Nilipata bahati ya kuishi Iringa katika miaka mingi tofauti na hizi hapa chini ni sehemu nilizo wahi kuishi na aina ya maisha niliyoyafurahia 2003 - niliishi Iringa Don Bosco nikiwa Mwalimu wa kujitolea shule ya Mawelewele Secondary. Yalikuwa ni maisha mazuri mno katika nyumba ya kupanga ya bibi mmoja na hapo nilifahamiama na dereva wa daladala aliyekuwa jirani yangu na boss wake ambae siku hzi "tigo" hapo iringa. tiGo ni wale wana usalama wanaotumia boda boda 2006 - nilirudi Iringa baada ya masomo nje ya nchi nikiwa kama muajiriwa nikaishi Gangilonga na Wilolesi kwa kipindi kirefu cha miaka 2 hapo nikatengeneza network kubwa ya marafiki na biashara. Nilifanikiwa kumilliki Bar na vyombo vya usafiri wa biashara hapo Iringa. nilifurahia maisha ya kwenda Twisters, Shooters na mawindo Tumaini University , Mkwawa na Ruco pia2007 - nilihamia Njombe, nikawa naishi Mgendela kabla ya kuhamia Nazareth njombe. nilipata marafiki wengi wafanya biashara na wakulima hali iliyofanya nikajiingiza kwenye kilimo cha Mahindi Ludewa - Kata ya Lugarawa karibu na Mission na pia kulima viazi Bulongwa Makete. Kukaa kwangu Ludewa kulinipa marafiki wengi Mkongobaki, Mlangali, Lupande na Milo kote huko nimewekeza. Ukiachilia mbali Makete maeno ya Bulongwa, nilifurahia sana kukaa Makete mjini na nilikuwa mteja maarufu wa mgahawa wa Mama Jimmy na niliishi Hotel ya Hill Park kwa muda wote huoMwaka 2009 - niliondoka Iringa na Tanzania kwa ujumla, nayakumbuka sana Maisha yangu ya ujana nikiwa Iringa , Njombe, Makete na Ludewa. I will always cherish those good old times I spent there, inshallah nitarudi tena hali ikiimarikapomerini secondary 2003-2004 nilihamia level jumapili tunakwenda kanisani mabandani makla kitu kinaitwa waki(wali kiepe unachanganywa) full baridi basi lipo moja tu kwacha
Duh,ruaha pia,2001 olevel
Mkwawa..makanyagio kwa mzee chuwa...
kwa nelkon (RIP), bungeni.
Mkwawa High School 2003/2004 kabla haijabadilishwa kuwa chuo!To be honest hakuna shule nzuri kimiundombinu km ilivyokuwa mkwawa kwa shule zet za serekali!Maisha yalikuwa pouwa sana unakutana na watu kutoka kila pembe ya Tz!
kwa nelkon (RIP), bungeni.
Hahaa dogo! Wakati huo inaitwa Ruaha technical sec school frm 1 1989 to 1992 ile shule tumeijenga sisi kwa kubeba tofali pale na kuchimba msingi kwa kuwa kulikuwa hakuna fimbo ndo adhabu zenyewe. Kuna kitu ilikuwa inaitwa self reliance kila siku kuna darasa linabaki kufanya hiyo elimu ya kujitegemea, hapo kazi ni kwenu mtabeba tofali mpaka mshangae toka kule chini kabisa mtoni ruaha. Kila siku asubuhi pale assembly kuna sala inasomwa maana ile shule ipo chini ya wa Bahai. Nakumbuk
Hahaa dogo! Wakati huo inaitwa Ruaha technical sec school frm 1 1989 to 1992 ile shule tumeijenga sisi kwa kubeba tofali pale na kuchimba msingi kwa kuwa kulikuwa hakuna fimbo ndo adhabu zenyewe. Kuna kitu ilikuwa inaitwa self reliance kila siku kuna darasa linabaki kufanya hiyo elimu ya kujitegemea, hapo kazi ni kwenu mtabeba tofali mpaka mshangae toka kule chini kabisa mtoni ruaha. Kila siku asubuhi pale assembly kuna sala inasomwa maana ile shule ipo chini