Kwa wanaume tu: Anaomba ushauri

Dec 13, 2015
21
2
Salamu zenu wakubwa kwa wadogo?

Ishu iko ivi, nina rafiki yangu wa karibu ambaye ameniomba ushauri. Mimi binafsi sijui nimshauri kipi kizuri. Naileta mbele yenu, wana JamiiForum hasa wanaume tumsaidie huyu ndugu yetu aokoe jhazi.

Mada iko kama ifuatavyo;

Ni mwanaume mwenye miaka 27. Bado anahangaika kutafuta maisha. Alikuwa na girlfriend wake ambaye walipendana sana hata kipindi rafiki yangu huyu akiwa hana kitu, kwa mdada huyu alimheshimu, alimjali na kumpenda.

Rafiki yangu amepata sehemu ya kujishikiza. Kwa jinsi anavyompenda msichana wake, anahofu kuwa anaweza akapoteza kibarua chake. Kibarua chenyewe, kinatishiwa kuota nyasi muda wowote.

Kosa lolote dogo linamfanya rafiki yangu huyu atishiwe kufukuzwa kila mara. Na mara mbili aliwahi kufukuzwa sababu ya msichana wake kujisahau kumhimiza rafiki yangu awahi kibaruani.

Jamaa amemwambia msichana wake waachane ili yeye aendelee kutafuta maisha. Msichana amelia sana na kuomba kujirekebisha.

Na rafiki yangu anakubali kuwa msichana wake ana mapenzi ya kweli kwake. Yeye anampenda ila hayuko radhi kupoteza kibarua.

Jamani, kwa ushauri wenu, mnaona ni busara wawili hawa wakaachana ama unaona jamaa afanye nini hapo?
 
Yaani sijui hata unataka nini!!! mtu hajamuoa then anamzuia asiwahi kazini!!! what: what: what:
 
Kwahiyp"father superior, post: 15284384, member: 343883"]Hakumzuia, bali walipitiwa na usingizi[/QUOTE]
Kwahiyo unataka nini?
So jamaa anachelewa job kisa analala na demu?
 
Back
Top Bottom