Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Nimekukosa Pia!

Likizo Iyo Vipi Unaenda Wapi!?

Ndo Hutaki Kumuangalia Shemeji Wako Chang Wook Ni Nzuri Ile Drama Icheki Kwanza Ndo Uende Likizo Puleeeez.

Bogoshipseyo Chingu.
baadhi ya nyakati napenda kuwa msomaji zaidi ndio maana hujipumzisha kwa wiki au zaidi
baadhi ya nyakati hupenda kujiweka mbali na JF kama nilivyofanya siku tano zilizopita (kuanzia jumanne hadi jumapili).
sometimes najikuta nakutana na mjadala unaonifanya nitamani kuchangia hususan kwenye thread nilizokwisha zizoea ndipo hapo balaa la kuwa addicted na JF linapojitokeza.

siwezi kukaa muda mrefu sana bila ya kumjibu mtu na huo ndio udhaifu wangu
 
baadhi ya nyakati napenda kuwa msomaji zaidi ndio maana hujipumzisha kwa wiki au zaidi
baadhi ya nyakati hupenda kujiweka mbali na JF kama nilivyofanya siku tano zilizopita (kuanzia jumanne hadi jumapili).
sometimes najikuta nakutana na mjadala unaonifanya nitamani kuchangia hususan kwenye thread nilizokwisha zizoea ndipo hapo balaa la kuwa addicted na JF linapojitokeza.
Bogoshipseyo Chingu.
 
Drama bora kabisa kati ya nilizowahi kuzishuhudia.. Huyu jamaa Lee Byeong Hun ambaye ni mtayarishaji wa Tamthilia hii pia Amewahi kufanya Kazi nyingine nzuri ya kuitwa
wewe muhuni kutoka pyongyang unapaswa uwe na heshima mbele ya wazee wako wa kambo.
huyo babu director lee byung heon amezaliwa miaka 74 iliopita.
ameanza kufanya kazi tokea mwanzoni mwa miaka ya 70 na project zake takribani zote amefanya ndani ya shirika la MBC.
kuna project moja ameisimamia inaitwa 500 Years of Joseon (kuanzia mwaka 1983 hadi 1990) inajaribu kuzungumzia mtiririko wa matukio yaliotokezea ndani ya joseon kwa takribani miaka 500 ya kuanzishwa kwake.

kusimamia project kwaa miaka 8 si jambo la masihara hata kidogo.
1570547819915.png
 
Mungu ametupa uwezo wa kuweza kutambua hisia tulizonazo na hata zile hisia za wenzetu wanazokumbana nazo kila siku, kadiri ninapoiangalia when the camellia blooms mawazo mengi hunijia kichwani mwangu (mawazo hasi na chanya).

hisia za kimapenzi zimebeba maajabu makubwa sana, unaweza kuwa na uhusiano wa muda mrefu na mwenza wako lakini akashindwa kukupa furaha ndani ya nafsi yako na ukamuona si chochote kwako, ajabu zaidi kwa muda mchache unaweza kujikuta unaanza kuvutiwa na mr/ mrs x ambaye ameanza kukufanya uwe na amani ya nafsi ulioikosa kwa bwana / bibi yule kwa muda mfupi muliofahamiana.

sitoshangaa tena kuwaona wadau humu ndani wanaanzisha mahusiano ya kimapenzi japokuwa wanafahamiana kwa njia ya keyboard, hisia za mapenzi ni zaidi ya biashara ya kujichua inayopumbaza na kulemaza (nimekusudia kujichua mgongo jamani)

daemusin na gong hyo jin ni marafiki kuanzia leo, utakapomuona daemusin ndio umemuona gong hyo jin.
wanaojipendekeza kwa daemusin / gong hyo jin wakome na wachakae.
nataka niachane na imani ya buddha kumbe mapenzi yana raha na utamu kuliko pilau la krismasiaaa nililoalikwa na Khantwe ahjummaaaa.

kang ha neul humu ndani amebeba uhusika wa ajabu sana, jamaa ni mwehu mnooooo.

sielewi ni sababu ipi inayowafanya wazazi waliotelekezwa kimahusiano wawe ni wagumu sana kuzipokea hisia mpya za
kimapenzi kutoka kwa wengineo iwe ni mwanamke au mwanamme, nafahamu kuna uoga fulani huja pindi unapopitia ugumu kutelekezwa kihisia na mwenza wako wa mwanzo lakini binadamu hatufanani bwanaaaaa.
hivyo basi si sahihi hata kidogo kutuangushia nyumba ya lawama wengineo tusiohusika na breakup zenu pindi tunapoamua kuwatokea kwa lengo jema la kuanzisha mahusiano.

jamani bongo movies mpaka stori nyepesi kama hii munashindwa kutengeneza, location za uswahilini, mavazi ya ushwahilini, maisha ya uswahilini, mpaka vyakula vya uswahilini.
mdogo mdogo tumeshagonga 10% kwa kuangaliwa kila siku ya jumatano na alhamisi.

single mother oyeee = when the camellia blooms drama.
single father oyeee = one night spring drama.
1570549294014.png
 
Lee Byung Hun, Han Ji Min, Nam Joo Hyuk, Shin Min Ah, And More Confirmed For New Drama
On October 8, Lee Byung Hun, Han Ji Min, Shin Min Ah, Bae Sung Woo, and Nam Joo Hyuk were confirmed for “HERE” (working title).

It is reported to tell the story of an international NGO (non-governmental organization), but additional details have not yet been revealed publicly. However, viewers are already anticipating the collaboration of top actors and Noh Hee Kyung, who is known for hit dramas such as “Live,” “It’s Okay, That’s Love,” and “That Winter, The Wind Blows.”

“HERE” is scheduled to begin filming in 2020..
=========================================================
nimebaki najiuliza hii ni drama au variety show?
nimezoea kuona variety show ndio zinawakutanisha celebrities maarufu kwa wakati mmoja na sio drama.

han ji min = si muigizaji mwepesi hivyo basi kivyovyote dau lake ni kubwa
shin min ah = dau lake pia ni kubwa.
nam joo hyuk = bwana mdogo pia anafanya vizuri kivyovyote dau lake ni kubwa kiupande fulani.

lee byung hun ndio usisemee, mwaka 2009 kupitia IRIS DRAMA season 1 inasemekana alilipwa bonus ya dolla millioni 1 na producer kutoka japan, miaka 9 baadae kupitia MR SUNSHINE DRAMA inasemekana alilipwa takribani $3.2 million kwa episode 24 alizoshiriki.

bila ya kusahau kuna gharama nyengine za uzalishaji.
1570559426617.png
 
wewe muhuni kutoka pyongyang unapaswa uwe na heshima mbele ya wazee wako wa kambo.
huyo babu director lee byung heon amezaliwa miaka 74 iliopita.
ameanza kufanya kazi tokea mwanzoni mwa miaka ya 70 na project zake takribani zote amefanya ndani ya shirika la MBC.
kuna project moja ameisimamia inaitwa 500 Years of Joseon (kuanzia mwaka 1983 hadi 1990) inajaribu kuzungumzia mtiririko wa matukio yaliotokezea ndani ya joseon kwa takribani miaka 500 ya kuanzishwa kwake.

kusimamia project kwaa miaka 8 si jambo la masihara hata kidogo.
View attachment 1226844
Pumbavu zake Huyu muhuni.
Anatuzo ngapi?!, na Hiyo Project ya miaka 500 ya Joseon ina episode ngapi?!
 
BTW acha tabia yako yakufuta quotes zako kwangu dogo, nilikaa kimya zile nyingine ila ile ya juzi kwenye mabeki visiki nimesema hapana! Lazima nikuambie kama hivi
emoji4.png
teh teh teh
tokea urudi kwa mara nyengine JF baada ya likizo ndefu umekuwa tofauti na ulivyokuwa mwanzoni na sababu za kuwa hivyo naomba ziendelee kubaki kwenye kiwiliwili chako (kiukweli hazinihusu), bahati nzuri hayo mabadiliko si peke yangu ninayoyashuhudia bali hata wadau wengine kupitia majukwaa tofauti wameuona utofauti wako (ule mzuka wa kuchangia umekuwa ni mdogo sana kiupande wako).

ndio maana hata kiupande wangu imenibidi nibadilishe mdundo wa muziki kama ulivyobadili wewe ili niendane na kasi yako na sifanyi hivyo kwa nia mbaya inayoongozwa na wivu, chuki zinazoambatana na hasira za kijinga.

ndio maana nimekuwa mzito wa kunukuu comment zako, kumention jina lako na hata niki replay sichukui muda nazifuta.

mawazo ya kijinga hunitawala kwa kiasi kikubwa sana (labda hii comment hata nikinukuu itakuwa namzingua huyu mwandamu hivyo basi bora niifute kabla hajaiona, nikimention jina lake pia itakuwa namzingua n.k)

dah! sikujua kama hali hiyo huwa haikufahishi ndio maana nimekuwa nikiendeleza hiyo tabia mbaya kwa zaidi ya mara moja.


samahani sana kwa hayo matendo yote ya kijinga jinga nilioyatenda huko nyuma, nafahamu wanadamu inatuwia vigumu sana kusamehe yaliopita kwa sababu ya maumivu kama alivyofanya prezidaaa japo kwa njia ya maigizo, pia naamini kuomba kwangu msamaha itakuwa ni sababu tosha ya kuitanua barabara yetu ya mahusiano kuanzia sasa, hakuna umuhimu wa kuifuta home page ya tovuti kwa sababu ya errors zinazotokana na server haliyakuwa button ya refresh ipo hapo juu.

Niruhusu niurefresh urafiki wetu unaoendelea kudumu kwa mwaka wa nne huu tokea nijiunge na JF haijalishi ni urafiki unaoongozwa zaidi kwa njia ya keyboard
 
49 Reactions
Reply
Back
Top Bottom