Kwa waliooa tu: Mke kutime simu na kuikagua

Kwa waliooa tu: Mke kutime simu na kuikagua

Well tatizo hapo ni kule kuwatusi watu wako kwenye sim ila yeye kushika sim na kukuhoji juu ya ufanyayo kwa sim yako ni powa sana anakujali / wivu raaa sana

Mwambie aache kutukana watu kwa sim ila usimnyime watu wanatafta kama huyo
 
Ukiona mwanamke anakushuku hata kwa vitu vidogo na huvifanyi kabisa wala kuashiria kuvifanya, hebu mchunguze yeye alivyo sasa au historia ya maisha yake ya awali, wengine wanaogopa vivuli vyao wenyewe.
 
Hii tabia ya kugombania simu imekuwa kero sasa,na haya yote yametokana na watu kuendekeza michepuko na kuvunja maadili,,,ndoa zimekosa uaminifu na watu hawafurahii ndoa ila wanavumilia tu,,,,,badilikeni mrudieni Mungu
 
jitahidi awe anashinda na simu yako - japo siku mbili kwa wiki
 
Picha niliyopata ni kwamba umeshaanza kumchoka mkeo kimapenzi na mkeo keshashtuka. Kwanini nimeona hivyo...it's because umetuonyesha age gap kati ya wewe na yeye and she is 1 year older than you! Naomba hivyo vimchepuko vyako uvipige chini! Mkeo anaonekana kuwa very desperate about your behaviour!...kwahiyo badilika kaka...inaonekana kabisa mwanzoni alikuwa anakuamini vizuri tu!
Jamani ninaandika kwa ghadhabu sana juu ya hii tabia ya huyu mwanamke, huyu mwanamke huwa anatabia ya kuchukua simu yangu na kupitia message, call zote na baada ya hapo huanza kusaka namba ambazo hupigwa au kupiga sana na kutukana, tumeingia kwenye migogoro sana na amegombana na watu wengi sababu ya simu tu.

Mi sio malaika jamani lakini kwa tabia hii ninaona ndoa ngumu, maana yake sio siri nakwazika sana kwa namna anavyonichimba na kuleta zogo. Nimejitahidi sana kumkemea lakini imeshindikana, haya sio maisha kabisa kwangu na kila akiibua zogo ndo nazidi kumchukia na kuingiwa na mawazo mabaya, mke sina haja naye hata tukitengana ni vizuri nina miaka 30 yeye 31, ndoa ina miaka kumi na tuna mtoto mtoto mmoja.


Naombeni ushauri kwa faida ya huyu mtoto
.
 
Ni kweli Mkuu Kete ngumu maisha yanahitaji interaction,
mfano wiki jana kamtukana dd mmoja katokea kunielewa sana na anazo mbaya anasimamia maduka 2 mazito,
nnlikuwa nimemweka sawa anitumie Laki 5,
lakn huyu mwanamke sijjui alichukua no ake muda gan akamtukana sana na kumtishia mbaya,
huyo dd tushapima na tuko safi maisha yanaendelea
...


Mkuu nadhani tatizo lote liko hapo juu kwenye red, I may be wrong...
 
jamaa una ghadhabu sana......ila elewa Mungu hakutuumba tuishi na migogoro kila uchao....furaha na amani yako viko JUU yako wewe mwenyewe..........bora wewe umeweza kusema hapa, wako wengi wanaugulia kimya kimya..
 
aisee hii kitu inanitesa hadi leo.nilishika simu ya mpenz wangu na ilikuq ndo mara ya kwanza tunakunakutana yaani ndo tulikua tupo peke etu..yaani gafra nikashika simu ake ile nafungua tu kumbe alikua watsaap akichat na best ake wakinizungumzia mim tena si kwa mazuri ila ni kwa mabaya nikilichukia kiukweli na kuivunja hile simu!!..siku ingne nilishika tena hee tobaa!! kumbe anampenz mwengne tena wakiambizana kuwa wamemisiana huku wakiambizana ukija ntakupa mapenz motomoto...niliumia sana na hadi leo naumia..(ila jambo hili la sms za mpenzi mwenywe hajafahamu kama mi nimeona)zinaumiza asiee naumia tu mdogomdgo ila ipo siku ntamwambia ili ajue uupuz anaoufanya nami naujua
 
Huyo mama hana makosa, km simu yako haina ubaya wowote na unajiamini kwanini uchukie?????
Simu km imejaa uchafu lazima uchukie.
Tafakar sana kabla ya kuchukua hatua.
 
aisee hii kitu inanitesa hadi leo.nilishika simu ya mpenz wangu na ilikuq ndo mara ya kwanza tunakunakutana yaani ndo tulikua tupo peke etu..yaani gafra nikashika simu ake ile nafungua tu kumbe alikua watsaap akichat na best ake wakinizungumzia mim tena si kwa mazuri ila ni kwa mabaya nikilichukia kiukweli na kuivunja hile simu!!..siku ingne nilishika tena hee tobaa!! kumbe anampenz mwengne tena wakiambizana kuwa wamemisiana huku wakiambizana ukija ntakupa mapenz motomoto...niliumia sana na hadi leo naumia..(ila jambo hili la sms za mpenzi mwenywe hajafahamu kama mi nimeona)zinaumiza asiee naumia tu mdogomdgo ila ipo siku ntamwambia ili ajue uupuz anaoufanya nami naujua

Umeshapewa "red flag", angalia upya mustakabali wa mahusiano yenu. wanakudiscuss nini na rafiki zake?
 
Mi simu naacha na haichukui hata akiichukua sizuii. Ya kwake mie ndo operator wake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom