Mungu ametupa uwezo wa kuweza kutambua hisia tulizonazo na hata zile hisia za wenzetu wanazokumbana nazo kila siku, kadiri ninapoiangalia
when the camellia blooms mawazo mengi hunijia kichwani mwangu (mawazo hasi na chanya).
hisia za kimapenzi zimebeba maajabu makubwa sana, unaweza kuwa na uhusiano wa muda mrefu na mwenza wako lakini akashindwa kukupa furaha ndani ya nafsi yako na ukamuona si chochote kwako, ajabu zaidi kwa muda mchache unaweza kujikuta unaanza kuvutiwa na mr/ mrs x ambaye ameanza kukufanya uwe na amani ya nafsi ulioikosa kwa bwana / bibi yule kwa muda mfupi muliofahamiana.
sitoshangaa tena kuwaona wadau humu ndani wanaanzisha mahusiano ya kimapenzi japokuwa wanafahamiana kwa njia ya keyboard, hisia za mapenzi ni zaidi ya biashara ya kujichua inayopumbaza na kulemaza (nimekusudia kujichua mgongo jamani)
daemusin na gong hyo jin ni marafiki kuanzia leo, utakapomuona daemusin ndio umemuona
gong hyo jin.
wanaojipendekeza kwa daemusin / gong hyo jin wakome na wachakae.
nataka niachane na imani ya buddha kumbe mapenzi yana raha na utamu kuliko pilau la krismasiaaa nililoalikwa na
Khantwe ahjummaaaa.
kang ha neul humu ndani amebeba uhusika wa ajabu sana, jamaa ni mwehu mnooooo.
sielewi ni sababu ipi inayowafanya wazazi waliotelekezwa kimahusiano wawe ni wagumu sana kuzipokea hisia mpya za
kimapenzi kutoka kwa wengineo iwe ni mwanamke au mwanamme, nafahamu kuna uoga fulani huja pindi unapopitia ugumu kutelekezwa kihisia na mwenza wako wa mwanzo lakini binadamu hatufanani bwanaaaaa.
hivyo basi si sahihi hata kidogo kutuangushia nyumba ya lawama wengineo tusiohusika na breakup zenu pindi tunapoamua kuwatokea kwa lengo jema la kuanzisha mahusiano.
jamani bongo movies mpaka stori nyepesi kama hii munashindwa kutengeneza, location za uswahilini, mavazi ya ushwahilini, maisha ya uswahilini, mpaka vyakula vya uswahilini.
mdogo mdogo tumeshagonga 10% kwa kuangaliwa kila siku ya jumatano na alhamisi.
single mother oyeee =
when the camellia blooms drama.
single father oyeee =
one night spring drama.