Dhana zinazowachanganya wengi kwenye muziki wa rap

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Ni rahisi kuziita common confused terminologies ambapo wapo wanaojua tofauti kati yao na huzichanganya kimazoea lakini wapo wanaotumia dhana hizi kwa kuzichanganya pasipo kujua tofauti zao. Hawa wanaweza kuitwa ignorant au blind followers.

Nimeandaa dhana nane ambazo nimezielezea kwa ufupi. Kwa mwenye uelewa zaidi ya huu uliobainishwa na kuainishwa hapa basi anaruhusiwa kujazia palipopungua.

1. RAP VS HIP HOP
As far as I remember, sikuwahi kujua kama kuna utofauti kati ya Rap na HIP HOP lakini katika kuchimba huku na kule ndipo nikagundua kuwa Rap ni aina ya muziki lakini Hip Hop ni UTAMADUNI mkubwa sana unaobeba viambata vingine vidogovidogo huku Rap ikiwa miongoni mwake.

Kuna wapiga machata ambao ni wana HIP HOP lakini hawajawahi kurap.
Wakati Solo akisema; "KUNA KURAP NA KUBWATA/ MAREPA NA MARAPA, KATUNI, TUNGO TATA/ WAPI ULIPO WE KAKA?"

Pina akagongelea nyundo kwenye msumari kwa kusema; "WASANII WANAUZA SURA, SI TUNAUZA MANENO/ KURAP MBONA WANARAP HATA WAIMBA MAYENO"

Umeshajua sasa kuwa NOT EVERY RANDOM GUY SEEN IN JERSEY IS A PLAYER, SOME ARE MERE BALL BOYS.

2. RAPPER VS EMCEE
Kuna upotoshaji mkubwa na mkanganyiko wa hali ya juu kuhusu watu hawa wawili.
Rapa anaweza akaingia popote na kuchana kwenye mdundo wowote lakini ili mtu aitwe EMCEE lazima akae kwenye mdundo wa Rap.

Tutabishana kuhusu midundo ya Rap, lakini ukikumbuka maneno kama " hii biti ni ngumu sana", "piga biti flani hivi ya kuchezeka" ndipo utaelewa mantiki ya kusema mdundo wa Rap.

Rejea aya ya pili ya hoja hii kisha kamsikilize KRS ONE akisema kwamba; AS A HIP HOP SCHOLAR, YOU ARE NOT EXPECTED TO BE HIP HOP ON MONDAY AND BE SOMETHING ELSE ON TUESDAY"
Tumeelewana siyo?

Kibongobongo, hii imeenda mbali, Emcee anaitwa hivyo na kupewa heshima yake lakini rapa anaitwa BONGO FLEVA.

Lord Eyes kwenye ngoma yake iitwayo NIMECHOKA ft NAZIZ anasema;
"Maprodyuza wa Kibongo, maDj wa Kibongo

Hii ni HIP TO THE HOP siyo FLEVA ZA BONGO (OOOIII)" halafu wanapokezana na Naz kwa kusema;
"WE NI RAPA, MI NI EMCEE"
Stori za kama Lord ni Rapa au Emcee, baki nazo. Nimefanya reference tu.

3. VERSE VS STANZA
Katika taaluma ya fasihi, verse ni mstari mmoja au mshororo ila stanza huitwa ubeti kwa Kiswahili, ikimaanisha mkusanyiko wa mistari au mishororo.

Si unakumbuka D KNOB alivyosema kwenye ELIMU MITAANI
"STUDIO MIKKA ANACHONGA, ANAULIZA KWANINI WIMBO WANGU UNA VESI MOJA??"
Kuna wimbo wenye mstari mmoja?? Hapa tunaona D KNOB ameenda na upepo wa wengi ambao unavuma mpaka leo hii.

4. WIMBO VS NYIMBO
Sijajua mwasisi wa neno NYIMBO kurejelea umoja ni nani, kiasi kwamba kizazi cha sasa kinaona ni sahihi kusema hivyo baada ya athari ya muda mrefu iliyotengenezwa na kaka zetu.

5. FASIHI VS MUZIKI
Kuanzia kizazi cha kwanza mpaka kizazi cha sasa, wasanii wengi hususani rappers huchukulia muziki na fasihi kama kitu kimoja.

Wengi hujinadi kuwa wanafanya FASIHI wakati wanachofanya ni muziki. Wanachochanganya ni kwamba muziki na fasihi ni watoto wa tumbo moja. Kupisha kupotosha wakiona neno muziki hawalitaki Basi watumie neno SANAA.

6. PRODUCER VS BEAT MAKER
Technically, producer ni yule aliyeingia darasani kuusoma muziki kuanzia maandalizi mpaka umaliziaji wa utengenezaji wa muziki husika lakini hapa Bongo, dogo mmoja ana passion ya muziki, amedownload VOLOKO, CUBASE au vitu gani gani sijui huko kapiga kick, kapiga snare, kagonga matrei ya mayai ukutani, studio hii hapa, ameshaitwa prodyuza!!

7 UNDERGROUND VS UPCOMING
"JAPO NIMETOKA NINA HASIRA KAMA UNDERGROUND" LANGA
"MAUNDERGROUND WANAFANYA RAP INANG'ARA" PROF JAY

Naomba mnisaidie kama wawili hawa waliwalenga wasanii wa mfumo wa maisha ya muziki uitwao HANDAKI au walimaanisha vijana waliokuwa wakichipukia kwenye Rap?
Underground ni mtu ambaye anaweza kuwa yupo miaka yote ila hafungamani na terms and conditions za mkondo mkuu wa upashanaji habari wakati msanii CHIPUKIZI ni yule ambaye yupo chini huko anajitafuta na anatafuta mtu wa kumshika mkono ili amwoneshe sehemu ya kupita na kuufikia mkondo mkuu.

NOT EVERY UNDERGROUND HEAD IS UPCOMING
Hii ni sawa na kusema THERE IS A HUGE DIFFERENCE BETWEEN A LOW KEY PERSON AND A PERSON WHO IS LESS KNOWN

Nilisema nina dondoo nane?? Hiyo ya mwisho itakuka siku nyingine.
 
Young Killer, ameingiza missing evеr since afunge ndoa,
Kuna time niliamini Bongo HIP HOP angеiokoa,
Sina ubaya brother, na sikatai unafanya poa,
But mi si shabiki ya hizo ngoma mpya unatoa...
 
Young Killer, ameingiza missing evеr since afunge ndoa,
Kuna time niliamini Bongo HIP HOP angеiokoa,
Sina ubaya brother, na sikatai unafanya poa,
But mi si shabiki ya hizo ngoma mpya unatoa...
Hii Ngoma ya khaligragph alipita na idea ya Ngoma ya fid Q.. inayoitwa "Tema knowledge"... Humu fid anawalaumu Sana wasanii wa hip-hop kufanya Ngoma za ovyo Sana..
"Nikisikiliza hip-hop ya bongo si-gain na-lose vingi...
Mistari Yao ni mfano wa kile kisichofaa kuandikwa
Sauti zao si za michano walifaa wajiunge misifa..."
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom