Kwa WANACHADEMA na Wapenda Haki wote

Kwa WANACHADEMA na Wapenda Haki wote

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2011
Posts
1,237
Reaction score
1,828
kwa WanaCHADEMA na wapenda Haki wote

Tangu sakata la kuvuliwa Ubunge kwa Nasari lianze nilifikiri kukaa kimya kwanza,baada ya kimya kirefu naomba nieleze machache ninayofahamu ili kuweka rekodi sawa

Mosi. Nassari anakiri kuwa hajakosa vikao vitatu kama Spika aliyodai. Anasema kikao cha Septemba 2018 alihudhuria,mkutano wa Novemba 2018 alishiriki vikao vya kamati na Januari 2019 aliandika barua akatuma kwa njia ya Email akiwa USA,tafsiri yake barua ilihusu mkutano wa Januari 2019. Ushahidi wa kushiriki vikao vya Septemba na Novemba upo na utawasilishwa mahakamani

Pili. Bahati mbaya sana kwa wanaCHADEMA kumwamini Spika Ndugai ambaye hastahili kuaminiwa kwa lolote.Spika Ndugai ndie spika aliyeharibu na kushusha hadhi na heshima yake bunge kuliko Spika wote katika Historia ya Bunge letu. Hivi Spika Ndugai ambaye bila aibu amelifanya bunge kuwa TAWI la Serikali anawezaje kuaminiwa?

Hivi spika ambaye anatangaza hadharani kuwa hajui aliko Mh Tundu Lissu anawezaje kuaminiwa?
Why tusiamini kuwa sakata hili la Mh Nasari lina jambo kubwa la siri nyuma yake?

Inawezekana kuna jambo linatarajiwa kufanywa na hili la Mh Nasari ni kiini macho tu.

Ndugu zangu wapiganaji katika mstari wa mbele wa mapambano,hili ni shambulio dhidi ya mmoja wetu,sharti tuamke tupigane upande wa haki.

Ni hatari mno kushambuliani sisi kwa sisi,wajibu wetu ni kuungana na kushikamana dhidi yake maadui wa Haki na Demokrasia

Wakati huu ambao Mh Nasari anapigania haki yake na haki yao wapiga kura wake Mahakamani ni wakati wa kushikamana sana,tusimpe adui nafasi

Binafsi hata Spika angekuwa sahihi kiasi gani siwezi kumwamini wala kuwa upande wake.Inatosha kabisa aliyomfanyia Mh Lissu,na wabunge wengine wa Upinzani

Spika anapaswa kupuuzwa katika hili la Mh Nassari,hapaswi kupewa hata chembe ya imani

By Nanyaro
 
chadema ni wepesi sana kutangaza kufungua kesi halafu wanapotea
Walitangaza kuwa mawakili wao sita,watamfungulia kesi wallace karia,mpaka leo kimya
Huyo Nassari hakua na haja kuita press,angewahi tu mahakamani
cha kufurahisha hata uongozi wa juu wa chadema unaoneka ulikua hauna taarifa za utoro wa mbunge wao,mpaka kufikia sultani anamwambia Nassari atoe tamko
 
Nasari hata jimboni kwake hua haonekani matokeo yake amemfanya mkuu wa Wilaya kuwa ndiye mbunge.

Nasari anaonekana jimboni akiwa na vimisaada anavyoomba huko Marekani ili kuwavuta wapiga kura ,anasahau kuwa kama mbunge kazi yake kubwa sio kutoa misaada Bali kusikiliza kero za wananchi na kuzifikisha serikalini au bungeni .

Sasa amekwaa kisiki na Gongo la Nduga.

Huyu dogo ni msanii sio wa kuamini hata kidogo. Apumzishwe tu jimbo kirudi CCM. Kama ameuza jimbo basi arudi Uraiani mana hata CCM hawawezi kumpa nafasi ya kuwakilisha wananchi mana hataki na ameshindwa.
Asubiri uteuzi wa ukuu wa Wilaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi sidhani kama kuna mwanamabadiliko yeyote anaye mwamini huyo Ndugai isipokuwa baadhi ya wanamabadiliko na wapenda haki hawakulizishwa na maelezo ya Nasari.

Nasari either kwa mshituko wa jambo lenyewe naona kama maelezo yake hajitoshelezi. ila wanamabaldiliko wote wako nyuma yake kama ataendelea kupigania haki yake kwa nguvu zaidi kwanza aende mahakama kuzuia maamuzi ya bunge. Pili aitishe mkutano aongee na wapiga kura wake.
 
"Hivi spika ambaye anatangaza hadharani kuwa hajui aliko Mh Tundu Lisu anawezaje kuaminiwa? "
Spika anaona mitandaoni kama wewe ila hakuna taarifa official za alipo na maendeleo ya matibabu ya Lissu....
Ndio sababu anasema HAJUI..
 
Pili.Bahati mbaya sana kwa wanaCHADEMA kumwamini Spika Ndugai

Hivi kuna mwanachama au shabiki wa CHADEMA anayemwamini Ndungai?
Nitastaajabu sana kusikia kuwa wapo watu ndani ya CHADEMA ambao bado wanamwamini kwa lolote. Hii itakuwa ni kama aina ya ndoa mbaya, lakini muolewa pamoja na mateso afanyiwayo anaona ni bora abaki!

Mosi.Mh Nasari anakiri kuwa hajakosa vikao vitatu kama Spika aliyodai.

Kama ushahidi huu upo, utamsaidia sana.

Lakini pamoja na haya yote uliyoyaweka hapa, huwezi kuondoa mchanganyiko/sintojua aliyoisababisha Nassari mwenyewe.

Hata kabla ya furumusha hii, Nassari alijiweka katika hali ya mashaka kutokana na aidha aliyofanya, au ambayo hakuyafanya.

Hata kama alihudhuria baadhi ya vikao kwa muda mfupi, sehemu kubwa aliyokosa kuonekana bungeni bila ya maelezo ni mchango mahsusi wanaoutumia mahasimu wa CHADEMA

Taarifa/barua inayozungumziwa, nayo maelezo yake ni ya kiajabu, hasa kwa mtu ambaye ni mwakilishi mwenye ujuzi na uzoefu wa kujieleza vizuri.

Je, Chama chake kilikuwa na taarifa zote za mambo aliyokuwa akihusika nayo wakati anakosa vikao vya bunge?

Mnapojua mnawindwa msambaratishwe, halafu nyinyi wenyewe mnatoa mwanya chee kabisa wa kuwavuruga, watu wanaowaangalia na kuwasikitikia watasema nini katika hali kama hiyo.

Ndugai katumia tu udhaifu huo kuendeleza njia za kuwavuruga. Na mbaya zaidi, sina hakika kama kujieleza kwa Nassari alikofanya kunaondoa shaka zote kwamba kanunuliwa!

Huwezi kujiweka kamba ya kukunyonga mwenyewe shingoni huku adui yako yupo hapo akikutazama tu. Ni dhahiri atachukua mwanya huo kukunyonga kirahisi.

Sasa sijui kama hili liwe funzo kwa CHADEMA, maanake naona ni wagumu sana wa kujifunza. Matendo yote mnayofanyiwa bado hamuwezi kujifunza kuepuka mitego mibovu namna hii?
 
kwa WanaCHADEMA na wapenda Haki wote

Tangu sakata la kuvuliwa Ubunge kwa Mu Nasari lianze nilifikiri kukaa kimya kwanza,baada ya kimya kirefu naomba nieleze machache ninayofahamu ili kuweka rekodi sawa
Mosi.Mh Nasari anakiri kuwa hajakosa vikao vitatu kama Spika aliyodai.Anasema kikao cha Septemba 2018 alihudhuria,mkutano wa Novemba 2018 alishiriki vikao vya kamati na Januari 2019 aliandika barua akatuma kwa njia ya Email akiwa USA,tafsiri yake barua ilihusu mkutano wa Januari 2019. Ushahidi wa kushiriki vikao vya Septemba na Novemba upo na utawasilishwa mahakamani

Pili.Bahati mbaya sana kwa wanaCHADEMA kumwamini Spika Ndugai ambaye hastahili kuaminiwa kwa lolote.Spika Ndugai ndie spika aliyeharibu na kushusha hadhi na heshima yake bunge kuliko Spika wote katika Historia ya Bunge letu,Hivi Spika Ndugai ambaye bila aibu amelifanya bunge kuwa TAWI la serikali anawezaje kuaminiwa?
Hivi spika ambaye anatangaza hadharani kuwa hajui aliko Mh Tundu Lisu anawezaje kuaminiwa?
Why tusiamini kuwa sakata hili la Mh Nasari lina jambo kubwa la siri nyuma yake?
Inawezekana kuna jambo linatarajiwa kufanywa na hili la Mh Nasari ni kiini macho tu
Ndugu zangu wapiganaji katika msitari wa mbele wa mapambano,hili ni shambulio dhidi ya mmoja wetu,sharti tuamke tupigane upande wa haki.Ni hatari mno kushambuliani sisi kwa sisi,wajibu wetu ni kuungana na kushikamana dhidi yake maadui wa Haki na Demokrasia
Wakati huu ambao Mh Nasari anapigania haki yake na haki yao wapigakura wake Mahakamani ni wakati wa kushikamana sana,tusimpe adui nafasi

