Kwa wanandoa tu: Hivi mwanaume ( baba wa familia hula chakula cha siku anachokipenda yeye mwenyewe au anacho/ atakacho kitaka mke wake?

PAZIA 3

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,074
1,857
Bila shaka title inajieleza,

Najua wanaume wengi ni watafutaji, mara nyingi warudipo nyumbani hukuta chakula tayari kimekwisha kuandaliwa na msimamizi mkuu ni mama ( mke).

Swali, je, nikweli huwa mwanaume unakula chakula unachokitamani kwa siku hiyo? Mara nyingi akina mama hata Kama anashughuri zake, inapokuja swala la kununua chakula au mboga, hujiwadhia yeye zaidi na kununua.

Na usiposhukuru kwa kusema chakula cha leo ni kitamu ni habari nyingine, mh🤣🤣🤣🤣🤣 wamama muwe mnatushirikisha kila muandaapo chakula
 
Haya mambo ya kupeana zamu za kuamua sijui leo tule nini ni ya ushuani huko kuna siku ilipoisha zamu ya wazazi kuamua chakula ikaja zamu ya mtoto kuamua chakula si akachagua ubuyu. Kama ujuavyo ushuani Junior akisema haipingwi na yupo sahihi siku zote.

Mi nadhani kama uchumi uko vizuri mnapanga ratiba kwa pamoja.
 
Back
Top Bottom