Kwa waliowahi kuishi Iringa, comment hapa tafadhali

nakumbuka mwaka 2003-2004 sekondari mkwawa,ukiwa na 500 siku nzima uingii mesini,unaenda sehemu inaitwa makanyagio.100 asubuhi unapata chai kwa maandazi matatu,mchana 200 wali kwa maharage,jioni 200 tena unapata wali kwa maharage.

Unakimbia wali maharagwe ya shule ukafuate ya mtaani?kweli we kijana? Au kwa kuwa ya shule yalikuwa hayaungwi?
 
Advance Tosamaganga,enzi hizo. Ulanzi ulpatikama Ipamba,pia tulikwenda huko Ipamba kutafuta mende kwa ajili ya disection.
Vilevile vyura kwa ajili ya disection tuliwafuata Msiwasi.
Mabansi tuliyapata kwa masista au kwa mama mingoyo.
 
Mimi nimesoma ruaha university college(2009/2012),nilipanga chumba katika maeneo mawili tofauti,mara ya kwanza nilipanga maeneo ya ngome kihesa mwaka 2009/10 na miaka iliyobakia niliishi maeneo jirani na shule ya sekondari mwembetogwa.wakati nikiwa mwembetogwa nimekuwa nikipata chakula katika mgahawa wa mzee sadiq kwa bei poa jirani na stendi kuu ya mabasi.
 
nilisoma pale living stone int school (lisco) njombe .karibu na kibena..nakumbuka sana yale malori yanayofanana na matrekta yanayobeba magogo yakipita pale, kwa aliesoma pale ani pm, nimemiss sana old school stories including ile ishu ya vibwengo
 
Advance Tosamaganga,enzi hizo. Ulanzi ulpatikama Ipamba,pia tulikwenda huko Ipamba kutafuta mende kwa ajili ya disection.
Vilevile vyura kwa ajili ya disection tuliwafuata Msiwasi.
Mabansi tuliyapata kwa masista au kwa mama mingoyo.

Mkuu kwenye nyekundu yanaitwa MABANZI
na yule mama ni MAMA MINGOI
 
Mkwawa 2000-2002 kuoga wiki kwa wiki, makanyagio kula mabanzi( mabanzi ni mandazi makubwa kama kichwa cha mtoto) mesi jtano mchana hapatoshi sababu ya ugali nyama, hatari zaidi ni jmosi mchana sababu ya wali. msimu wa juisi( ulanzi) maisha mteremko......dada kaenda nayo masine....namis sana Iringa
 
pomerini secondary 2003-2004 nilihamia level jumapili tunakwenda kanisani mabandani makla kitu kinaitwa waki(wali kiepe unachanganywa) full baridi basi lipo moja tu kwacha
 
Don bosco seminary banaa, baridi ndo ki2 ambacho sintakisahau

Don Bosco Seminary Mwaka gani Mkuu nakumbuka miaka hiyo Waseminary pale Mafinga walikuwa wakitufundisha mafundisho kila Jumapili ukiniambia ni mwaka gani nikiwakumbuka nitakutajia.

 
Back
Top Bottom