Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Hazina purukushani hazina kushtuana roho,romance zimedhibitiwa vizuri. Kitu kinashuka taratiiibu kama ni weekend halafu unayo full mambo yanakua bomba

Hivi ulishawahi kuangalia movie kisha actor au actress akashtuka au kakurupushwa nawe ukashtuka moyo ukaruka sarakasi za kutosha?hizi mambo ni chache sana kwenye family drama ila sasa tatizo lake watazamaji wakinogewa director anaamua kuirefusha au kuivuuutaaa mpaka kero.
upo sahihi familia ni kama maji safi ambayo huwezi kuyaepuka kimatumizi, baadhi ya wakati unatamani uwe mbali na familia yako kwa kigezo cha kutaka uhuru at the end unajikuta unatamani tena kurudisha ukaribu na wanafamilia wenzako.

hii dhana ya familia inaonekana wakorea wameifahamu zaidi ndio maana wanapendelea kuangalia drama zenye maudhui hayo.
 
WAIKIKI SEASON 2
Kwa wale wapenzi wa comedy season 2 ya waikiki imeanza rasmi siku ya jana, haijalishi hukubahatika kuangalia season 1 hii inakuhusu kuifuatilia.
unapaswa mbavu zako uzipeleke kwanza kwa fundi seremala apate kuziweka sawa zisije zikavunjika (ni amri na si ombi) kabla hujaingia kwenye ulimwengu wa waikiki.

aminas japokuwa bado unaendelea kusherehekea ushindi wa simba, na Taifa stars pindi utakapomaliza kugonga chupa zako za soju ya makonda naomba urudi kijiweni kwetu kabla sijachukia tafadhali.

Lee Yi Kyung a.k.a mzee wa gwenchanah gwenchanah ndiye muigizaji pekee aliyeshiriki season 1 na 2.
namnukuu director Lee Chang Min:

lee yi kyung amekuwa akija mara kwa mara ofisini kwangu, sikufikiria mara mbili kufanya maamuzi ya kumchagua tena kushiriki season 2. Kuhusu kuwachagua waigizaji wengine aliendelea kusema takribani waigizaji wote wana viwango vikubwa, nilitaka kuonyesha upande mwengine wa vipaji vyao vya uigizaji (comedy) na kiukweli nilikuwa nikiwagombeza mara kwa mara pindi wanapofanya makosa
View attachment 1054148


lets go (가자 = gaja)
nimemkumbuka my beautiful chewbacca na style yake ya muharmusi fashion style
View attachment 1054150
  1. Watch Eulachacha Waikiki 2 Episode 1 online at Dramanice
hii taarifa nimeiona wakati ambao bando langu limebakia mb 350, pumbavu nitaitafuta magharibi ya leo inshaallah ep 1 pamoja na 2 kama itakuwa imeshawekwa subtitle na viki.

update:
episode 1 ya season 1 iliangaliwa kwa asilimia 1.7.
episode 1 ya season 2 imeangaliwa kwa asilimia 2.118.

tusisahau JTBC ni cable tv hivyo basi ni tofauti na mashirika ya umma kama vile MBC, KBS, SBS kwa kufuatiliwa, unaweza kukuta hata huko korea kuna watu ni mwendo wa TBC mchana kutwa.
Nimeanza kuitazama nmecheeeka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hazina purukushani hazina kushtuana roho,romance zimedhibitiwa vizuri. Kitu kinashuka taratiiibu kama ni weekend halafu unayo full mambo yanakua bomba

Hivi ulishawahi kuangalia movie kisha actor au actress akashtuka au kakurupushwa nawe ukashtuka moyo ukaruka sarakasi za kutosha?hizi mambo ni chache sana kwenye family drama ila sasa tatizo lake watazamajo wakinogewa director anaamua kuirefusha au kuivuuutaaa mpaka kero.
hahahahahaaaaaa sina cha kuongeza.
 
Nachoipendea Waikiki Ni Auta Cheka Tu! Lazima Kuna Kitu Utatoka Nacho! Vingi Nimejifunza Na Najifunza Pitia Hii Drama!
huyu rebecca amezidi maajabu (hatari sana lakini salama)
majira ya usiku ndio nilianza kuifuatilia huwezi amini nilikuwa nacheka mpaka niwakaamsha waliokuwa usingizini.

ile scene ya historical film imenichekesha sana, jun ki anataka kwenda chooni ameshikwa na haja ndogo upande wa pili director hasikii lugha yoyote.

chewbacca alipaswa arudi tena.

hahahahahahahahaaaaaa$^&*^#@)({}:".,/
 
huyu rebecca amezidi maajabu (hatari sana lakini salama)
majira ya usiku ndio nilianza kuifuatilia huwezi amini nilikuwa nacheka mpaka niwakaamsha waliokuwa usingizini.

ile scene ya historical film imenichekesha sana, jun ki anataka kwenda chooni ameshikwa na haja ndogo upande wa pili director hasikii lugha yoyote.

chewbacca alipaswa arudi tena.

hahahahahahahahaaaaaa$^&*^#@)({}:".,/

Nimecheka Kuna Mahala Nilikuepo Kuna Mtu Mpka Akaamua kunifukuza!

Jun Ki Ni Chizi chizi Wa Mwisho! Akili Zake Si Nzuri....Ila Rebecca Katisha 🤣🤣🤣

Nilipende pia Ile Scene Ya Wo Shik Alivyopelekwa Kubembea na Mijitu Mizima Ile!

Hiii Drama Ni Nzuri Sana Kiukweli!
 
Touch Your Heart” Shares Behind-The-Scenes Photos And Thoughts From Cast As Drama Comes To An End

tvN’s “Touch Your Heart” aired its final episode on March 28.

Lee Dong Wook : ameigiza uhusika wa mwanasheria anayeitwa Kwon Jung Rok
nina furaha kuona waigizaji wote na staff members wakiwa na afya njema baada ya kumalizika kwa drama hii, nilifanya kazi na Yoo In Na miaka miwili iliopita kupitia drama inayoitwa Goblin, namshukuru sana kwa ushirikiano wake mkubwa aliounyesha kwangu, mwisho nataka niwashukuru watazamaji wote wa touch your heart drama kwa kuwa nasi kipindi chote.

Yoo In Na
nimefurahi baada ya kupata nafasi ya kuigiza uhusika wa Oh Jin Shim, nitoe shukurani zangu za dhati kwa waigizaji wote, director, staff tuliofanya kazi kwa takribani miezi minne bila ya kuwasahau mashabiki wote wa drama hii.

kumalizika kwa touch your heart ndio ujio wa Her Private Life drama ifikapo April 10.
ina maana next wednesday and thursday hakutakuwa na drama kupitia TvN.

vizuri sana kwa kunipunguzia mzigo wangu wa MB, kama ndege ya taifa inapakwa rangi kwa millioni 5 badala ya millioni 200 kwa nini mlalahoi kama mimi nisifurahie bajeti yangu ya mb.
1553809424323.png
 
Nimecheka Kuna Mahala Nilikuepo Kuna Mtu Mpka Akaamua kunifukuza!

Jun Ki Ni Chizi chizi Wa Mwisho! Akili Zake Si Nzuri....Ila Rebecca Katisha 🤣🤣🤣

Nilipende pia Ile Scene Ya Wo Shik Alivyopelekwa Kubembea na Mijitu Mizima Ile!

Hiii Drama Ni Nzuri Sana Kiukweli!
hahahahahahahaaaaaa
halafu season 2 ameamua kuja na style ya kujaza maji mdomoni halafu anayarusha kama mdudu nyoka.
teh teh teh yule jamaa nina wasiwasi amezaliwa tarehe 32 DECEMBER.
ukisikia comedy ndio zile na si za huku kwetu

ana style fulani ya kucheka hata kama upo kwenye ibada lazima ufuate nyayo zake.
 
Hurrayyyyyyyyy
Hatimaye nimemaliza kuangalia King Gwanggaeto The Great. Nimechokaaaaa
Ilikuwa safari ndefu ya episodes 92 ila ya kuvutia na kusikitisha.
Ni nzuri, nimeikubali.

Asante Great Conqueror kwa pendekezo, lilikuwa pendekezo bora.
Bado naangalia na Yi San pia japo sijafika mbali sana, nipo episode ya 28 nataka niangalie mpya nichangamke kidogo.

Nimepewa mapendekezo mengi ila naona bora niangalie The Memories of Alhambra. Nasikia ni nzuri...

Damushin nampenda sana Jin Jin Hee, alijua kunishika kwenye Dong Yi sana. Romance yake na Dong Yi ilikuwa balaa hahaaaaa
Sikulala vizuri wiki nzima hadi nilipoimaliza. Hata kwenye Jewel in the Palace (The Great Jang Geum) alitisha sana, jamaa anazijulia scene zake na wadada hatariiiiiii.
Kuna drama moja niliiona kaicheza inaitwa The Great Seer, nitaiangalia nikipata muda.

Halafu Damushin kuna pendekezo moja la drama ulinipa nimeisahau, ilikuwa baada ya mimi kumaliza kuangalia Jing Birok nikaomba list ya historical drama zenye akili na siasa kali, nimeisahau kidogo.
Kama utaweza kunikumbusha nitashukuru.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Halafu @Damushin kuna pendekezo moja la drama ulinipa nimeisahau, ilikuwa baada ya mimi kumaliza kuangalia Jing Birok nikaomba list ya historical drama zenye akili na siasa kali, nimeisahau kidogo.
Kama utaweza kunikumbusha nitashukuru.
yi bang win poem

This won’t matter, that won’t matter.
The walls behind the temple of the city's deity* has fallen - shall it be this
Let us mingle together like this and enjoy it for a hundred years.
(Yi Bang-won is declaring the death of the era - the Goryeo Dynasty)

great thinker jeong mong jo poem: anamjibu
Though I die and die again a hundred times,
That my bones turn to dust, whether my soul remains or not,
Ever loyal to my Lord, how can this red heart ever fade away?

  1. kwenye siasa hakuna makubaliano ndio maana kila siku kuna umwagaji wa damu unaoweza kuepukika, tafsiri halisi ya neno siasa ni kitendo cha kulipiza kisasi kwa mpinzani wako haijalishi ametenda jambo jema, kwenye siasa umwagaji wa damu na ulipizaji kisasi hautakwisha, hiyo ndio maana halisi ya siasa.
  2. kwenye siasa sote tunaishi kwenye kilele cha mlima na wala haichukui muda mkubwa sana kwa mmoja wetu kudondoka kwenye kilima cha siasa,
  3. kwenye siasa yeyote aliyepoteza nguvu hana utofauti wowote na marehemu na hata nguo ya ndani pia atapangiwa kuvaa.
nisikuchoshe itafute hii drama haijalishi umeshaangalia six flying dragons pamoja na the greet seer drama.
ila usisahau ni wachache sana wanaoua kwa upanga na wao wakafa kwa upanga isipokuwa yule ambaye ataweka udhaifu kwenye ngome yake kama alivyofanya mwanaharakati jung do jeon a.k.a sambong.

nimetembelea kissassian.sh bahati mbaya sijakutana na link ya hii drama​
 
@Damushin nampenda sana Jin Jin Hee, alijua kunishika kwenye Dong Yi sana. Romance yake na Dong Yi ilikuwa balaa hahaaaaa
Sikulala vizuri wiki nzima hadi nilipoimaliza. Hata kwenye Jewel in the Palace (The Great Jang Geum) alitisha sana, jamaa anazijulia scene zake na wadada hatariiiiiii.
Kuna drama moja niliiona kaicheza inaitwa The Great Seer, nitaiangalia nikipata muda.
ulishawahi kuagalia drama yake inayoitwa MISTY?

jewel in the palace sijaiangalia
dong yi hata sikumbuki nilifika episode ya ngapi, nyakati hizo ndio naingia ulimwengu wa korea, kuna rafiki alikuwa anapenda drama za korea mpaka akaniingiza kwenye ulimwengu huu na kutoka siwezi kama uchawini.
 
my queen hata huku kwetu tunatembelewa na misimu minne kila mwaka lakini cha ajabu msimu wa jua kali ndio hutaka sifa kama za bwana yule mvaa suti za bendera.
laiti kama nisingelikuwa ni mfuasi wa buddha basi usiku huu ningelikwenda kwa mchumba wa zamani nikamshushia mapovu kama ya lee jun ki, bahati nzuri sana ndio hivyo mimi ni mwendo wa kukesha kwenye hekalu za dini pendwa.

aminas japokuwa muda huu unaota ndoto za panya anamshinda paka kwa ujanja, nikupe taarifa my queen taeyeon amerudi.

four seasons, nadhani huu wimbo unakuhusu japokuwa maisha yako ya mahusiano siyafahamu (nimegeuka mtabiri).
we missed each other we are sick of each other
you were my world but ill let you go.


ninavyowapenda waimbaji wakorea asilimia 95 wanaweza kuperform live bila ya mashabiki kuchoshwa na mikono juu kama tunamuomba mungu atushushie fedha na dhahabu huko aliko.
wenzetu halafu wanawajenga waimbaji wao kupitia show tofauti zinazoendeshwa na vyombo vya habari na chengine hawajisikii pindi wanapoalikwa kuperform labda wazongwe na ratiba.
unakuta vyombo vya habari vingi vinavyoendesha variety show za muziki wana kumbi na studio zao kubwa sana.
wakorea wametuacha mbali sana utafikiri wamepata uhuru miaka 300 iliopita.
 
siku 3 zilizopita:
Girls’ Generation’s Taeyeon took No. 1 on global iTunes charts and more:
Taeyeon’s b-side “Blue” has also been a hit elsewhere in the world. It came in at No. 1 on the iTunes Top Songs chart in 11 regions: Saudi Arabia, United Arab Emirates, Singapore, Thailand, Cambodia, Malaysia, Philippines, Taiwan, Hong Kong, Macao, and Vietnam.

kama waarabu kanzu wapenda dini kwa maslahi yao tu wanapenda muziki wa korea kwa nini mimi mlala hoi nisiyemiliki hata kisima cha maji machafu nisiwapende wakorea.
korea forever mpaka nifanikiwe kumiliki apartment yangu maeneo ya BUSAN.

sidhani kama mwanadamu asiyevutiwa na rangi blue, ndio asili ya mawingu, bahari na ndio rangi inayo onyesha creativity pamoja na intelligency.
ndio rangi inayowakilisha loyalty,wisdom na hata uaminifu, ukiangalia rangi ya blue stress zote za umasikini zinakimbia lakini jaribu kuangalia rangi ya ...................................., unaweza kujikuta upo ICU kwa stress.
hata marehemu wote wanapenda rangi blue huko waliko kwa sababu wamechoshwa na giza.
wajinga wataitaja rangi kijani na manjano kwenye nafasi tupu nilioiwacha hapo juu​

kuna mtumishi mmoja kwa jinsi nilivyoshindwa kupata usingizi muda huu nina wasiwasi ananinyemelea achukue roho yake lakini nishamwambia kama ndio lengo lake basi silali, tutakesha pamoja kama mbuzi mzazi.
 
Halafu @Damushin kuna pendekezo moja la drama ulinipa nimeisahau, ilikuwa baada ya mimi kumaliza kuangalia Jing Birok nikaomba list ya historical drama zenye akili na siasa kali, nimeisahau kidogo.
Kama utaweza kunikumbusha nitashukuru.
kwangu mimi huwezi kuizungumzia nchi ya Joseon bila ya jeong do jeon(sambong). nikiangalia harakati zake za kupigania usawa kwenye taifa la Goryeo kwa kupambana na waziri mkuu lee I-Nim mpaka akaamua kuwa muasi na kufanya mapinduzi, kutafautiana na rafiki yake kipenzi Jeong mong ju (poeun) great thinker wa kipindi hicho ambaye alikuwa akiamini wao kwa pamoja wana uwezo wa kurudisha heshima ya taifa la goryeo ila bahati mbaya sambong hakuwa tena na mawazo ya goryeo, kwangu mimi urafiki wa sambong na poeun ulikuwa ni zaidi ya urafiki wa lipumba na seif.

ukiangalia drama hii ya jeong do jeon ndipo utapata kufahamu zaidi jinsi walivyokutana kwa mara ya kwanza kati ya sambong na general yi seong ye mnamo mwaka 1383 kwenye kambi za hamgyong wakati ambao yi seong ye alikuwa anaongoza vita dhidi ya wavamizi wa japan.

mwaka 1388 wakati ambao taifa la mongols lilipoivamia taifa la goryeo ndipo yi seong ye akaamrishwa kuivamia kaskazini mwa liaodong ila cha kushangaza lee seong ye akakataa oda ya mfalme na ya general choi young na akatoa sababu zifuatazo kwa ushauri wa mwanamipango sambong
  1. taifa la goryeo ni dogo hivyo halina uwezo wa kuvamia taifa kubwa
  2. hali ya hewa ilikuwa ni ya mvua hivyo basi msafara wa kuelekea kaskazini utakumbana na dhoruba nyingi
  3. kama nchi itaelekea vitani upande wa kaskazini basi wajapan watavamia upande wa kusini
  4. kwa kuwa ni wakati wa mvua basi wananchi wanapaswa kulima na si kwenda vitani baada ya majibizano ya muda mrefu yi seong ye akaamua kurudi mji mkuu wa gaegyeong pamoja na jeshi lake na kutokezea vita ya wenye kwa wenyewe jambo lililopelekea general choi young kushindwa vita na ukawa ni mwisho wake wa kuwa na nguvu.
1553908326709.png

huyu choi young alijitabiria kabla ya kifo chake ya kwamba kaburi lake halitaota majani, ilichukua miaka mingi mnooo kaburi lake kuota majani.


kukosa nguvu kwa choi young kulipelekea kambi inayopigania goryeo ipoteze nguvu kubwa na kubaki jeong mong jo peke yake na upinzani dhidi ya rafiki yake kipenzi sambong ulizidi hadi kupelekea kutoa amri ya sambong anyongwe.

ila siku chache kabla ya kunyongwa kwa sambong lee bang won ambaye alikuwa ni mtoto wa tano wa general yi seong ye alimuua jeong mong jo (poeun) kwenye daraja la sonjukkyo na ukawa ndio mwisho wa harakati zake za kuipigania goryeo.
kabla ya kifo chake aliandika shairi na kumtumia yi bangwon ampelekee baba yake ambalo nimeliweka post ya juu.

Though I die and die again a hundred times,
That my bones turn to dust, whether my soul remains or not,
Ever loyal to my Lord, how can this red heart ever fade away?
jamaa alikuwa mzalendo aliyepitiliza, alikuwa akimaanisha ya kwamba kwenye maisha yake hawezi kuitumikia GORYEO halafu baadae aitumikie JOSEON hata kama atakufa mara 100.

yi seong ye akawa mfalme wa joseon na ukawa ndio mwisho wa utawala wa wang clan ulioasisiwa na mfalme wang gun na kuanza kwa utawala wa lee (yi) clan sambong akawa waziri mkuu wa joseon na ndiye aliyesimamia ujenzi wa ikulu ya joseon na akaipa jina la Gyeongbokgung palace ambayo mpaka leo inatumika kwa ajili ya kuigizia drama na pia kuwa ni kivutio cha utalii.

hii ikulu wananchi waliwahi kuichoma moto kwenye vita ya imjin baada ya mfalme seonjo kukimbia ikulu
1553908599573.png

vita ya madaraka ikaingia tena kwenye taifa la joseon baada ya yi bang won kutokuchaguliwa kuwa ni mrithi wa kiti cha mfalme ambapo nafasi yake alipewa mtoto wa kwanza wa mke wa pili wa general yiseongye (yi bangseok) na aliamini aliyesababisha yeye kukosa nafasi ni sambong kutokana na bifu la kumuua rafiki yake poeun.

kosa lile lile alolifanya general choi young la kutaka goryeo ivamie nchi ya china kwa ajili ya kuurudisha mji wa liaodong ambao kihistoria ilikuwa ni ngome ya goguryeo kabla utawala wake haujaanguka naye sambong alilirejea tena kwani naye aliamini joseon ina uwezo wa kuipiga china. siku chache baada ya kufa kwa malikia sindeok naye yi bangwon aliitumia nafasi hii kufanya mapinduzi kwa kuwaua ndugu zake ambao walizaliwa na mama wa kambo na pia kumuua sambong na wafuasi wake na akabeba ufalme.
1553908688730.png

yi bangwon akamtangaza sambong kama ni muasi wa taifa na mwili wake utupwe na pia akamtangaza jeong mong jo kama ni shujaa wa goryeo.
cha ajabu yi bang won bado aliendelea kutumia baadhi ya mifumo ilioanzishwa na sambong chini ya utawala wake.
  1. sambong aliamini ya kwamba nchi bora ni ile ambayo ina good connections kati ya kiongozi mkuu na wafuasi wake, it means yeye aliamini ya kwamba mfalme hapaswi kuwa na nguvu kubwa ya kimaamuzi kwa sababu itakuwa ni hatari hususani itakapotokezea siku ambayo taifa litatawaliwa na mwendawazimu wa matendo na si akili.
  2. yi bang won na wafuasi wake waliamini ya kwamba nchi bora ni ile ambayo itajengwa kwa nguvu na maamuzi ya mfalme au raisi kwa nyakati hizi kama ilivyo katiba ya TANZANIA ukiangalia kwa jicho la tatu.
  3. nilichopenda ni kwamba wote walikuwa wanawapigania raia na si maslahi yao tofauti na viongozi wa kileo, huyu yi bang won licha ya kujenga misingi imara ya joseon lakini alikuwa ni muuaji aliyevuka mipaka, inamaana sambong alikuwa sahihi kiupande fulani
ukimaliza hii itafute the great king sejong drama, imeelezea kiundani maisha ya lee bang won na utawala wake pamoja na utawala wa mtoto wake yi do (sejong the great).
raha ya drama za joseon uzifuatilie kwa mtiririko wa wafalme zinavutia sana​

best drama kwa mwaka 2014, humu ndani muna veterani watupu wanaofahamu maana halisi ya sanaa.
 
Back
Top Bottom