Kwa wale waliooa mapema kabisa tupongezane

dimaa

JF-Expert Member
Jul 30, 2016
4,143
5,610
Amani iwe juu yenu,

Mimi binafsi nilioa mapema sana katika harakati za kutuliza michepuko. Nilioa nikiwa kidato cha pili, hadi nafika cha nne tayari nilikua na mtoto mkubwa tu na hadi namaliza elimu yangu ya juu nilikua na watoto wawili. Hili shauri lilitoka kwa wazazi kutokana na wao kua na dini, wakasema mwanetu ili aepuke vishawishi ni kumpatia mwenzake 2 ili atulie, hivyo ikanilazimu nikubali tu kuchukua jiko.

Karibuni sana kwa wale waliochukua majiko (wake) mapema kabisa tupongezane.

By

Mtanashati

Young

Dimaa.
 
inawezekana ulioa ukiwa kidato cha pili swali je ulikuwa na umri gani??? isijekuwa ulikuwa na miaka wa uzee wakti upo kidato cha pili
 
inawezekana ulioa ukiwa kidato cha pili swali je ulikuwa na umri gani??? isijekuwa ulikuwa na miaka wa uzee wakti upo kidato cha pili
Inawezekana mtu yupo kidato cha akawa mzee eeee???
 
Mliowahi kuoa mlidhani wanawake watakwisha. Sasa mmepigwa na butwaa kitaa kuna totoz kali na nyie mmeshajipiga pini na vi bibi vizee! Mtuwache turinge sie ambao tumechelewa kuoa. In the end of the day tunakamata totoz kali zaidi yenu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom