Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kazz0

Kazz0

Member
Joined
Mar 15, 2015
Messages
48
Points
95
Kazz0

Kazz0

Member
Joined Mar 15, 2015
48 95
Kama wewe ni mpenzi wa Korean Dramas, karibu katika thread hii tupate ku share kuhusu kazi hizo hatari za mkorea.

Tuambiane;

- Ipi ni drama yako bora ya kila wakati kwako?

- Ni ya aina gani? (Wengi tumezoea kusema za 'mjini' na 'vijijini')

-Nini kinakuvutia sana katika hiyo Drama?

Pia:

- Nani ni Msanii wako Bora wa kiume na wa kike na baadhi ya drama alizoigiza?

- Nani ni sexiest Actor au Actress kwa maoni yako?

- Ipi ilikua Drama yako ya kwanza ya kikorea kuiona?

- Ni Drama gani ya kikorea unaitafuta sana na unapata wakati mgumu kuipata? (Unaweza ukasaidiwa kuipata na mashabiki wengine)

*Pia tumia thread hii kufahamishana kuhusu drama mpya zilizotoka au unayohisi ni nzuri ila haijapata umaarufu sana!!

Karibu tujumuike! Saraghae! Kumooyo!!

=========

Baadhi ya Links za Dramas mbali mbali za Korea...;

Be Strong Geum Soon

Princess Ja Myung Go

THREE DAYS (2014)

Swallow the Sun

Jumong

King Guenchoggo

=====

Links za ku-download drama za Kikorea;

- Watch Drama Online | Korean Drama | Japanese Drama | Taiwanese Drama | Hong Kong Drama | Chinese Drama
- GoodDrama.Net

======

Updated: Kwa mjadala na kubadilishana uzoefu kuhusu series za jumla za movies mbalimbali, za zamani na mpya, Unaweza pia kufuatilia UZI HUU hapa Series (Special thread)
..

Kazi kwako.. Enjoy!
 
Great Conqueror

Great Conqueror

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2018
Messages
374
Points
1,000
Great Conqueror

Great Conqueror

JF-Expert Member
Joined Apr 14, 2018
374 1,000
mkuu vipi maisha ya uhubiri wa dini ya mtakatifu kristo yameshakushinda sasa unataka kuwa mwanasiasa mwenye jicho la kuona mbali kama alivyokuwa mtaalamu ryu seong ryeong?
'samahani kama itakuwa nimekukwaza brother'​
 1. ndani ya drama hii anazungumziwa kwa kiasi kikubwa sana genius wa siasa anayeitwa ryu seong ryeong na harakati zake za kuifanya joseon inakuwa na amani pamoja na kujiandaa kijeshi dhidi ya uvamizi wowote utakaotokezea lakini bahati mbaya baadhi ya mawaziri na mfalme seonjo walimpuuza.
 2. jingbirok maana yake ni kitabu cha kujisahihisha na kimeandikwa na msomi ryu seung ryong ambaye pia alikuwa ni mtu wa karibu sana na admiral yi soon shin ambaye kwenye vita ya imjin ndio alikuwa muhusika mkuu wa masuala ya kijeshi na pia aliwahi kuwa waziri mkuu. Aliandika kitabu hiki baada ya kuachana na harakati za siasa chini ya utawala wa mfalme seonjo. kitabu hiki kimekuwa ni moja kati ya chanzo muhimu kinachotumika kuelezea uhusiano wa mgogoro kati ya china, korea na japan.
 3. mwaka 1969 serikali ya korea ilikichaguwa kitabu hiki kama ni miongoni mwa hazina 132 bora za utawala wa korea (National Treasures of South Korea)
 4. Ryu Seong-ryong aliandika Jingbirok ili kuwa kama ni ukumbusho wa kuzuia uvamizi wa vita kama ya imjin (1592-1598) usitokee tena, kutafakari juu ya makosa walioyafanya ya kupuuzia taarifa za japan kujianda na uvamizi,jambo ambalo lilipelekea joseon kupoteza miji yake mitatu na kusababisha vifo vya maelfu ya wananchi wasio na hatia na wengineo kutumikishwa utumwani nchini japan na hata china.
 5. hadithi ya drama hii inaanza kabla ya vita ya imjin na vita ya noryang ambayo ilipelekea kifo cha admiral yi soon shin. kama si juhudi kubwa za kidiplomasia na za kivita alizozichukua ryu seong ryeong basi tungelishuhudia joseon ikitawaliwa na japan na ming china, na pengine kwa wakati huu taifa la korea lisingelikuwepo.
 6. wakati vita ilipozodi mfalme seonjo aliamua kuikimbia nchi yake kwa kupitia mto yalu na kujificha nchini china (ming), cha kushangaza wafuasi wake wengi walikubaliana na maamuzi ya mfalme lakini ryu seung ryong alimshauri mfalme seonjo asifanye hivyo kwani kitendo hicho kingeliwafanya japan na ming (china) kuigawa joseon, licha ya kuwa ming walikuwa wakiisaidia joseon kwenye vita hiyo lakini kwenye mali hakuna udugu wala urafiki wa kudumu.
 7. ryu seung ryeong binafsi ndio alikuwa akiwaongoza yi soon shin na general kwon yun kwenye vita ya ardhini dhidi ya wajapan. ukiangalia admiral yi soon shin kuanzia episode ya 4 watatu hawa wanakuwa marafiki sana tokea udogoni mwao.
 8. baada ya vita kumaliza wapinzani wake wa kisiasa walimshinda kwenye vita chafu ya kiutawala na ndipo akavuliwa nyadhifa zote na kuamua kuondoka kwenye mji mkuu wa hanyang na kuelekea Hahoe Village, North Kyungsang Province, kwenye mji mkuu hakurudi tena ndipo akaandika kitabu hiki cha jingbirok.
 9. jina lake la utotoni aliitwa Igyeon, shuleni alikuwa akiitwa Seoae, kwenye drama ya admiral yi soon shin kwon yun alikuwa anapenda kumuita yi seong ryeong jina la bookworm kwa sababu alikuwa anapenda kusoma vitabu.
 10. nilichompendea huyu great thinker ni kwamba licha ya kutokea upande wa "Eastern faction" lakini lilipokuja suala lenye maslahi na nchi hakuona tabu kuachana na siasa za kimatabaka na kuungana na "western faction" kwa lengo la kuipigania nchi yake tofauti na wanasiasa wengineo.
  wanasiasa wa sasa wanaposema mapambano ya kupigania maendeleo na maslahi ya nchi dhidi ya wanyonyaji hayana chama wala ukabila basi waonyeshe matendo yao ya ukweli kama alivyofanya ryu seong ryeon mnamo karne ya 16 na si kutishiana bunduki za kuwindia nyumbu.
==================================================================
ngoja nifukue tena kaburi la watu bila ya idhini ya mwenyewe natumai atanisamehe kwa tendo hili ovu nililolifanya na pia atanisamehe kwa kumwita uchawini :D:D:D
nanukuu maneno ya mwanadada Nifah aliyoandika humu ndani japo kwa ufupi baada ya kumaliza kuiangalia hii drama;
Nilichojifunza
Niseme ukweli sijawahi kuangalia drama yoyote ya kikorea yenye absolutely 0 romance kama hii! Huku ni serious politics mwanzo mwisho!
Na ajabu nimeipenda mnoooo!
Nimevutiwa, nimehamasika niwe mzalendo kwa nchi yangu ila kuna tofauti kubwa kati ya nchi yangu na Joseon ile ya takribani miaka 500 iliyopita!
Demokrasia, uhuru wa kutoa maoni ni vitu vilivyonivutia zaidi.
Sasa najiuliza kama wenzetu walikuwa mbali hivyo kidemokrasia karne hizo kibao zilizopita vipi sasa hali ikoje? Ndio maana wameweza hata kumtoa madarakani na kumfunga Rais wao! Haki I love Korea.
Walionivutia
Ryu

Huyu ndiye muandishi mwenyewe wa Jing Birock hivyo ameweza kutendea haki na nimehasika sana na ujasiri wake wa kumkosoa mfalme bila kujali mfalme atachukua hatua gani dhidi yake!
Mfalme alikuwa mdogo mbele ya Ryu kiasi muda mwingi analia tu maana nyakati zote Ryu aliibuka mshindi wa mijadala na matokeo baada ya mijadala.
Admiral Yi Soon Sin
Huyu mtu sijui nimuelezee vipi! Ndiye character aliyenivutia kuliko wote. Nimependa weledi wake wa vita na msimamo wake ktk kile alichokiamini hata kama ingepelekea tishio la uhai wake kwa kukiuka maagizo ya kipuuzi ya mfalme Seonjo.
Huyu mtu amenifanya mpaka nikajiuliza hivi ktk nchi yetu ile ya kisiwa cha Madagascar kweli tuna mtu kama Yi Soon Shin?
King Seonjo
Huyu mfalme amenifanya nitamani kuingia ktk drama mara nyingi nimtandike vibao! Ni mfalme mpuuzi na muoga ambaye sijawahi kuona drama yenye mfalme dhaifu kama yeye.
Nimeshangaa tuzo aliyopewa na MBC mwaka 2015 ya Best Actor... Au ni vile kaweza kuigiza kama mfalme goigoi? Lol
Toyotomi Hideyoshi
Baba yake na Tsurumatsu hahaaaaa.
Majina ya Kijapani yamenichekesha sana. Kiasi watu nyumbani kwangu wamepata taabu kila mmoja na jina lake. Lol
Huyu jamaa kajua kuuvaa uhusika vilivyo! Mwanzoni alikuwa ananiogopesha hata mimi ila baadae nikamzoea na hakika kajua kunivunja mbavu hasa anavyowaita wasaidizi wake akina Maeda, Ishida n.k
Konishi Yukinaga & Kato Kiyomosa
Unawezaje kuacha kufurahia ‘ligi’ ya majemedari hawa wawili wa vita? Mmoja akiwa msomi na mtoto wa familia ya wafanyabiashara mashuhuri (Konishi) huku mwenzie Kato asiye na elimu,jasiri,na mtiifu kwa kiongozi wake.
Mara zote Konishi aliibuka mshindi wa ligi zao kwakuwa alikuwa na matumizi makubwa ya akili kuliko mwenzie Kato aliyeamini ktk matumizi ya nguvu.
Mabishano yao ni moja kati ya burudani kubwa nilizozipata ktk drama hii.
Nilikuwa nacheka kama mwehu.
Great Conqueror dongsaeng, emperor wang guhn imeshakuchosha?
Umesahau kuwa nilizaliwa pale Nilizaliwa Pale Yodongseong na nikakulia Gwamingseong na Pyeongyangseong. Utagundua kuwa vita zipo damuni, kifupi naendelea na Wang Guhn, nataka nifuatiliea General Park Sulhae atamuoa dada yake Kyeo non?!, and what will happen baada ya kifo cha Binti wa Yanggil,.

Nilitaka kula ugali na mboga maana ugali mkavu unakaba shingo.
 
Daemusin

Daemusin

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Messages
5,849
Points
2,000
Daemusin

Daemusin

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2015
5,849 2,000
Umesahau kuwa nilizaliwa pale Nilizaliwa Pale Yodongseong na nikakulia Gwamingseong na Pyeongyangseong. Utagundua kuwa vita zipo damuni, kifupi naendelea na Wang Guhn, nataka nifuatiliea General Park Sulhae atamuoa dada yake Kyeo non?!, and what will happen baada ya kifo cha Binti wa Yanggil,.

Nilitaka kula ugali na mboga maana ugali mkavu unakaba shingo.
nikupe pole sana kwa kusubiria ndoa ya general park dhidi ya dada yake kyu hyun.
teh teh teh bora nisikuhadithie kinachotokezea mbeleni.

merciful buddha
wanawake wenye msimamo kama jiwe la msingi la klabu ya simba oyeeeeeeee
 
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Messages
20,374
Points
2,000
Da'Vinci

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2016
20,374 2,000
mkuu vipi maisha ya uhubiri wa dini ya mtakatifu kristo yameshakushinda sasa unataka kuwa mwanasiasa mwenye jicho la kuona mbali kama alivyokuwa mtaalamu ryu seong ryeong?
'samahani kama itakuwa nimekukwaza brother'​

 1. ndani ya drama hii anazungumziwa kwa kiasi kikubwa sana genius wa siasa anayeitwa ryu seong ryeong na harakati zake za kuifanya joseon inakuwa na amani pamoja na kujiandaa kijeshi dhidi ya uvamizi wowote utakaotokezea lakini bahati mbaya baadhi ya mawaziri na mfalme seonjo walimpuuza.
 2. jingbirok maana yake ni kitabu cha kujisahihisha na kimeandikwa na msomi ryu seung ryong ambaye pia alikuwa ni mtu wa karibu sana na admiral yi soon shin ambaye kwenye vita ya imjin ndio alikuwa muhusika mkuu wa masuala ya kijeshi na pia aliwahi kuwa waziri mkuu. Aliandika kitabu hiki baada ya kuachana na harakati za siasa chini ya utawala wa mfalme seonjo. kitabu hiki kimekuwa ni moja kati ya chanzo muhimu kinachotumika kuelezea uhusiano wa mgogoro kati ya china, korea na japan.
 3. mwaka 1969 serikali ya korea ilikichaguwa kitabu hiki kama ni miongoni mwa hazina 132 bora za utawala wa korea (National Treasures of South Korea)
 4. Ryu Seong-ryong aliandika Jingbirok ili kuwa kama ni ukumbusho wa kuzuia uvamizi wa vita kama ya imjin (1592-1598) usitokee tena, kutafakari juu ya makosa walioyafanya ya kupuuzia taarifa za japan kujianda na uvamizi,jambo ambalo lilipelekea joseon kupoteza miji yake mitatu na kusababisha vifo vya maelfu ya wananchi wasio na hatia na wengineo kutumikishwa utumwani nchini japan na hata china.
==================================================================ngoja nifukue tena kaburi la watu bila ya idhini ya mwenyewe natumai atanisamehe kwa tendo hili ovu nililolifanya na pia atanisamehe kwa kumwita uchawini :D:D:D
nanukuu maneno ya mwanadada Nifah aliyoandika humu ndani japo kwa ufupi baada ya kumaliza kuiangalia hii drama;

Nilichojifunza
Niseme ukweli sijawahi kuangalia drama yoyote ya kikorea yenye absolutely 0 romance kama hii! Huku ni serious politics mwanzo mwisho!
Na ajabu nimeipenda mnoooo!

Nimevutiwa, nimehamasika niwe mzalendo kwa nchi yangu ila kuna tofauti kubwa kati ya nchi yangu na Joseon ile ya takribani miaka 500 iliyopita!
Demokrasia, uhuru wa kutoa maoni ni vitu vilivyonivutia zaidi.

Sasa najiuliza kama wenzetu walikuwa mbali hivyo kidemokrasia karne hizo kibao zilizopita vipi sasa hali ikoje? Ndio maana wameweza hata kumtoa madarakani na kumfunga Rais wao! Haki I love Korea.

Walionivutia
Ryu

Huyu ndiye muandishi mwenyewe wa Jing Birock hivyo ameweza kutendea haki na nimehasika sana na ujasiri wake wa kumkosoa mfalme bila kujali mfalme atachukua hatua gani dhidi yake!

Mfalme alikuwa mdogo mbele ya Ryu kiasi muda mwingi analia tu maana nyakati zote Ryu aliibuka mshindi wa mijadala na matokeo baada ya mijadala.

Admiral Yi Soon Sin
Huyu mtu sijui nimuelezee vipi! Ndiye character aliyenivutia kuliko wote. Nimependa weledi wake wa vita na msimamo wake ktk kile alichokiamini hata kama ingepelekea tishio la uhai wake kwa kukiuka maagizo ya kipuuzi ya mfalme Seonjo.

Huyu mtu amenifanya mpaka nikajiuliza hivi ktk nchi yetu ile ya kisiwa cha Madagascar kweli tuna mtu kama Yi Soon Shin?

King Seonjo
Huyu mfalme amenifanya nitamani kuingia ktk drama mara nyingi nimtandike vibao! Ni mfalme mpuuzi na muoga ambaye sijawahi kuona drama yenye mfalme dhaifu kama yeye.
Nimeshangaa tuzo aliyopewa na MBC mwaka 2015 ya Best Actor... Au ni vile kaweza kuigiza kama mfalme goigoi? Lol

Toyotomi Hideyoshi
Baba yake na Tsurumatsu hahaaaaa.
Majina ya Kijapani yamenichekesha sana. Kiasi watu nyumbani kwangu wamepata taabu kila mmoja na jina lake. Lol

Huyu jamaa kajua kuuvaa uhusika vilivyo! Mwanzoni alikuwa ananiogopesha hata mimi ila baadae nikamzoea na hakika kajua kunivunja mbavu hasa anavyowaita wasaidizi wake akina Maeda, Ishida n.k

Konishi Yukinaga & Kato Kiyomosa
Unawezaje kuacha kufurahia ‘ligi’ ya majemedari hawa wawili wa vita? Mmoja akiwa msomi na mtoto wa familia ya wafanyabiashara mashuhuri (Konishi) huku mwenzie Kato asiye na elimu,jasiri,na mtiifu kwa kiongozi wake.

Mara zote Konishi aliibuka mshindi wa ligi zao kwakuwa alikuwa na matumizi makubwa ya akili kuliko mwenzie Kato aliyeamini ktk matumizi ya nguvu.

Mabishano yao ni moja kati ya burudani kubwa nilizozipata ktk drama hii.
Nilikuwa nacheka kama mwehu.Great Conqueror dongsaeng, emperor wang guhn imeshakuchosha?
Fanya uwe unatuchambulia na muvi zetu zile.. Sio kwa uchambuzi huu murua kabisa!
Ungekua unachambua za Hollywood ningeinjoi sana. U good
 
Great Conqueror

Great Conqueror

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2018
Messages
374
Points
1,000
Great Conqueror

Great Conqueror

JF-Expert Member
Joined Apr 14, 2018
374 1,000
Yule
nikupe pole sana kwa kusubiria ndoa ya general park dhidi ya dada yake kyu hyun.
teh teh teh bora nisikuhadithie kinachotokezea mbeleni.

merciful buddha
wanawake wenye msimamo kama jiwe la msingi la klabu ya simba oyeeeeeeee
Lo! Inamaana Binti aligoma?!!!!
 
Demiss

Demiss

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2017
Messages
32,465
Points
2,000
Demiss

Demiss

JF-Expert Member
Joined May 4, 2017
32,465 2,000
Kumbe muendelezo mpaka mwakan looh
kingdom wameishia season 1 na ilicontained episode 6.
season 2 mpaka mwakani inshallah ndio itaonyeshwa tena kupitia netflix

mwanzoni nilikuwa mshabiki mkubwa sana wa kazi za mwanamama kim eun seok lakini tokea nimfahamu shoga yake anayeitwa kim eun hee nimejikuta nahamishia majeshi yangu yote upande wake.

wote ni waandishi wazuri wa script ila ninachompendea kim eun hee ni uwezo wake wa kuandika hadithi zinazobeba mandhari tofauti ya matukio anayotaka kutufikishia wana hadhira kuanizia signal, ghost, sign drama pamoja na 3 days drama.

alichokifanya mwanamama kim eun hee ni kuigeuza webtoon inayoitwa Land of the Gods ambayo ameiandika mwenyewe kuwa drama.
View attachment 1180788
 
koncho77

koncho77

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Messages
5,467
Points
2,000
koncho77

koncho77

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2014
5,467 2,000
Hahaha! Huyo Togon unavyomuona "boya" kiasi hicho ni sababu tu ana maadui kila kona na hana mtu wa kumwamini na kila anayeonekana yuko karibu yake kwa namna moja au nyingine ni mnafiki wa kutupwa.

Ukifuatilia hata watu walioko karibu yake sana hususan hata Queen Dowager naye anamtumia tu kwa maslahi yake licha ya kuwa ni mama yake mzazi. Vita kali sana ya madaraka hiyo!

Kwahiyo katika hali kama hiyo inamlazimu kuwa mpole mpaka pale atakapopata mahala pa kusimamia na kujenga ushawishi wa kutosha ili kuweza kuzivunja-vunja ng'ome za maadui zake wa kisiasa.

Isitoshe hiyo hali yake ya "uzembe" unayoiona ndiyo kwa namna moja ama nyingine iliwafanya hata wale maadui zake wakuu wampuuze bila kujua kuwa jamaa naye ana "mishe" zake za siri na anajipanga kimyakimya ili kulipa kisasi kwa wabaya wake.
Sungnyang na Mfalme wa Koryo wanisamehe sana kwa kweli maana walikuwa majembe lakini huyu Togon yaani hapandi kichwani mwangu kwa kweli
 
FRANC THE GREAT

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Messages
1,792
Points
2,000
FRANC THE GREAT

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined May 27, 2016
1,792 2,000
Dah...shukran mkuu but hii sio yenyewe...nataka ile ya kifalme...
Aisee! Sawa ndugu lakini itakuwa vyema sana ukarejea na kuyaelezea angalau kidogo maudhui ya hiyo ya kifalme ili wadau kwa ujumla wapate mwanga wa kukusaidia maana pengine inafahamika humu lakini kwa jina tofauti kidogo. Ahsante!
 
FRANC THE GREAT

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Messages
1,792
Points
2,000
FRANC THE GREAT

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined May 27, 2016
1,792 2,000
Wakati tukiendelea na *Ongoing* si mbaya pia tukijikumbusha Projects zilizopita nyuma. Watu wa 'Mitandao' wanasemaga 'Throwback Thursday' lakini hii ni katika Korean Drama.

Ni wangapi waliopata kuishuhudia Project moja hivi ya takribani miaka mitano iliyopita, inayokwenda kwa jina la Doctor Stranger?

Kama umepata kuitazama basi 'Hongera Sana' na kama bado wala hujachelewa kwa maana ipo na inapatikana kwa njia mbalimbali ikiwemo mitandao na wavuti mbalimbali za K-Drama Ulimwenguni.

Ni Drama yenye maudhui ya kisasa, wengine mnapenda kusema "ya kimjini mjini" au naweza kusema kuwa si ya kijijini bali ni ya mjini iliyokuwa ikirushwa hewani na kituo kikubwa sana cha Televisheni cha SBS cha nchini Korea Kusini mnamo May 5 hadi July 8 mwaka 2014.

Drama hii inahusu au inamhusu kijana mmoja ajulikanaye kwa jina la Park Hoon. Kijana huyu anaishi na baba yake mzazi aitwaye Park Cheol. Park Hoon na babaye wote ni raia wazalendo kabisa na watiifu wa sheria bila shuruti wa taifa la Korea Kusini.

Nitaelezea kisa cha mwanzoni kabisa cha Drama hii kinachohusu maisha ya utotoni ya kijana huyu Park Hoon pamoja na baba yake:

Baba yake Park Hoon ni daktari bingwa hususani katika masuala ya upasuaji (Thoracic Surgeon) taaluma ambayo ilimvutia pia kijana huyo mdogo kuisomea na kujifunza pia kupitia baba yake. Tukirejea utotoni kipindi Park Hoon akiwa mdogo mnamo mwaka 1994, walipelekwa nchi jirani ya Korea Kaskazini kipindi ambacho kulikuwa na hatari kubwa sana ya kutokea kwa vita baina ya nchi hizo mbili.

Kabla sijaendelea, huenda utakuwa ukijiuliza kuwa huyu ndugu yetu Park Hoon hakuwa na mama?

Hapana! Alikuwa naye lakini wazazi wa kijana huyu Park Hoon waliachana ama walitengana kisha mtoto yaani Park Hoon kubaki upande wa baba yake.

Ni kitu gani basi kingesababisha vita hiyo kati ya Korea Kusini na Korea Kaskazini?

Ni kuwa, Serikali ya Korea Kusini ilipenyezewa taarifa ya siri kuwa Marekani ilikuwa na mpango wa kushambulia vinu vya nyuklia vya Korea Kaskazini na iwapo Marekani itafanya hivyo basi akina 'Kiduku' lazima nao watalipa kisasi kwa kupitia Korea Kusini ambaye ni mmoja wa washirika wakuu wa Marekani.

Ilikuwa ni "patashika nguo kuchanika" maana vifaru vya kijeshi vya Korea Kusini vilikuwa vikipita barabarani na Jeshi la Korea Kusini lilikuwa tayari kabisa kuikabili Korea Kaskazini lakini kwa upande wa wanasiasa hasa viongozi wa juu wa Korea Kusini hawakuwa tayari kwa vita hiyo na jirani yao Korea Kaskazini maana kwa mtazamo wao kama vita ingetokea basi ingeleta madhara makubwa sana ambayo ingechukua muda mrefu sana kuyarekebisha madhara hayo.

Bahati nzuri na nikutoe hofu ni kwamba vita haikutokea na amani ilirejea lakini ilibaki kidogo tu ama kwa kifupi naweza kusema "Almanusura Wazichape". Hali ya utulivu na amani haikurejea tu ghafla bali kuna mtu alifanya kazi kubwa sana ya kuuzima mzozo huo, naye si mwingine bali ni Bw. Park Cheol, baba yake mtoto Park Hoon.

Ni kitu gani alichokifanya huyu ndugu yetu Park Cheol kilichosababisha vita isitokee?

Ni kwamba katika utawala wa Korea Kaskazini kulikuwa na mgonjwa wa moyo ambaye alikuwa akikaribia kufa. Si mwingine bali ni kiongozi wa kwanza wa taifa hilo la Korea Kaskazini ambaye bado alikuwa madarakani, Kim Il-sung (Babu yake Kim Jong-un wa sasa).

Sasa, Wamarekani walikuwa wakivizia kifo cha huyo 'Bwana Mkubwa' wa Korea Kaskazini ili waitumie fursa hiyo kuipatia 'kichapo' nchi hiyo na kuharibu miundombinu yao ya nyuklia, ambapo nayo Kaskazini kivyovyote ingelipa kisasi kwa shambulio dhidi ya Korea Kusini. Na kama vita vingeibuka, viwango vya mionzi vilivyosababishwa na shambulio la nyuklia pekee vingefanya theluthi moja ya taifa hilo ya Korea Kusini isikalike kwa miaka 200 ijayo. Hatari sana!

Kutokana na kujulikana kwa Dk. Park Cheol (Baba yake Park Hoon) nchini Korea Kusini kutokana na taaluma yake na uwezo wake wa hali ya juu ilibidi ufanyike mpango wa haraka sana wa kumpeleka daktari bingwa huyo kulekule Kaskazini ili akamtibie jamaa mpaka apone la sivyo akifa tu, 'balaa' litakalotokea baada ya hapo watakao baki hai watasimulia wajukuu zao.

Mpango huo wa kumpeleka Bw. Park Cheol huko Korea Kaskazini unasimamiwa vilivyo na Waziri aliyefahamika kama Jang Suk-joo ambaye alikuwa na ukaribu sana na Daktari wetu Dr. Park Cheol.

Baada ya Dr. Park Cheol kupelekwa huko Korea Kaskazini kibao kiligeuzwa na aliwekwa kizuizini pamoja na mwanaye Park Hoon mpaka pale atakapofanikiwa kumfanyia upasuaji wa matibabu ya moyo Mkuu wa taifa hilo la Korea Kaskazini ambaye tayari nilikwisha kukutajia jina lake hapo awali (Babu yake Kiduku).

Uwezo wa Dr. Park Cheol na moyo wake wa ushujaa uliwezesha kufanyika kwa upasuaji huo wa moyo na kufanikiwa kumrejeshea uhai mgonjwa aliyekaribia kufa.

Wakati utakapokuwa ukitizama hicho kipande (Scene) katika hiyo Drama hukohuko uliko lazima utapata hisia fulani hivi ya shangwe kutokana na mafanikio ya Dr. Park Cheol katika chumba cha upasuaji huku akiwa amezungukwa na walinzi na huku bastola ikiwekwa kichwani pa mwanaye Park Hoon ambayo ingeusambaratisha ubongo wa mwanaye huyo endapo baba, Dr. Park Cheol angeshindwa kumtibu 'Bwana Mkubwa' wa taifa hilo.

Ushindi huo wa Dr. Park Cheol katika chumba cha upasuaji ndiyo uliwezesha kumponya mwanaye na yeye pia bila kusahau taifa lake la Korea Kusini dhidi ya vita sababu kutokana na hilo, Marekani ilighairisha mpango wake wa mashambulizi baada ya 'Bwana Mkubwa' wa Korea Kaskazini kuokolewa kutoka katika kifo baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo na Dr. Park Cheol.

Nyumbani Korea Kusini ilikuwa ni shangwe na furaha iliyoje baada ya kufanikiwa kuzuia vita iliyokuwa ikikaribia kutokea na kila mwananchi wa Korea Kusini alisherehekea kwa namna yake. Jambo la kushangaza zaidi ni kuwa, mafanikio ya Dr. Park Cheol yalimpa sifa sana yule Waziri Jang aliyempeleka Dr. Park Cheol kule Kaskazini. Ni jambo la kushangaza kwelikweli maana wananchi walimsifu zaidi Waziri Jang bila kujua kuna 'mwamba' mmoja yupo Kaskazini huko akifanya yake ili taifa lipone.

Mfano hata wewe msomaji wa bandiko hili, siku ufanye jambo kubwa sana na la maana katika jamii linalohitaji ujasiri na ushujaa wa hali ya juu alafu sifa ziende kwa mwingine kabisa, sijui utajisikiaje!

Kilichotokea baada ya jamaa, huyo Waziri kulewa 'sifa' matatizo mengine nchini Korea Kaskazini yakaibuka ambapo Dr. Park Cheol pamoja na mwanaye walikataliwa kurudi kwao Korea Kusini ikiwa ni njama za ndugu Waziri kuyaiba mafanikio ya Dr. Park Cheol na kujinufaisha kisiasa ili aweze kuyatumia mafanikio hayo kama karata muhimu ya Uchaguzi wa Urais uliokuwa ukikaribia nchini Korea Kusini.

Dr. Park Cheol na mwanaye walinyang'anywa haki ya kurudi nchini kwao na kulazimishwa kusalia katika nchi ya ugeni baada ya visa vingi sana na vya hatari kutokea.

Wakiendelea na maisha mapya kabisa nchini Korea Kaskazini mtoto mdogo kabisa Park Hoon anakutana na msichana mdogo pia aitwae Song Jae-hee na kuzoeana ghafla licha ya kukutana kwa siku ya kwanza kabisa.

Hapo nimeelezea kwa uchache tu kuhusu maisha ya utotoni ya kijana Park Hoon pamoja na baba yake bila kusahau misukosuko waliyopitia.

Ni nini kiliendelea baada ya hapo?

Je walifanikiwa kurudi kwao Korea Kusini?

Ili kuyapata majibu ama majawabu ya maswali hayo basi itafute Drama hiyo inayokwenda kwa jina la Doctor Stranger na bila shaka maswali hayo yatajibika machoni pako wakati utakapokuwa ukiendelea kuitazama Drama hiyo.

Ahsante sana na pia karibu kwa maoni au maswali!

1565889892312-png.1182294

1565890276676-png.1182303

1565890111406-png.1182298
 
AKILI TATU

AKILI TATU

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2016
Messages
1,684
Points
2,000
AKILI TATU

AKILI TATU

JF-Expert Member
Joined Feb 10, 2016
1,684 2,000
Pia kama kuna anayejua kazi kadhaa za huyu mwamba hapo chini anipe nizijue..ama aniambie yuko wapi nije kuzifuata..

images-1-jpeg.1182371
 
View attachment 1182294
View attachment 1182303
View attachment 1182298
Nakuheshimu sana jombaaaa
 
FRANC THE GREAT

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Messages
1,792
Points
2,000
FRANC THE GREAT

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined May 27, 2016
1,792 2,000
Hii ameigiza pia huyu mwaba hapo chiniView attachment 1182368
Pia naomba kujua filamu kadhaa alizoigiza huyu jamaa..namkubali sana aisee..move zake nyingi ni akili sana..hakurupuki
Huyo ni Mzee wa makamo Jun Kwang-ryul.

Kama unahitaji "ya kifalme" basi bila shaka utakuwa unahitaji Historical Drama na katika Historical Drama alizoigiza huyo mzee nguli kabisa katika Tasnia ni kama zifuatavyo;
 • Jumong (2006)
 • Warrior Baek Dong Soo (2011)
 • Jang Hee-Bin / Royal Story (2003)
 • King and I (2007)
 • Royal Gambler (2016)
 • Flower in Prison (2016)
 • Jung-Yi, Goddess of Fire (2013)
 • Heo Joon (1999)

Kati ya hizo nilizokutajia, alizoigiza kama 'Mfalme' ni mbili nazo ni;
 • Jumong (2006): Aliigiza kama Mfalme Geumwa wa Buyeo
 • Jang Hee-Bin / Royal Story (2003): Aliigiza kama Mfalme Sukjong wa Joseon

Kazi nyinginezo alizofanya huyo mzee wa makamo ni kama ifuatavyo;
 • Swallow the Sun
 • The Man in the Mask
 • Witch at Court
 • You Are Too Much
 • Sign n.k.

Mpaka hapo nadhani tutakuwa tumekula ng'ombe mzima kasoro mkia ambao bado tunautafuta.
 
FRANC THE GREAT

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Messages
1,792
Points
2,000
FRANC THE GREAT

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined May 27, 2016
1,792 2,000
Pia kama kuna anayejua kazi kadhaa za huyu mwamba hapo chini anipe nizijue..ama aniambie yuko wapi nije kuzifuata..

View attachment 1182371
Hapa unamzungumzia Ji Sung.

Kazi alizofanya Ji Sung hususani Drama zipo nyingi tu na zifuatazo ni baadhi tu:
 • Defendant (2017)
 • Kim Su-Ro, The Iron King (2010)
 • Kill Me, Heal Me (2015)
 • Royal Family (2011)
 • The Great Seer (2012)
 • Swallow the Sun (2009)
 • Protect The Boss (2011)
 • Secret Love (2013)
 • Entertainer (2016)
 • Doctor John (2019)
 • Familiar Wife (2018) n.k.
 
FRANC THE GREAT

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Messages
1,792
Points
2,000
FRANC THE GREAT

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined May 27, 2016
1,792 2,000
Episode ya 9 tu nimeikinai
Duh! Hilo pengine ni kutokana na 'Role' ya Ji Chang-wook.

Lakini, sidhani kama Ji Chang-wook alifeli sana kwa sababu ndivyo 'Storyline' ilivyokuwa inamtaka afanye. Maana hata katika Historia inaelezwa kuwa Toghon Temur aliyumbishwa na akayumba sana katika utawala wake kipindi cha mwanzoni. Alikuwa 'Very Weak'.

Alikuwa akiendeshwa sana na Warlords kama akina Bayan n.k. lakini alivyokuwa akizidi kukua (Mature), alibadilika sana na ule woga na udhaifu wa mwanzoni ulipungua kwa kiasi kikubwa kama si kuisha kabisa.

Na kwa upande wa Ji Chang-wook mwenyewe nadhani hii Empress Ki ni moja ya Drama ambazo jamaa amecheza vizuri sana kuliko baadhi ambazo alicheza pia kama vile Historical Drama: Warrior Baek Dong Soo n.k.
 
AKILI TATU

AKILI TATU

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2016
Messages
1,684
Points
2,000
AKILI TATU

AKILI TATU

JF-Expert Member
Joined Feb 10, 2016
1,684 2,000
Hapa unamzungumzia Ji Sung.

Kazi alizofanya Ji Sung hususani Drama zipo nyingi tu na zifuatazo ni baadhi tu:
 • Defendant (2017)
 • Kim Su-Ro, The Iron King (2010)
 • Kill Me, Heal Me (2015)
 • Royal Family (2011)
 • The Great Seer (2012)
 • Swallow the Sun (2009)
 • Protect The Boss (2011)
 • Secret Love (2013)
 • Entertainer (2016)
 • Doctor John (2019)
 • Familiar Wife (2018) n.k.
Nimeona mbili tu za defendant na swallow the sun..jamaa namkubali sana katika kazi zake..vipi naweza pata kwenye flash hizo kazo zake kama unazo mkuu??
 
Forum statistics

Threads 1,325,757
Members 509,278
Posts 32,201,993
Top