Kwa wanaozikumbuka nyimbo za NUTA

Kwa wanaozikumbuka nyimbo za NUTA

Mtoboasiri

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2009
Posts
5,100
Reaction score
1,955
"Na sasa naondokaaa, nakwenda zangu, katika kijiji mwenzenu, cha ujamaaa. Nimechoka sasa jamani, na mambo ya mjini.
Nakwenda, ndugu zangu wamenieleza niende katika kijiji cha ujamaaa.

Nakwenda, nikajiunge na wenzangu nipate mahitaji yangu na taabu iniondokee."
 
Mwenye rekodi hii na zile Msondo namba moja na mbili ani PM tafadhali tufanye dili
 
Naomba mwenye albam zote za Komando Hamza Kalala zenye vibao kama
1. "Nimekusamehe ila sitokusahau..."
2. "Tulizaliwa wote, kijiji kimoja..."
3. "Husseni ee wegudina waja wandeka kumikonongo, salam sana wainyonga mpaka gugu oo sagambe..."
4. "toka lini ngoma ya watoto nayo ikakesha..."
5...
6...
7...
jamani nimesahau majina ya vibao hivyo ndo maana nimeweka kwa kutumia baadhi ya mistari.
 
nakucha nakubulagwa maganiko, hamza kalala nalila masomanda eeh.
 
nimekusamehe lakini sitokusahau
kwenye dhiki na faraja tuko tuko wote
uliniacha nateseka peke yangu
pasipo msaada wowote mama ee
 
nakucha nakubulagwa maganiko, hamza kalala nalila masomanda eeh.

Nalihaya kwiza nassa, aliyo naliduma, nalidumila kunguno...,
ing'ombe jamala masundo, huko uliko ni mbali oh mama esta, nakung'wila ki nalila masumanda...

Haka kawimbo hua kananikumbusha nyumbani enzi za 90 na.
 
Nyimbo za TANU au NUTA?
eeeeee TANU yajenga nchiiiiiiii............
 
Nyimbo za TANU au NUTA?
eeeeee TANU yajenga nchiiiiiiii............

Dogo, NUTA i.e National Union of Trade Association (Msondo Ngoma), ikawa JUWATA (Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania) baada OTTU Jazz Band!
 
Nyimbo za TANU au NUTA?
eeeeee TANU yajenga nchiiiiiiii............

B52 !
Huu uzi , kwako maji ya shingo! Sijui nikwambie ukae pembeni labda, vya mbegu ama ma'handsome wa zamani tucheze nao.
Mleta mada hakika umenikunaje! Kuyakumbushia mambo ya Nuta ?
Hebu nikuchape na hii kwanza :
> Lakiini ahadi zako zoote za uongo,
Kusudi lako kupenda Daada kunikomoa,
Punguza chenga zako ooh,
za danadana, umekwisha nidanganya saana dadaa,
na kwa hiyo dada oohoo,
ninakunya unayoyafanya dadaa,
hayana maana.
NA HII
> Juhudi walizofanya hao wapigania uhuru zimewafanya kujitoa katika mikono ya wakoloni ,
na sasa Msumbiji ni huru,
vivaaa !
Vivaaa Msumbijii
vivaaa Frelimooo!
 
Dogo, NUTA i.e National Union of Trade Association (Msondo Ngoma), ikawa JUWATA (Jumuiya ya Wafanyakazi Tanzania) baada OTTU Jazz Band!
Dah siunajua sisi mambo mengi tumeyakuta ukubwani?
Ila akina Juwata nawakumbuka ila NUTA mgogoro aisee
 
B52 !
Huu uzi , kwako maji ya shingo! Sijui nikwambie ukae pembeni labda, vya mbegu ama ma'handsome wa zamani tucheze nao.
Mleta mada hakika umenikunaje! Kuyakumbushia mambo ya Nuta ?
Hebu nikuchape na hii kwanza :
> Lakiini ahadi zako zoote za uongo,
Kusudi lako kupenda Daada kunikomoa,
Punguza chenga zako ooh,
za danadana, umekwisha nidanganya saana dadaa,
na kwa hiyo dada oohoo,
ninakunya unayoyafanya dadaa,
hayana maana.
NA HII
> Juhudi walizofanya hao wapigania uhuru zimewafanya kujitoa katika mikono ya wakoloni ,
na sasa Msumbiji ni huru,
vivaaa !
Vivaaa Msumbijii
vivaaa Frelimooo!
Hahahaaaa
Nimekukubali aisee....ila nina wasiwasi umezijulia pale Villa Park na Enzi hizo....
Kama ni enzi hizo tunakunayang'anya Husny kwa kuwa atakuwa amepoteza haki yake ya msingi ya kuwa na rika wake....
Lol
Chagua moja
 
Nimezijulia Amana mkuu!
Abt Husny tumuachie afunguke mwenyewe!
Bt remembar "Ya kale dhahabu!"
 
Ikiwa kama hunitaki kaka bora unambie mapema
wajua maisha ya siku hizi ya kujitegemea kaka lazima uelewe kaka
unayonisema kwa watu sio jambo la busara
wanawake wako wengi wazuri sanaa kupindukia
u sifikiri ninakukataa mimi ni wako wa daima
uyadharau yale wanayosema shaka ondoa ninakwambia
ubora wa mtu ni tabia hakika uzuri si shani.
 
Mama alivyomtendea babaa ni vibaya sanaaa
mama leo nieleze ni yupi baba alie nizaa
kama mimi ni mtoto asie na baba nifahamishe
majirani walinieleza baba yangu yupo hai
sasa ni miaka 13 sijamuona baba yangu
heri unipeleke kwetu mama nyumbani kwa baba yangu
eeemama eeh mamaeeh nipelekee kwa baba
visa ulivyomtendea baba yangu kwa kweli sikuridhika
hata matendo uliyoyatenda mbele ya mungu huna sheria
heri nile mapumba na kauzu bora nikiwa kwa baba yangu.Wimbo unaitwa nipeleke kwa baba.
 
Dah siunajua sisi mambo mengi tumeyakuta ukubwani?
Ila akina Juwata nawakumbuka ila NUTA mgogoro aisee

Dogo, NUTA ndio Juwata,Ottu,Msondo Ngoma Baba ya Muziki Discipline Fair Play,Ngoma ya Wakubwa na Ngoma kubwa kuliko zote. Na hii Ngoma kubwa kuliko zote imekuja baada ya Sikinde Ngoma ya Ukae kujiita kuwa wao Ngoma kubwa,sasa sisi Msondo tukawaambia kuwa sisi ndio Ngoma Kubwa kuliko zote.
 
kuna wimbo nautafuta uliimbwa maneno yake ni haya,
kampataaa mvulana mwingine yeyeee mwenye gari kubwa sana mtumba kamkataa kwa kuwa ni mshona viatu, mwenye wimbo huu naomba anitumie kwa whatsapp 0622418772
 
jamani naomba mwenye wimbo wa sara wacha majivuno uliopigwa na Urafiki jazz band aweke, nitashukuru aniwhatsapp kwa namba hii 0622418772
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom