Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Age Of Warriors.. Hawa wahuni ni nyoko. Nimejikuta kama " Emperor Wang Gun" naitazama mara mbili mbili, mara ghafla nikajikuta Naikumbuka "King Gwanggaeto the Great Conqueror", 'Dae Joyoung',. "Jeong Do Jeon" 'Great King Sejong' n.k
Hawa wahuni wanajua kucheza Historical Drama, sio hawa ndugu zake Daemusin mabishoo Seoul, kaZi kuuza sura. Hehehhe na Jinsi nionavyo Hizi Sura usitegemee scene ya mapenzi.
 
Age Of Warriors.. Hawa wahuni ni nyoko. Nimejikuta kama " Emperor Wang Gun" naitazama mara mbili mbili, mara ghafla nikajikuta Naikumbuka "King Gwanggaeto the Great Conqueror", 'Dae Joyoung',. "Jeong Do Jeon" 'Great King Sejong' n.k
Hawa wahuni wanajua kucheza Historical Drama, sio hawa ndugu zake Daemusin mabishoo Seoul, kaZi kuuza sura. Hehehhe na Jinsi nionavyo Hizi Sura usitegemee scene ya mapenzi.
humo ndani wakitongozana ni full kituko.
mwanamke na mwanamme wanakaa umbali wa mita 100 kama GK wa team A na B.

mwanamke: nakupendaaa
mwanamme: unasemaje sijasikia
mwanamke: nimesema nakupenda general
mwanamme: aaaahhhhh kumbe nije na panga huko uliko.
 
Daemusin!
Mimi sina uelewa sana na siasa, ustaarabu na uchumi wa nchi za Korea. Ila nimetokea kuvutiwa sana na huu mfumu ulioko kwenye makampuni kama Samsung,Hyundai etc..
Chaebol
naomba ukipata muda unieleze nielewe vizuri huu mfumo maana nimeusoma toka 2017 ila nimeelewa juu juu. Mimi hua ni mtupu kwenye masuala ya hesabu za fedha
 
mkuu niruhusu nikusahihishe japo kidogo:
  • jeong gwang leol ameshiriki kwenye guam heo joon ya mwaka 1999 na si mwaka 2013 kama ulivyoandika hapo juu.
  • guam heo joon ya mwaka 2013 muigizaji mkuu alikuwa ni marehemu kim ju hyeok.
  • pia mwaka 1975 kupitia kituo cha MBC muigizaji kim mu saeng ndiye aliyeigiza uhusika wa dr heo joon, huyu mzee kim mu saeng ambaye pia ni marehemu ndiye baba mzazi wa late actor kim ju hyeok. Heshima ilioje kwa wanafamilia wawili kwa nyakati tofauti kuigiza uhusika wa mwanadamu genius kwenye sekta ya afya anayeendelea na atakayeendelea kuheshimika ndani ya korea na nje ya mipaka yake.
Ahsante mkuu kwa masahihisho.

Nilidhani ndugu muuliza swali alihitaji ushiriki mwingine wa Yeong-po, yule wa kwenye Prince of Legend (Jumong) ama kwa jina lake halisi la Won Ki-jun ambaye ameshiriki pia katika hiyo Gu Am Heo Joon 'Remake' ya mwaka 2013. Ila kama ni mzee Jeong Gwang-leol, Yeah! upo sahihi kuwa ameigiza 'Orijino' Gu Am Heo Joon ama Heo Joon ya mwaka 1999.
 
Hiyo series ya the empress ki Togon au mfalme wa yuan atakufa? Maana me bado sijaimaliza
Pengine mpaka sasa hivi utakuwa umekwisha kuimaliza hiyo 'Empress Ki' na kwa maana hiyo utakuwa umepata jibu la swali lako ndugu.

Kama bado hujaimaliza basi nakushauri uimalizie ili upate jibu la swali lako maana kwa kitendo cha kulijibu swali hilo kunaweza kumuondolea hamu ya kuitazama Drama hiyo mdau ambaye bado hajapata kuitazama na kuimaliza.

Ila katika historia ni kweli alikufa.
 
Wadau Nisaidieni series nzuri 5 za mwka 2018/2019 sanasana zi base kwenye genre ya comedy.

Niliipenda sana " The fiery Priest" na mwanadada "Lee Ha-Nui" alinivutia sana ila nilipokuja kumfwata tena kwenye "Please Come Back, Mister" ameniangusha sana. Hivyo nataka niachane nayo, naombeni msaada wa zipi nzuri 18/19
Duh! kukutajia Comedies 5 nzuri ndani ya kipindi hicho kifupi cha 2018/2019 ni 'Limited' kimtindo maana nzuri nyingi zipo ila katika miaka tofauti tofauti kuendana na mitazamo ya kila mdau katika tasnia.

Mfano, kuna hiyo uliyoitaja hapo, 'Come Back Mister' ni Comedy nzuri sana ila ni ya mwaka 2016. Pia kuna 'Kill Me Heal Me' ya mwaka 2015 ambayo pia ni moja ya Comedies nzuri "kwa maoni yangu".

Nyinginezo ni;
  • Legend Of The Blue Sea (2016-2017)
  • Suspicious Partner (2017)
  • Introverted Boss (My Shy Boss) (2017)
  • Welcome To Waikiki (2018)
  • Strong Woman Do Bong Soon (2017)
  • I'm Not A Robot (2017-2018)
Na kuna nyingine ya kitambo kidogo, 'Master's Sun' ya mwaka 2013.
 
Back
Top Bottom