Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Weekend ilisindikizwa na imitation


Ila mmh sijui kiranga gani kilinipata nikaionja hospital playlist kushtuka nipo episode ya 10 kukurupuka hadi wa leo hakuna episode ya 11 halafu ya kumi imeishia patamu. Ongoing ni majanga

List zangu

Imitation(episode 12)genre music,romance,comedy

Rich family's son (episode 100)family drama

Nevertheless(sijaianza)

Modern farmer(episode 20)

Love from today(episode 100 na kitu)

Queen in hyun's man

The spies who loved me(boring ila naenda nayo hivyo hivyo)

family drama navuta kidogo kidogo bahati nzuri zina episode chache hata kwenye server ya FE unapata saiz ya 360
 
"Sang Do" hii ni moja kati ya series kali kati ya ambazo nimewahi kuziona, ITOSHE kusema ni series kali. Zile dhana tunazojifunza huko Vyuo vya walavi kuwa Mjasiliamali ni Risk taker, Restless, sijui anajua ku spot opportunities, anabadili shida kuwa fursa, sijui Ups and downs,, yote utayakuta humu ndani.
nimeshaimaliza kuitazama hii drama, fanya basi kunitumia mtaji wa millioni 100 ili nianzishe biashara yangu na nakuahidi utapata gawio la 20% itakayotokanwa na faida itakayozalishwa, ila usisahau hii biashara niliyoilenga muhasibu nitakuwa mwenyewe (P&L statement itakuwa ni lose kwa miaka 10 kama zilivyo kampuni za uchimbaji madini)
=====================

kizazi cha dhahabu cha wakorea kupitia tasnia ya uigizaji kinachukuliwa na upepo wa umri na hakitoweza kurudishwa tena, ukiwangaalia hawa wazee waliozaliwa kuanzia mwaka 1930 hadi walioshia kuzaliwa mwaka 1969 wanakupa burudani kubwa sana ya kiuigizaji iliojaa tafakari ndani yake yenye kuambatana na mzigo wa maswali yasiojibika.

hiki ninachokishuhudia kwenye televisheni yangu kina uhusiano wowote na maigizo au ni kinyume chake?

kuna hii generation ilioanzia mwaka 1970 nayo inajitahidi sana na bila ya shaka wataziba nafasi za wazazi wao pindi watakapopata pumziko la milele ila nikiwaangalia hawa mabishoo wa siku hizi wanaopakwa lipstick wananipa wasiwasi sana kama wataweza kufikia level ya ubora wa hicho kizazi, wengi wao hubebwa zaidi na umaarufu wao uliochangizwa zaidi na muonekano wao.

Mungu ajaalie pindi hii sanaa ya wakorea itakapomilikiwa moja kwa moja na utamaduni wa kimagharibi niwe nimeshatundiga daluga kufuatilia sanaa yao.
AMEN
 
dae una vituko. Mie nimeganda kwa airtel walipo nipo nao kwa night bundle hope hawatabadili watatutesa sana
namiliki line za mitandao yote maarufu nchini, hao Airtel ninavyowatamani majira ya usiku lakini ndio hivyo network inakuwa spidi ya kobe.
ukipata ubuyu wa unafuu wa MB usisite kunishitua
Halotel mungu anawaona kwa walichotufanyia
 
Jung Ho Keun mwamba namkubali sana.
Hiyo, on rooftop inahusiana na nini?.

Mie bado nipo episode ya 33/50( Sang Do), hii tabia ya kufuatilia series za miaka ya zamani wewe Daemusin ndie uliyeniambukiza mara baada ya kunipa recommendation ya The Age of warriors( 2003), Wang gun( 2000-2002). Kisha nianza kunogewa zaidi nilipoitafuta Dae jang geum( 2003), Damo( 2003), Emperor of sea( 2004), Yi san( 2006), The Great King Sejong( 2008). Na sasa nipo kwenye Hur Jun(1999-2000) na Sang do(2001-2002). Endapo nitazimaliza nitatafuta zingine japo changamoto kubwa huku( miaka hii ya zamani) baadhi ya Series kali hazina subtitles.
Kuna mtu atakwambia hapendi kuangalia series za zamani sababu ya quality, lkn kwa mtu apendaye story nzuri huku ndo kwao.

pichani ni muhuni wenu huyu nipo naye kwenye Hur Jun na Sang do, kote ni mzee Wa Fitna. Kiukweli anaziweza fitna huyu mwamba.View attachment 1923328
 
Nimemaliza Penthouse nimeipenda sana

nataka niangalie Cruel Palace je ni nzuri?
kiupande wangu sina majibu, niliangalia episode 5 tu takribani miaka 4 iliopita.
kikubwa nilichokiona labda niseme ni harakati za mwanamke zilizochochewa na kisasi, zinazomzalishia ndoto ya tamaa za kuumiliki mfumo dume kwenye ulingo wa siasa kwa kumtumia mwanawe baada ya kuonjeshwa ladha ya maisha ya familia ya kifalme.

labda nimwite huyu mkorea wa kizimkazi anayeitwa Great Conqueror anaweza kukupa tathmini yake
 
Song Il Kook is considering to lead a new drama 'Killer Queen' which deals with the story of a psychiatrist who becomes the daughter-in-law of a chaebol.

This will be his small screen comeback after 5 years.
1631138712348.png
 
Back
Top Bottom