Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kazz0

Kazz0

Member
Joined
Mar 15, 2015
Messages
48
Points
95
Kazz0

Kazz0

Member
Joined Mar 15, 2015
48 95
Kama wewe ni mpenzi wa Korean Dramas, karibu katika thread hii tupate ku share kuhusu kazi hizo hatari za mkorea.

Tuambiane;

- Ipi ni drama yako bora ya kila wakati kwako?

- Ni ya aina gani? (Wengi tumezoea kusema za 'mjini' na 'vijijini')

-Nini kinakuvutia sana katika hiyo Drama?

Pia:

- Nani ni Msanii wako Bora wa kiume na wa kike na baadhi ya drama alizoigiza?

- Nani ni sexiest Actor au Actress kwa maoni yako?

- Ipi ilikua Drama yako ya kwanza ya kikorea kuiona?

- Ni Drama gani ya kikorea unaitafuta sana na unapata wakati mgumu kuipata? (Unaweza ukasaidiwa kuipata na mashabiki wengine)

*Pia tumia thread hii kufahamishana kuhusu drama mpya zilizotoka au unayohisi ni nzuri ila haijapata umaarufu sana!!

Karibu tujumuike! Saraghae! Kumooyo!!

=========

Baadhi ya Links za Dramas mbali mbali za Korea...;

Be Strong Geum Soon

Princess Ja Myung Go

THREE DAYS (2014)

Swallow the Sun

Jumong

King Guenchoggo

=====

Links za ku-download drama za Kikorea;

- Watch Drama Online | Korean Drama | Japanese Drama | Taiwanese Drama | Hong Kong Drama | Chinese Drama
- GoodDrama.Net


======

Updated: Kwa mjadala na kubadilishana uzoefu kuhusu series za jumla za movies mbalimbali, za zamani na mpya, Unaweza pia kufuatilia UZI HUU hapa Series (Special thread)
..

Kazi kwako.. Enjoy!
 
Daemusin

Daemusin

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Messages
6,328
Points
2,000
Daemusin

Daemusin

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2015
6,328 2,000
Mpindue tu.
usinione nipo kimya bado nafikiria cha kukujibu na huenda jibu langu kwa njia ya maandishi likachukua muda mrefu :p:p
ngoja nianze na jibu hili kwanza then pengine mwaka ujao inshaallah nitawasilisha jibu la maandishi rasmi

ndoto imenifanya nikumbuke ujinga wa kuchelewa kwangu mpaka eunseom amekuja kuniibia.
kumbe anayeotwa alikwisha nifungulia milango zamani ila sikuwa nafahamu hilo.:p:p:p
anyeong
 
aminas

aminas

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2015
Messages
3,132
Points
2,000
aminas

aminas

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2015
3,132 2,000
usinione nipo kimya bado nafikiria cha kukujibu na huenda jibu langu kwa njia ya maandishi likachukua muda mrefu :p:p
ngoja nianze na jibu hili kwanza then pengine mwaka ujao inshaallah nitawasilisha jibu la maandishi rasmi

ndoto imenifanya nikumbuke ujinga wa kuchelewa kwangu mpaka eunseom amekuja kuniibia.
kumbe anayeotwa alikwisha nifungulia milango zamani ila sikuwa nafahamu hilo.:p:p:p
anyeong
Hmm! Haya Nasubili Hayo Maandishi
 
M

Mikate

New Member
Joined
Sep 8, 2019
Messages
1
Points
45
M

Mikate

New Member
Joined Sep 8, 2019
1 45
Asee kwangu mm Kuna movie inaitwa CITY HUNTER asee ile movie naeza irudia ata mara miaaa jamaa alieigiza anaitwa LEE MIN HO
 
aminas

aminas

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2015
Messages
3,132
Points
2,000
aminas

aminas

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2015
3,132 2,000
naombeni msaada jamani mwenzenu nijue nikitaka download hizi drama kwa urahisi nafanyaje
Nenda kwenye Site Moja Inaitwa MyAsiantv.se Umo Utakuta Kila Drama Unayotaka Kuangalia na Hata Kudownload.

Daemusin Msaada.
 
Numbisa

Numbisa

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2016
Messages
142,973
Points
2,000
Numbisa

Numbisa

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2016
142,973 2,000
KWA WANAOJUA JINSI YA KUDOWNLOAD KOREAN DRAMA JAMANI NAOMBA ANIEFUNDISHE
Tumia uc browser

Ingia google andika daebakdrama.com ingia humo tafuta movie uitakayo click utaona maneno click download fata hatua utaweza

Ukiikosa drama uitakayo humo ingia kissassian au dramanice search drama kisha click download chagua rapidvideo utadownload vizuri
 
Product

Product

Member
Joined
Sep 7, 2019
Messages
70
Points
125
Product

Product

Member
Joined Sep 7, 2019
70 125
Tumia uc browser

Ingia google andika daebakdrama.com ingia humo tafuta movie uitakayo click utaona maneno click download fata hatua utaweza

Ukiikosa drama uitakayo humo ingia kissassian au dramanice search drama kisha click download chagua rapidvideo utadownload vizuri
Asante Numbisa nipo naugulia maumivu ya bando langu,maana sikujua kama ingekua simple kiasi hiki.

Nawaza pa kupata external kubwa hapa maana usiku wa leo TOBOA NIGHT nitalitumia ipasavyo..

😍😍😍😍
 
I

innocent dependent

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Messages
604
Points
1,000
I

innocent dependent

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2019
604 1,000
Katka kuangalia season kwang sijawah kuona season kali kama hyo, na nmehangaika sana kutafuta zaid ya hyo mpaka sasa ni sawa na chinese drama season kali kama God of war.
Nielezee kidogo hiyo six flying dragons inahusu nini?
 
Numbisa

Numbisa

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2016
Messages
142,973
Points
2,000
Numbisa

Numbisa

JF-Expert Member
Joined Dec 12, 2016
142,973 2,000
Nice pia kuna dramacool9.co hata mie nilishawahi kupoteza bando pale dramania ilipogoma na harakati za kutafuta mbadala wake.

Hio toboa night ni ofa ya mtandao gani?
Asante Numbisa nipo naugulia maumivu ya bando langu,maana sikujua kama ingekua simple kiasi hiki.

Nawaza pa kupata external kubwa hapa maana usiku wa leo TOBOA NIGHT nitalitumia ipasavyo..

😍😍😍😍
 
Daemusin

Daemusin

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Messages
6,328
Points
2,000
Daemusin

Daemusin

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2015
6,328 2,000
Hutaki kuitwa Mkuuu Eeenh!

Arthdal Mbona Haijarudi Kama Nilivyoitegemea...!
kuna uwezekano kabila la white mountain ndio chanzo kikuu cha matatizo yanayojiri kwenye ardhi ya arthdal, inavyosemekana aramun haesulla (aliyeunganisha makabila ndani ya ardhi ya arthdal) asili yake pia alikuwa ni igutus ila cha kushangaza hiki kizazi cha bibi Asa sin wakiongozwa na Asa Ron wanakwenda kinyume na uhalisia wa mambo kwa kuficha ukweli tokea kuondoka kwa huyu bibi takribani miaka mingi iliopita.

season 1 and 2 tumepata kushuhudia nguvu ya damu ya huyu bibi Asa sin jinsi ilivyoweza kutapakaa mpaka kwenye ardhi ya Iark linakopatikana kabila la wahan(wahan tribe) na hatimaye imegundulikana ya kwamba Tanya ndiye mrithi halali wa kizazi cha Asa sin mwishoni mwa season 2.

kama aramun haesulla asili yake ilikuwa ni igutus basi hakuna ubaya wowote endapo kama atajitokeza mwanadamu mwengine mwenye asili ya igutus kuitawala ardhi ya arthdal, bahati mbaya sana Asa Ron na wenzake kwa kutumia nguvu ya kabila lao pamoja na ushawishi wao kidini kama tunavyofahamu dini hubeba nguvu kubwa sana pindi inapotumiwa kwenye siasa either kwa nia njema au kinyume chake wamewaaminisha wananchi wote wanaounda makabila ndani ya arthdal ya kwamba igutus na binadamu jamii ya neanthal ni wanadamu hatari na wanapaswa kusambaratishwa.

khofu hii walioijenga kwenye mioyo ya wananchi ndio iliopelekea hata baba yake tagon atumie kila njia ikiwemo kutoa uhai kwa wasiokuwa na hatia ili aifiche asili ya mtoto wake ili asijulikane kama ni igutus, khofu hii pia ilimwingia tagon mwenyewe ndio maana na yeye ameendelea kuificha asili yake na hata kuficha asili ya mtoto wa kumlea ambaye ni Saya.

kama ingeliwekwa wazi historia ya aramun haesulla basi tagon angelistahili kupewa heshima ya reincarnation ya aramun haesulla bila hata ya kumwaga damu kama itakavyotokezea episode ijayo kwa sababu na yeye asili yake ni igutus japokuwa hajawahi kuendesha farasi wa kanmoreu kama alivyofanya eunseom.

ningelipenda tagon pindi atakapofanikiwa mapinduzi yake ya umwagaji damu dhidi ya kabila la white mountain na wafuasi wao wakiongozwa na Asa Ron atatangaza hadharani ya kwamba yeye ni igutus na atathibitisha hata aramun haesulla mwenyewe alikuwa ni igutus hivyo basi hakuna ubaya wowote kwa igutus kuchanganyika na saram (binadamu wa kawaida)
1568405521685-png.1206696
 
Daemusin

Daemusin

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Messages
6,328
Points
2,000
Daemusin

Daemusin

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2015
6,328 2,000
Nimependa Saya Anavyomuaangalia Tanya.. (Siri Yako Usiseme)
saya afanana na popo kwa sababu hajulikani upande upi aliyoelekea kitabia (wema au uovu), ila jambo kubwa linalomuathiri ni malezi alioyapata tokea utotoni kupitia kwa wanadamu wawili waliojawa na tamaa za kimadaraka na ubinafsi, hatimaye na yeye amerithi tabia zile zile za wazazi wake ila tofauti kubwa ni kwamba uovu wake umezidi zaidi kwa sababu ya elimu alionayo ambayo mara kwa mara amekuwa akiitumia vibaya.

unaweza kujiuliza kwa nini aliamua kumwekea sumu kaka yake tagon?
je ni kweli ana mapenzi ya dhati kwa Tanya au ndio anataka kumtumia ili afanikishe malengo yake na baba yake?
hayo yote anayoyafanya na kuyapanga je ni kweli dhumuni lake kuu ni kuwathibitishia wananchi ya kwamba hata igutus wana haki ya kuheshimiwa au ana lengo jengine ambalo ni kupata madaraka pindi atakapoondoka tagon?
1568410510139-png.1206715
tofauti kubwa iliopo kati ya saya na eunseom ni kwamba eunseom ni mwanadamu ambaye yupo tayari kutoa msaada kwa anayeuhitaji muda wowote bila hata ya kutegemea kulipwa ujira wowote baadae ndio maana baadhi ya watu wanamshangaa kwa ihsani na wema alionao. ndio maana hata momo tribe wakiongozwa na mwanadada mwenye asili ya kijapani (erika karata) anayetumia jina la xabara ndani ya drama ameanzisha kampeni ya kumtafuta eunseom baaada ya kuwapa msaada na kusepa (nafikiri watataka awe kiongozi wao)

episode ya 14 nimeona tagon na taelha wameshaandaa mikakati ya kwenda kubeba makabila mengineo kwa njia ya upanga ila sidhani kama watafanikiwa kwa sababu namuona eunseom akichaguliwa kuwa kiongozi wa makabila mbali mbali ikiwemo ago tribe na wale jamaa wanaoogopewa wanaojipaka rangi (momo tribe), hii inamaanisha ya kwamba hatimaye eunseom anakwenda kukusanya nguvu itakayomsaidia kuiangusha nchi ya arthdal inayotawaliwa na tagon.

eunseom amebarikiwa kuwa na sifa za kuwa kiongozi kwa sababu ya tabia zake za kupenda haki na usawa kwa jamii na pia kupenda kwake kutoa msaada kwa wanaohitaji tofauti na tagon na mwanawe saya ambao wote kwa pamoja wanajaribu kutumia reference ya maisha yao magumu waliopitia kama ni kigezo tosha cha kuwafanya wayapambanie maisha kuelekea njia ya peponi hata kwa kumwaga damu isiyokuwa na ulazima.
rejea mauaji ya neanthal species pia rejea uvamizi dhidi ya wahan tribe.
tagon alitekeleza mission zote mbili kwa sababu apate kuendelea kuishi mjini kwa sababu baba alishamwambia aondoke mji mkuu ili asije akamletea balaa ndipo tagon akamwambia baba yake nipo tayari kukupa zawadi ya ardhi ya neanthal na watumwa kutoka wahan tribe ili nipate kuendelea kuishi makao makuu.
kilichotokezea baadae tagon pia alimuua baba yake mzazi.​

kama ni shida basi aliyepata shida zaidi ni eunseom lakini bado hajakata tamaa na wala hajawahi kutumia kipaji chake na uwezo alionao kwa ajili ya kuwaonea wengineo ili afanikishe malengo.

hivi kwa akili ya kawaida tagon angeliweza kumsaidia yule jamaa aliyewauza eunseom na wenzake kwenye kambi ya utumwa, dah! yule fala aliwatesa mnoo lakini eunseom akaona acha nimsaidie na mwisho alimwambia.
"naomba ukumbuke leo hii umesaidiwa na igutus (uliyekuwa ukimtukana na kumtesa kama mnyama)"​

igutus = binadamu aliyezaliwa na mzazi mmoja akiwa ni neanthal na mwengine ni saram (binadamu wa kawaida) kwa mujibu wa drama lakini a.k.a mixed race
1568410074449-png.1206713
 
Daemusin

Daemusin

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Messages
6,328
Points
2,000
Daemusin

Daemusin

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2015
6,328 2,000
Hahahhahaa. Kama Yule Muhuni Aloongozana Na Eunseom Kwenda Kwa Hao Mabaharia Yaani Yule Ndo Baharia Kabisaa.
kadri anavyoendelea kujiweka karibu na eunseom naamini ipsaeng atabadilika kitabia na atakuwa mtu muhimu sana kwa eunseom hususan kwenye safari yake ya kutafuta power kupitia makabila tofauti na yeye ndiye atakayeshuhudia mara kwa mara tabia njema alizonazo eunseom pamoja na ungwaji mkono atakaupata kupitia jamii tofauti
wenyewe wanasema ukikaa na mlevi na wewe utakuwa mlevi hivyo hivyo ukikaa na mtu mwema kama eunseom utaadilika kimatendo japo kwa 80%.

kuna uwezekano ipsaeng anatokea kwenye makabila yenye nguvu lakini yaliyomtokezea huko nyuma ndio yamemfanya awe na tabia za ajabu ajabu ikiwemo tamaa na usaliti. yaliyomkuta huko nyuma huenda ndio yamempelekea asiwaamini binadamu hata kwa sekunde 10

pia nina wasiwasi huenda anatokea ago tribe kabila ambalo kwa muda mrefu limekuwa kwenye vita zisizokwisha, kama utavuta kumbu kumbu season 1 episode 2 mwanzoni kabisa kuna nyakati tagon alikuwa anawambia wafuasi wake
"nimesikia kabila la ago wamerudisha amani na utulivu lakini muda wowote huenda wakatwangana tena"

kuna nyakati walipokuwa wamelala kwenye barafu alikuwa anamtaja inaishigi, moja kati ya legend god wanaoheshimiwa sana na kabila analotokea na inasemekana jamaa aliwahi kuokoka kwenye maporomoko ya maji na akaendelea kuwa hai, kama umeangalia preview ile yenye dakika 5 kuna nyakati eunseom anapewa mtihani wa kutupwa kwenye maji ina maana kama atasalimika huenda lile kabila lile watamchukulia eunseom kama ndiye reincarnation ya inaishigi.

momo tribe + ago tribe + wahan tribe + neanthal + white peak tribe + mubaek = eunseom
tagon na wafuasi wake kazi wanayo hapo mbeleni.

1568412469172-png.1206724
 
Daemusin

Daemusin

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Messages
6,328
Points
2,000
Daemusin

Daemusin

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2015
6,328 2,000
nimeota ndani ya ardhi yenu mutatoana roho wenyewe kwa wenyewe - ragaz
hatimaye utabiri wa ragaz unakwenda kutimia kwenye episode 15, tagon atawasambaratisha wale wote waliofanikiwa kuifahamu siri yake ya kwamba yeye ni igutus na pia ndiye aliyemuua baba yake mzazi.
mwenyewe anasema hapendi kumwaga damu ya wasiokuwa na hatia na alitamani kuwa mtawala atakayeleta usawa kwa makabila yote lakini sidhani kama itawezekana tena.

sijui ni lini tagon ataiweka siri yake hadharani ya kwamba yeye ni igutus.
kwa nini anaogopa na yeye ndiye aliyeshikilia makali ya kisu.
heshima kwake jang dong gun ahjussi kwa zawadi aliotupa mwaka huu baada ya suit drama.

kuna taarifa zisizo rasmi kwa asilimia 100 zinadai ya kwamba kuna uwezekano arthdal chronicles tukashuhudia tena muendelezo wake mnamo mwaka 2020, pia upo uwezekano wa hii drama kutengenezewa character games.
1568413644459-png.1206725
 

Forum statistics

Threads 1,336,224
Members 512,562
Posts 32,531,264
Top