangafu"

sedments zile ndo zinaitwa maboso, wakati yale mapovu yanaitwa Lifulo au mafulo kwa uwingi. Lakini otherwise tunashukuru kwa kutukumbusha tulikotoka. Twilumba hiilo
 
Back
Top Bottom