Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Emperor Wang Gun
Nimefanikiwa kufika Episode ya 106/200. Haikuwa rahisi kufika hapa, safari niliianza mwezi wa 6. Kila Episode ina wastani wa Dk 50-55, najua kuna watu hawajawahi kutazama drama ya yenye Episode 60+.
King Gung Ye:

Mara ya kwanza alikuwa anaonekana shujaa na mtu aliyewaongoza wenzie kukemea Uovu na kuwasihi watu wawe wema, si kwa maneno tu bali kwa Matendo. Lakini sasa amegeuka kuwa Mkatili.

King Kyeonn Hyeon:

Jamaa ni mtu mgumu huyu na shujaa wa Taifa lake.

Wang Gun:


anaendelea kujifunza mengi lakini pia ndiye nguzo kwenye Taifa la Taebong.
Katika majenerali wake Park Sulhee, ndiye namkubali, Jamaa ukimuona kama muhuni ama mjinga mjinga lakini kichwani yuko vizuri.
#ThrowdownContinues
 
baada ya kumaliza kuvuta bangi zangu nimeona niitikie wito.
ni kweli daemusin alikuwa na series takribani 30 lakini mwezi uliopita nilifanya operations safisha Kujimwambafy, si hivyo tu

hata nyakati hizi nikiangalia drama naishia kuzifuta episodes pindi ninapomaliza kuangalia (nimechokwa kunyonywa damu na parasites wasiojielewa wanaomsubiria daemusin kila siku awape series wakiamini nina undugu na madirectors), hivyo basi nahofia mchango wangu utakuwa ni mdogo sana kwa sasa.

nitajaribu kuangalia harakati za wadau wenyewe kama watakuwa serious hususani kinidhamu sioni tabu kuzidownload upya baadhi ya drama then nikaziupload hususani hizi zinazoendelea au zile zilizokwisha karibuni.

ngoja kwanza niirudishe telegram application kwenye PC then nitaangalia cha kufanya.
 
Duh.. Mbona kama linguistics ya KATAMBA, F. (2008)
 
Daemusin unahitajika hapa japo sipo telegram ila ukikubali nitajiunga huko
ndio mumeamua kuandaa petition ya kumtaka daemusin bin makinikiyya bin Kujimwambafy arudi telegram.

kwani kuna utofauti gani wa gharama pindi unapodownload episode moja kwa moja kwenye tovuti na kuapload kwenda kwenye group la telegram?

nijibuni hilo swali kwanza tafadhalini
 
wewe bwegeee wengine tumesoma mwari hakogi primary school, ndio nini kutuwekea lugha ya kibabe haliyakuwa unafahamu fika wengine uwezo wetu ni kuandika sentensi dhaifu za kiingilishi.

I DONTI ANDERSTANDING ANYTHING
Hayo mengine sijui, kwani miye ndo niliyekwambia uzaliwe kolomije? Sie wakati tunachagua Pyeongyang wewe ulipendelea huko. Kila mkulima atakula alichovuna.

ila Be active
 

Huwa nawaza mambo kadhaa hiyo series ya my country
1- wataweka zile action za kama kwenye sic flying dragons
2- muhyul (aliyekuwa mlinzi wa yi ban won) character wake yuko??
3- na wale mapacha wazee kazi mpaka moja wao akauliwa na leebang ji nao character yao iko ??
Ect
 
sijapata bakuli la urojo mpaka muda huu kwa sababu ya mvua hivyo basi acha nikujibu kama mwanadamu aliyezaliwa msimu wa njaa kama mayala paskali
  1. ubora wa drama na muigizaji haupimwi kwa kuangalia action pekee ila kama ni mpenzi wa action basi zimo.
  2. swali lako la pili ni sawa sawa na kumuuliza aliyeangalia kingdom of the wind drama baada kumaliza kuangalia jumong drama (je maro, hyeop bo, o yi, sayong, na wengineo watakuwemo?)
  3. muhyul hayumo kwa sababu historia yake haijaleta athari yoyote kubwa ndani ya joseon
  4. kama hayumo jung do jeon pamoja na greath thinker poeun unadhani watakuwemo hao mapacha wanaorembuwa macho kama samaki pono?.
mkuu jaribu kuiangalia huenda ikakuvutia
 
Hayo mengine sijui, kwani miye ndo niliyekwambia uzaliwe kolomije? Sie wakati tunachagua Pyeongyang wewe ulipendelea huko. Kila mkulima atakula alichovuna.

ila Be active
usinilaumu mimi ila walaumu mababu wa mababu zangu waliohama kenya nyakati hizo wakaja zanzibar kutafuta karafuu ndio maana sijui kiingilishi ila najivunia lafudhi yangu ya kiswahili iliobora zaidi kwa mwambao huu wa Afrika mashariki na kati.
bwege weweeee
nasikia huko kwenu panya kwa jina jengine ndio pilau masala.
 
Daemusin unahitajika hapa japo sipo telegram ila ukikubali nitajiunga huko

yes
daemusin amekuwa ni member wa 13 kujiunga ndani ya channel.
huko kwa Prime minister foleni za mara kwa mara hazitokukera?
niemefurahi kuikuta drama yangu pendwa ya secret forest season 1.
naisubiria season 2 yake inshaallah mnamo mwaka 2020.
 
Sikuwah Kula Urojo Kabla, Ila Kuna Siku ndugu Yangu Alinishawishi, Tangiapo Nimetengeneza Urafiki Nao, Mimi na Urojo Ni Machingu.

Ila We Binadamu Una Maneno Sana. Wanarembua Macho Kama Pono Dah!
 
Sikuwah Kula Urojo Kabla, Ila Kuna Siku ndugu Yangu Alinishawishi, Tangiapo Nimetengeneza Urafiki Nao, Mimi na Urojo Ni Machingu.

Ila We Binadamu Una Maneno Sana. Wanarembua Macho Kama Pono Dah!
umeona eeeeeee
nashangaa utavikuta vijitu uchwara vinauwekea ngumu urojo.

kachori
mishikaki
bagia za kunde au dengu
chipsi za muhogo
salad
katlesi ziwe za mbatata au mayai.
ongeza na maji ya urojo
pembeni yako una juisi kama una uwezo kama huna tafuta kopo la maji ya chai yasiokuwa na sukari unywe
chapati/ mkate/ maandazi

unakosaje mchanganyiko kama huu?
tuwashukuru sana wahindi kwa kutuletea vitafunwa pendwa.

nyinyi endeleeni kula sembe mchana kutwa kama mumeishiwa mazao mengine, ndio maana hamuna mapozi munapozungumza.

aisee mutuuu hebu nileteee hilo libaaakuli la daaagaaaa na hiyo sembe tutengeneze chakula pendwa kama biryani.
 

Hii Ya Chini Ndo Lafudhi Ilokosa Pozi Ama!?

Hahahaha, Mola Akueke.
 
si ndio munavyozungumza wengi wenu mukishabugia unga wa sembe matumboni mwenu.
pikeni japo wali basi baadhi ya nyakati.
tena kwenu mchele safi unapatikana cha ajabu sisi ndio tunaununua kwa wingi.

Naona Unaleta Jeuri Ya Kiunguja Etii Eeeh!!

Ugali Unaleta Nguvu Haujui Ama!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…