Demi
JF-Expert Member
- Nov 22, 2016
- 42,825
- 95,676
Ndugai anafahamu Lissu yupo NairobiNdugai alikuwepo siku yako kwanza pale Hospitali ya Dodoma,alishiriki kikao cha kuratibu safari ya Nairobi ya Mh Lisu.Baada ya kupigwa mkwara anamkana
Ndugai anafahamu Lissu yupo NairobiNdugai alikuwepo siku yako kwanza pale Hospitali ya Dodoma,alishiriki kikao cha kuratibu safari ya Nairobi ya Mh Lisu.Baada ya kupigwa mkwara anamkana
Nassari kawadharau sana ChademaNdugai hata akisema huu ni mchana toka nje uka angalie jua lipo?
Sijapata kuona mtu bogus kama huyo ndani ya bunge tokea uhuru
Sent using Jamii Forums mobile app
Hadi hapo Mhe. Nasari atakapofungua kesi, ikasikilizwa, akashinda na kurejea Bungeni ndipo tutakapokuwa na uwezo wa kujadili ubaya wa Mhe. Job Ndugai hasa kwa hili.kwa WanaCHADEMA na wapenda Haki wote
Tangu sakata la kuvuliwa Ubunge kwa Nasari lianze nilifikiri kukaa kimya kwanza,baada ya kimya kirefu naomba nieleze machache ninayofahamu ili kuweka rekodi sawa
Mosi. Nassari anakiri kuwa hajakosa vikao vitatu kama Spika aliyodai. Anasema kikao cha Septemba 2018 alihudhuria,mkutano wa Novemba 2018 alishiriki vikao vya kamati na Januari 2019 aliandika barua akatuma kwa njia ya Email akiwa USA,tafsiri yake barua ilihusu mkutano wa Januari 2019. Ushahidi wa kushiriki vikao vya Septemba na Novemba upo na utawasilishwa mahakamani
Pili. Bahati mbaya sana kwa wanaCHADEMA kumwamini Spika Ndugai ambaye hastahili kuaminiwa kwa lolote.Spika Ndugai ndie spika aliyeharibu na kushusha hadhi na heshima yake bunge kuliko Spika wote katika Historia ya Bunge letu. Hivi Spika Ndugai ambaye bila aibu amelifanya bunge kuwa TAWI la Serikali anawezaje kuaminiwa?
Hivi spika ambaye anatangaza hadharani kuwa hajui aliko Mh Tundu Lissu anawezaje kuaminiwa?
Why tusiamini kuwa sakata hili la Mh Nasari lina jambo kubwa la siri nyuma yake?
Inawezekana kuna jambo linatarajiwa kufanywa na hili la Mh Nasari ni kiini macho tu.
Ndugu zangu wapiganaji katika mstari wa mbele wa mapambano,hili ni shambulio dhidi ya mmoja wetu,sharti tuamke tupigane upande wa haki.
Ni hatari mno kushambuliani sisi kwa sisi,wajibu wetu ni kuungana na kushikamana dhidi yake maadui wa Haki na Demokrasia
Wakati huu ambao Mh Nasari anapigania haki yake na haki yao wapiga kura wake Mahakamani ni wakati wa kushikamana sana,tusimpe adui nafasi
Binafsi hata Spika angekuwa sahihi kiasi gani siwezi kumwamini wala kuwa upande wake.Inatosha kabisa aliyomfanyia Mh Lissu,na wabunge wengine wa Upinzani
Spika anapaswa kupuuzwa katika hili la Mh Nassari,hapaswi kupewa hata chembe ya imani
By Nanyaro
Kinacho ni furahisha sasa ni kwamba, kete ya umri katika uchaguzi imefungwa, tutaanza kuangalia matendo ya mtu zaidi kuliko umri wake.Nanyaro pamoja na kwamba nyie ni viongozi wetu msidhani hatuna ufahamu wowote. Tabia zenu kwa sasa zimetuacha na wakati mgumu sisi wanachama na washabiki wa cdm kuanzia kumchukua Lowassa mpaka huu utoto wa Nassari.
Sio Ndugai tu, hatumuamini hata Magufuli na jaji mkuu na mwanaccm yoyote, lakini kwa hili la Nassari mmetuangusha sana. Kwa taarifa yako Nassari kachukua hela ya ccm na hatakaa aende mahakamani. Tumefedheheka sana ukizingatia jinsi tulivyohatarisha maisha yetu kulinda kura za wapinzani kisha mnaleta huu ujinga.
Halafu nje ya mada, sasa ni muda wa Mbowe kustaafu, tena aondoke na huo mzigo wake unaoitwa Mashinji.
Nasari hata jimboni kwake hua haonekani matokeo yake amemfanya mkuu wa Wilaya kuwa ndiye mbunge.
Nasari anaonekana jimboni akiwa na vimisaada anavyoomba huko Marekani ili kuwavuta wapiga kura ,anasahau kuwa kama mbunge kazi yake kubwa sio kutoa misaada Bali kusikiliza kero za wananchi na kuzifikisha serikalini au bungeni .
Sasa amekwaa kisiki na Gongo la Nduga.
Huyu dogo ni msanii sio wa kuamini hata kidogo. Apumzishwe tu jimbo kirudi CCM. Kama ameuza jimbo basi arudi Uraiani mana hata CCM hawawezi kumpa nafasi ya kuwakilisha wananchi mana hataki na ameshindwa.
Asubiri uteuzi wa ukuu wa Wilaya.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo ndio wapinzani wanakosea sana.Simwelewi 1000 digits anaposema kuwa Jerry Muro ndo amekuwa Mbunge. Kwa taarifa ya 1000 digit na wenzie waliolewa mvinyo wa CCM, kazi kubwa ya mbunge ni kuwawakilisha watu wake bungeni kwa:
a) Kutunga sheria
b) Kupitisha bajeti ya serikali ambayo kutekelezwa kwake (na serikali) kutaleta maendeleo
c) Kuisimamia serikali.
Mambo yote haya yanafanywa na mbunge akiwa mjengoni. Swali kwa 1000 digits: Ni lini Jerry Muro ameingia bungeni kufanya hayo niliyoyataja kwa niaba ya wati wa Meru Mashariki?. Jerry Muro anafanya kazi yake kama kiiongozi wa serikali; kazi ambayo angeifanya tu hata kama mbunge yupo muda wote jimboni na bungeni. Kwa kufanya hivyo hakumfanyi awe mbunge.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]Hivi akili huwa mnampa nani awashikie? Hakika unafiki utawahukumu siku ya mwisho