Nifah
JF-Expert Member
- Feb 12, 2014
- 31,511
- 65,143
kwangu mimi huwezi kuizungumzia nchi ya Joseon bila ya jeong do jeon(sambong). nikiangalia harakati zake za kupigania usawa kwenye taifa la Goryeo kwa kupambana na waziri mkuu lee I-Nim mpaka akaamua kuwa muasi na kufanya mapinduzi, kutafautiana na rafiki yake kipenzi Jeong mong ju (poeun) great thinker wa kipindi hicho ambaye alikuwa akiamini wao kwa pamoja wana uwezo wa kurudisha heshima ya taifa la goryeo ila bahati mbaya sambong hakuwa tena na mawazo ya goryeo, kwangu mimi urafiki wa sambong na poeun ulikuwa ni zaidi ya urafiki wa lipumba na seif.
ukiangalia drama hii ya jeong do jeon ndipo utapata kufahamu zaidi jinsi walivyokutana kwa mara ya kwanza kati ya sambong na general yi seong ye mnamo mwaka 1383 kwenye kambi za hamgyong wakati ambao yi seong ye alikuwa anaongoza vita dhidi ya wavamizi wa japan.
mwaka 1388 wakati ambao taifa la mongols lilipoivamia taifa la goryeo ndipo yi seong ye akaamrishwa kuivamia kaskazini mwa liaodong ila cha kushangaza lee seong ye akakataa oda ya mfalme na ya general choi young na akatoa sababu zifuatazo kwa ushauri wa mwanamipango sambong
View attachment 1057742
- taifa la goryeo ni dogo hivyo halina uwezo wa kuvamia taifa kubwa
- hali ya hewa ilikuwa ni ya mvua hivyo basi msafara wa kuelekea kaskazini utakumbana na dhoruba nyingi
- kama nchi itaelekea vitani upande wa kaskazini basi wajapan watavamia upande wa kusini
- kwa kuwa ni wakati wa mvua basi wananchi wanapaswa kulima na si kwenda vitani baada ya majibizano ya muda mrefu yi seong ye akaamua kurudi mji mkuu wa gaegyeong pamoja na jeshi lake na kutokezea vita ya wenye kwa wenyewe jambo lililopelekea general choi young kushindwa vita na ukawa ni mwisho wake wa kuwa na nguvu.
huyu choi young alijitabiria kabla ya kifo chake ya kwamba kaburi lake halitaota majani, ilichukua miaka mingi mnooo kaburi lake kuota majani.
kukosa nguvu kwa choi young kulipelekea kambi inayopigania goryeo ipoteze nguvu kubwa na kubaki jeong mong jo peke yake na upinzani dhidi ya rafiki yake kipenzi sambong ulizidi hadi kupelekea kutoa amri ya sambong anyongwe.
ila siku chache kabla ya kunyongwa kwa sambong lee bang won ambaye alikuwa ni mtoto wa tano wa general yi seong ye alimuua jeong mong jo (poeun) kwenye daraja la sonjukkyo na ukawa ndio mwisho wa harakati zake za kuipigania goryeo.
kabla ya kifo chake aliandika shairi na kumtumia yi bangwon ampelekee baba yake ambalo nimeliweka post ya juu.
Though I die and die again a hundred times,
That my bones turn to dust, whether my soul remains or not,
Ever loyal to my Lord, how can this red heart ever fade away?
jamaa alikuwa mzalendo aliyepitiliza, alikuwa akimaanisha ya kwamba kwenye maisha yake hawezi kuitumikia GORYEO halafu baadae aitumikie JOSEON hata kama atakufa mara 100.
yi seong ye akawa mfalme wa joseon na ukawa ndio mwisho wa utawala wa wang clan ulioasisiwa na mfalme wang gun na kuanza kwa utawala wa lee (yi) clan sambong akawa waziri mkuu wa joseon na ndiye aliyesimamia ujenzi wa ikulu ya joseon na akaipa jina la Gyeongbokgung palace ambayo mpaka leo inatumika kwa ajili ya kuigizia drama na pia kuwa ni kivutio cha utalii.
hii ikulu wananchi waliwahi kuichoma moto kwenye vita ya imjin baada ya mfalme seonjo kukimbia ikulu
View attachment 1057743
vita ya madaraka ikaingia tena kwenye taifa la joseon baada ya yi bang won kutokuchaguliwa kuwa ni mrithi wa kiti cha mfalme ambapo nafasi yake alipewa mtoto wa kwanza wa mke wa pili wa general yiseongye (yi bangseok) na aliamini aliyesababisha yeye kukosa nafasi ni sambong kutokana na bifu la kumuua rafiki yake poeun.
kosa lile lile alolifanya general choi young la kutaka goryeo ivamie nchi ya china kwa ajili ya kuurudisha mji wa liaodong ambao kihistoria ilikuwa ni ngome ya goguryeo kabla utawala wake haujaanguka naye sambong alilirejea tena kwani naye aliamini joseon ina uwezo wa kuipiga china. siku chache baada ya kufa kwa malikia sindeok naye yi bangwon aliitumia nafasi hii kufanya mapinduzi kwa kuwaua ndugu zake ambao walizaliwa na mama wa kambo na pia kumuua sambong na wafuasi wake na akabeba ufalme.
View attachment 1057744
yi bangwon akamtangaza sambong kama ni muasi wa taifa na mwili wake utupwe na pia akamtangaza jeong mong jo kama ni shujaa wa goryeo.
cha ajabu yi bang won bado aliendelea kutumia baadhi ya mifumo ilioanzishwa na sambong chini ya utawala wake.
ukimaliza hii itafute the great king sejong drama, imeelezea kiundani maisha ya lee bang won na utawala wake pamoja na utawala wa mtoto wake yi do (sejong the great).
- sambong aliamini ya kwamba nchi bora ni ile ambayo ina good connections kati ya kiongozi mkuu na wafuasi wake, it means yeye aliamini ya kwamba mfalme hapaswi kuwa na nguvu kubwa ya kimaamuzi kwa sababu itakuwa ni hatari hususani itakapotokezea siku ambayo taifa litatawaliwa na mwendawazimu wa matendo na si akili.
- yi bang won na wafuasi wake waliamini ya kwamba nchi bora ni ile ambayo itajengwa kwa nguvu na maamuzi ya mfalme au raisi kwa nyakati hizi kama ilivyo katiba ya TANZANIA ukiangalia kwa jicho la tatu.
- nilichopenda ni kwamba wote walikuwa wanawapigania raia na si maslahi yao tofauti na viongozi wa kileo, huyu yi bang won licha ya kujenga misingi imara ya joseon lakini alikuwa ni muuaji aliyevuka mipaka, inamaana sambong alikuwa sahihi kiupande fulani
raha ya drama za joseon uzifuatilie kwa mtiririko wa wafalme zinavutia sana
best drama kwa mwaka 2014, humu ndani muna veterani watupu wanaofahamu maana halisi ya sanaa.
Aiseeee wewe jamaa ni noma sana
Kwa wengine wasiojua hizi mambo zetu za Korea mimi huwa naonekana najuaaaa ila hapa najiona kabisa sijui.
Sasa jana baada ya kumaliza kuangalia King Gwanggaeto nikajikuta namuuliza swali mtu ambaye hajui mambo ya Korea baada ya kugundua Houyan ndio Beijing ya leo China.
Swali nililomuuliza ni kwamba “Ni wazi Korea, Japan na China zilikuwa ktk muunganiko. Ilikuwaje zimejitenga kama ilivyo leo hii?”
Nimengalia drama nyingi ila sio ktk mtiririko, na ili upate kulifahamu hili vyema basi uweze kuunganisha drama hizo ktk mtiririko...
Naomba unipe mtiririko mzuri/sahihi wa hizo drama ambazo zinaelezea/kuonesha mgawanyiko huo.
Hata ukielezea kwa maandishi pamoja na hizo drama itakuwa vizuri zaidi, asante.
Sent from my iPhone using JamiiForums