Binafsi hata Spika angekuwa sahihi kiasi gani siwezi kumwamini wala kuwa upande wake.Inatosha kabisa aliyomfanyia Mh Lisu,na wabunge wengine wa Upinzani

Spika anapaswa kupuuzwa katika hili la Mh Nasari,hapaswi kupewa hata chembe ya imani

By Nanyaro
Narenduuu...ndwakoruuuu...Nassari hata angekuwa alikuwa Dodoma hiyo September kwa jinsi nimjuavyo angetoa risiti ya lodge aliyoipata.Ngoja aendelee kuwaburuza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Hivi spika ambaye anatangaza hadharani kuwa hajui aliko Mh Tundu Lisu anawezaje kuaminiwa? "
Spika anaona mitandaoni kama wewe ila hakuna taarifa official za alipo na maendeleo ya matibabu ya Lissu....
Ndio sababu anasema HAJUI..

Ndugai alikuwepo siku yako kwanza pale Hospitali ya Dodoma,alishiriki kikao cha kuratibu safari ya Nairobi ya Mh Lisu.Baada ya kupigwa mkwara anamkana
 
Ndugai alikuwepo siku yako kwanza pale Hospitali ya Dodoma,alishiriki kikao cha kuratibu safari ya Nairobi ya Mh Lisu.Baada ya kupigwa mkwara anamkana
Boss sio kumkana.... not official...
Alipokwenda USA wakadhani amepona.. Lissu akajibu nyinyi sio madaktari wangu na hamjui kinachoendelea... meaning?
hakuna connection kati ya ofisi ya bunge na anakotibiwa..... Then its unofficial
Yes ana bad feeling na serikali kwakuwa hawalimpii tiba na labda woga wa usalama wake...then ficha mboga tunahamisha ugali.
Its a game na labda kukomoana in a way
 
...
Binafsi hata Spika angekuwa sahihi kiasi gani siwezi kumwamini wala kuwa upande wake.Inatosha kabisa aliyomfanyia Mh Lisu,na wabunge wengine wa Upinzani

Spika anapaswa kupuuzwa katika hili la Mh Nasari,hapaswi kupewa hata chembe ya imani

By Nanyaro
Ujumbe wako ni kwa wanachadema na wapenda haki wote. Unawataka wapenda haki wampuuze Ndugai hata kama anachosema ni kweli, have you lost your sanity?!
 
Tabia ya kutengeneza vimwanya vya CCM kuwavuruga ama kuwanunua alafu baadaye mnakuja kutuigizia machozi yenu mashavuni ili tuyafute MUACHEEE wapiga kura hawapo JF na mjini tu vijijini wamejaa.

Jengeni Ngome imara ya upinzani itumieni ruzuku ya Chama vizuri.

Wanawayumbisha na vimatukio nanyi mnayumba futeni neno Nyumbu

Hamkujipanga Hamjajipanga je hamtajipanga?

Namkumbuka tu bro Pascal Mayalla na Uzi wake.

Ndugai hata akisema huu ni mchana toka nje uka angalie jua lipo?
Sijapata kuona mtu bogus kama huyo ndani ya bunge tokea uhuru

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tabia ya kutengeneza vimwanya vya CCM kuwavuruga ama kuwanunua alafu baadaye mnakuja kutuigizia machozi yenu mashavuni ili tuyafute MUACHEEE wapiga kura hawapo JF na mjini tu vijijini wamejaa.

Jengeni Ngome imara ya upinzani itumieni ruzuku ya Chama vizuri.

Wanawayumbisha na vimatukio nanyi mnayumba futeni neno Nyumbu

Hamkujipanga Hamjajipanga je hamtajipanga?

Namkumbuka tu bro Pascal Mayalla na Uzi wake.

Ndugai hata akisema huu ni mchana toka nje uka angalie jua lipo?
Sijapata kuona mtu bogus kama huyo ndani ya bunge tokea uhuru

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom