kwa WanaCHADEMA na wapenda Haki wote
Tangu sakata la kuvuliwa Ubunge kwa Mu Nasari lianze nilifikiri kukaa kimya kwanza,baada ya kimya kirefu naomba nieleze machache ninayofahamu ili kuweka rekodi sawa
Mosi.Mh Nasari anakiri kuwa hajakosa vikao vitatu kama Spika aliyodai.Anasema kikao cha Septemba 2018 alihudhuria,mkutano wa Novemba 2018 alishiriki vikao vya kamati na Januari 2019 aliandika barua akatuma kwa njia ya Email akiwa USA,tafsiri yake barua ilihusu mkutano wa Januari 2019. Ushahidi wa kushiriki vikao vya Septemba na Novemba upo na utawasilishwa mahakamani
Pili.Bahati mbaya sana kwa wanaCHADEMA kumwamini Spika Ndugai ambaye hastahili kuaminiwa kwa lolote.Spika Ndugai ndie spika aliyeharibu na kushusha hadhi na heshima yake bunge kuliko Spika wote katika Historia ya Bunge letu,Hivi Spika Ndugai ambaye bila aibu amelifanya bunge kuwa TAWI la serikali anawezaje kuaminiwa?
Hivi spika ambaye anatangaza hadharani kuwa hajui aliko Mh Tundu Lisu anawezaje kuaminiwa?
Why tusiamini kuwa sakata hili la Mh Nasari lina jambo kubwa la siri nyuma yake?
Inawezekana kuna jambo linatarajiwa kufanywa na hili la Mh Nasari ni kiini macho tu
Ndugu zangu wapiganaji katika msitari wa mbele wa mapambano,hili ni shambulio dhidi ya mmoja wetu,sharti tuamke tupigane upande wa haki.Ni hatari mno kushambuliani sisi kwa sisi,wajibu wetu ni kuungana na kushikamana dhidi yake maadui wa Haki na Demokrasia
Wakati huu ambao Mh Nasari anapigania haki yake na haki yao wapigakura wake Mahakamani ni wakati wa kushikamana sana,tusimpe adui nafasi
Binafsi hata Spika angekuwa sahihi kiasi gani siwezi kumwamini wala kuwa upande wake.Inatosha kabisa aliyomfanyia Mh Lisu,na wabunge wengine wa Upinzani
Spika anapaswa kupuuzwa katika hili la Mh Nasari,hapaswi kupewa hata chembe ya imani
By Nanyaro