Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

WAIGIZAJI WA KIKE WASAIDIZI (SUPPORTING ACTRESS) WANAONIVUTIA KWENYE TAMTHILIA ZA
KOREA.


Mara ya mwisho nakumbuka niliweka listi ya waigizaji wa kiume ambao (wenye umri wa Zaidi ya miaka 40) ambao mara nyingi huigiza kama supporting actors ambao tokea nianze kufuatilia Korean drama wamekuwa wakinivutia kutokana na uwezo wao wa kuigiza haijalishi nafasi gani wanaigiza.Leo ni zamu ya wanawake, inawezekana siwafahamu wengi sana ila hawa wafuatao ni baadhi ya wanaonivutia kutokana na uwezo wao katika tasnia ya uigizaji.

1) Song Ok Sook: kama ni mfuatiliaji mzuri wa Korean drama ni lazima utakuwa unamfahamu mwanamama huyu ambaye amezaliwa miaka 56 iliyopita.Ni mwanamama (ahjumma) mcheshi sana na anayeheshimu kazi yake,miongoni mwa kazi alizoigiza ni BIG MAN,TREE WITH DEEP ROOTS, QUEEN SEONDEOK,MISSING YOU,ROOFTOP PRINCE.

b1zEZgG4_96042d_c.jpg


2) Lee Il Hwa: inawezekana ameshakuwa ni mtu mzima ila bado ni mrembo na mara nyingi anaigiza kama ni mama.ameigiza tamthilia kama QUEEN OF AMBITION,YOU WHO COME FROM THE STAR,ILJIMAE,UGLY ALERT.
View attachment 373321


3) Kim Sung Ryung: mara ya mwanzo nilimuona kwenye tamthilia ya YOU ARE BEAUTIFUL alikuwa mkorofi sana,baadae nilimuona kwenye Princess Jamamyung ambayo aliigiza kama mke wa mfalme wa taifa la Nakrang ambaye pia ni mama wa Jamyung,pia nilimuona kwenye THE HEIRS,IL JIMAE,QUEEN OF AMBITIONS, ana miaka 49.
View attachment 373323

4) Oh Yeon Soo: ana miaka 44 aliigiza tamthilia ya PRINCE OF THE LEGEND kama ni mama wa Jumong,chakuvutia na kushangaza yeye na Song il kook ambaye aliigiza kama jumong wamezaliwa mwaka mmoja.kwenye tamthilia ya GYE BAEK pia aliigiza kama ni Queen wa taifa la Baekje,tamthilia nyengine ni TRIANGLE na IRIS 2.
View attachment 373326


5) Kim Mi Kyung: ana miaka 52,ana kipaji na ni mbunifu haijalishi ni nafasi gani anaigiza katu hatomkera mtazamaji.nimemuona kwenye tamthilia nyingi sana kama vile FAITH,THE HEIRS,ITS OKAY THAT’S LOVE,MISSING YOU,MASTERS SUN,SUNGYUKNWAN SCANDALS.
View attachment 373331


6) Kim Soo Mi: ana miaka 64 alinivutia sana kwenye , VAMPIRE IDOL, LEGENDARY WITCH,KING AND I,INCARNATION OF MONEY ni mtaratibu sana anapozungumza.

View attachment 373332
7) Bae Jong Ok:ana miaka 52 na ni miongoni mwa waigizaji ninaowakubali sana haijalishi nafasi gani anaigiza nilimpenda sana kwenye KIM SO ROO,pia ameigiza tamthilia kama THAT WINTER THE WIND BLOWS,na SPY ambayo alicheza kama mpelelezi wa taifa la Korea ya Kaskazini.
View attachment 373333


8) Kim Hae Sook: ana miaka 60 ni ahjumma,unaweza kumuweka katika kundi lolote unalotaka ikiwa ni ukorofi,upole,vichekesho.nilimpenda kwenye WINTER SONATA ambayo aliigiza kama ni mama wa Choi Jin Woo.tamthilia nyengine alizoigiza ni CAIN AND ABEL,HOTEL KING,I CAN HEAR YOUR VOICE, PINOCCIO
View attachment 373334


9) Ban Hyo Jung: ana miaka 73 nimebahatika kuangalia drama mbili tu alizoigiza yeye ambazo ni SHINING INHERITANCE na ROOFTOP PRINCE.
Ban-Hyo-Jung-as-President-Yeo-Gil-Nam-Tae-Yong%E2%80%99s-grandmother.jpg


10) Im Ye Jin: ana miaka 56 alinivutia kwenye BOYS OVER FLOWER,MY PRINCESS na QUEEN SEONDEOK.
View attachment 373336


11) Kyun Miri:ana miaka 52 aliigiza drama ya jumong kama ni mama wa daeso na young po,pia ameigiza tamthilia ya JEWEL IN THE PALACE.

View attachment 373339
12) Go Hyun Jung: ana miaka 45 ila bado ni mrembo na alikichafua sana kwenye QUEEN SEONDEOK
View attachment 373337

13)Lee Bo Hae:ameigiza drama kama vile AMAN CALLED A GOD,IRIS 2,KING GWAGGAETO,terms of endearment
d3kB2YZL_e075b1_c.jpg

14)kim mi sook:kwa maoni yangu yeye ndio bridget bardot wa korea naamini kama ni mfuatiliaji wa korean drama utakubali,ameigiza tamthilia nyingi tu kama vile CITY HUNTER,FLOWER IN PRISON,QUEEN INSOO,ALL ABOUT MY MOM
latest

15)
Choi Ran :nilimpenda kwenye HONG GIL DONG katika harakati za kugombamia madaraka ya kifalme,ana miaka 56.tamthlia nyengine alizoigiza ni POSEIDON,SWALLOW THE SUN,GYE BAEK,YOU ARE BEAUTIFUL.
Choi_Ran-p2.jpg

16)
Chae Sira:
jee umepata nafasi ya kuangalia tamthilia ya HAESHIN(emperor of the sea) EMPRESS CHUNCHU,TERMS OF ENDEARMENT,QUEEN INSOO,UNKIND LADIES,ni mwanamama ngangari anayejua nini maana ya uigizaji.ana miaka 49 ila mimi nimempenda kwenye tamthilia ya FIVE FINGERS
View attachment 374452
Hah! Kipindi hiki ulikuwa na madude ya kutosha.
 
Young po kacheza zingine zipi tofauti na Jumong?
Kacheza 'Drama' nyingine nyingi tu tofauti na Jumong (Prince of Legend):
  • Everybody, Kimchi! (2014)
  • Kangnam Scandal (2018)
  • Pit-a-pat, My Love (2011)
  • That Man Oh Soo (2018)
  • Gu Am Heo Joon (2013)
  • Twinkle Twinkle (2011)
  • Can't Stop Now (2009)
  • Beautiful Mind (2016)
  • Always Spring (2016)

Ongezea na nyingine 'Historical' inaitwa Jejungwon (2010).
 
Tangu nianze kuangalia Korean drama to me I think jumong ndo best drama of all time
Wahenga waliwahi kusema hivi, nanukuu;

"Chanda chema huvikwa pete", mwisho wa kunukuu.

Ninachomaanisha ni kuwa, kizuri siku zote hakina budi kupewa sifa yake njema na kwa msingi huo basi, nami pia sina budi kuipa sifa njema Prince of the Legend ama Jumong kwa jinsi ilivyoweza kuyafanya yafuatayo;

  • Kutupatia mafundisho ya kihistoria yahusuyo kuanzishwa kwa taifa imara kabisa la kipindi hicho la Goguryeo. Taifa ambalo limewahi kutoa viongozi mashuhuri sana na wababe wa vita wa kipindi kile kama vile, mwanzilishi mwenyewe wa taifa hilo, The Great Dongmyeong wa Goguryeo ama ukipenda muite 'Jumong', bila kusahau mwamba wa vita mwingine ajulikanaye kama Gwanggaeto The Great. Pia bila kusahau Majenerali wengi wa vita walioliwezesha taifa hilo kuwa imara zaidi hususani katika masuala ya kijeshi.

  • Pia, imetupatia burudani ya kutosha kabisa hususani jinsi gani wahusika katika shughuli nzima ya uandaaji wa 'Drama' hiyo walivyoweza kufanya kazi kubwa sana yenye utulivu wa hali ya juu katika kuiandaa na kisha kuitengeneza 'Drama' hiyo. Hakika wanastahili pongezi sana. Katika upande wa burudani hasa ucheshi tunakumbuka jinsi gani Young-po na 'genge' lake walivyoweza kutufanya tufurahi bila kusahau akina Dochi, Mo Palmo na wengineo waliohakikisha kwamba tunaendelea kuitazama 'Drama' hiyo na kuifurahia bila kuchoka.
 
aise guys nitumie application ipi kudownload korean series kwenye PC maana torrent inakataa. "Kingdom" ni pekee ilikubali.
 
, The Great Dongmyeong wa Goguryeo ama ukipenda muite 'Jumong', bila kusahau mwamba wa vita mwingine ajulikanaye kama Gwanggaeto The Great. Pia bila kusahau Majenerali wengi wa vita walioliwezesha taifa hilo kuwa imara zaidi hususani katika masuala ya kijeshi.
Huyo Gwanggaetto ndo mwenye Gogryeo yake, Spirit aliitoa kwa Jumong akafanya makubwa zaidi yake.
Lakini pia Haujamtaja Daemusin( god of war) pia alikuwa mwamba huyu.
 
Huyo Gwanggaetto ndo mwenye Gogryeo yake, Spirit aliitoa kwa Jumong akafanya makubwa zaidi yake.
Lakini pia Haujamtaja Daemusin( god of war) pia alikuwa mwamba huyu.
Yeah! Daemusin pia.

Ahsante kwa kunikumbusha kuhusiana na huyo mtu ambaye pia alikuwa na mchango mkubwa sana katika taifa imara kabisa la Goguryeo tena hasa pale alipoweza kulivamia na kuteka maeneo (Conquer) taifa lingine lililokuwa likisumbua sana kipindi hicho la Buyeo ya Mashariki lililokuwa likitawaliwa na Mfalme mmoja maarufu pia aitwae Daeso.

Hayo yalikuwa ni mafanikio makubwa sana ya Daemusin na Goguryeo yake ambaye alikuwa ni mjukuu wa muanzilishi wa taifa hilo la Goguryeo, Jumong.
 
Yeah! Daemusin pia.

Ahsante kwa kunikumbusha kuhusiana na huyo mtu ambaye pia alikuwa na mchango mkubwa sana katika taifa imara kabisa la Goguryeo tena hasa pale alipoweza kulivamia na kuteka maeneo (Conquer) taifa lingine lililokuwa likisumbua sana kipindi hicho la Buyeo ya Mashariki lililokuwa likitawaliwa na Mfalme mmoja maarufu pia aitwae Daeso.

Hayo yalikuwa ni mafanikio makubwa sana ya Daemusin na Goguryeo yake ambaye alikuwa ni mjukuu wa muanzilishi wa taifa hilo la Goguryeo, Jumong.
Pia kuikonka Nangrang
 
ni kwa sababu damu ilikuwa bado inanichemka tofauti na nyakati hizi za mwishoni mwa utawala wangu
Franc the Great anaonekana ndo mrithi. Ila nasikitishwa huenda ufalme huu ukaanguka, kiukweli hali ni mbaya kama nayoishuhudia sasa hivi ya Silla.
Ila huyu Binti ambaye ni mwana wa mfanya biashara wa Geumsung, ambaye msimuliaji anatueleza kuwa atakuja kuwa mke wa pili wa mzee Wang Guhn, ni binti anaejielewa na yuko vizuri kichwani. Ndo naingia ep 60/200
 
Back
Top Bottom