Kwa wale tunaoishi Dar es Salaam tu

Kwa wale tunaoishi Dar es Salaam tu

BIA BORA

Senior Member
Joined
Oct 21, 2013
Posts
144
Reaction score
164
wakuu ebu tukumbushane, wale tuliotokea mikoani na kuhamia dar...je ulikuja dar kwa usafiri gani?? ulifikia kwa nani?? vipi experience yako ndani ya mwezi mmoja?? NIni kilikushangaza sana??

mi nakumbuka nilipokuja mwaka 1990, nilipanda gari ya mizigo kutokea mwanza, tulitumia siku tatu, baada ya kusimama singida na dodoma. nilishangaa sana kuona nyumba karibu zote zina umeme, hata kwa shangazi nilipofikia. balabala ya kawawa na al hassani mwinyi zilikua single road.

JOTO lilinifanya nilale uchi wa mnyama, niliapa sitorudi kijijini mpaka kieleweke..hatimaye kimeeleweka

nipe experience zenu wakuu
 
This is how we learn how to post!
 
Mimi nilikuja miaka ya 2000's na nilikuja kwa ramani, nilielekezwa nikishuka Ubungo toka nje kamata daladala ya Kariakoo, shuka msimbazi ndo nilipokelewa pale na mzee mmoja mbishi wa town wa kitambo sana wa mtaani kwetu. Nakumbuka nilifikia mtaa wa Mzizima. Ktk siku kama 5 za mwanzo nilikuwa nachanganya sana direction, sometimes North napaona South, kesho East napaona West (hii nadhani huwa inawatokea wengi especially unapofika eneo geni)

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Sasa sema kwa mliokuja dar, sio mnaoishi dar. Mimi naishi Dar pia lkn sikuja. My first day ilikuwa Ocean Road Hosp, wajanja wa jiji tulizaliwa pale, madogo zetu wakafuatia Muhimbili kwenye manyau.

Karibuni saridalama
 
Nilikuja Dar Disemba 2006, sitosahau hizo siku baada ya kusafiri kwa basi siku 4 wakati kawaida ni siku 2 kwa wale ndugu zangu wa bukoba.
 
Nilikuja Dar mwaka 2000 January mapema tu baada ya kumaliza kufanya mtihani wa WAZIRI KAPUYA (FORM FOUR KWA WALE MNAOKUMBUKA KILICHOTOKEA)
Nilikuja kwa Fuso ikiwa imebeba ng'ombe (harufu yake sasa ,.......we)
Nilifikia kisutu soko la kuku na kuanza maisha huku nikiwa nalala kwenye mabox ambayo tuliyatumia kutandika balazani kwa mama mmoja pale maeneo ya FIRE
Then niaanza kuuza juice za kufunga na maji ya Pakti ya kampuni za masafi,penguine na baridi muda si mrefu matokeo yakawa yametoka na bahati nzuri nikawa nimefauru kuendelea na shule so nikaenda zangu shule mikoani
 
Sasa sema kwa mliokuja dar, sio mnaoishi dar. Mimi naishi Dar pia lkn sikuja. My first day ilikuwa Ocean Road Hosp, wajanja wa jiji tulizaliwa pale, madogo zetu wakafuatia Muhimbili kwenye manyau.

Karibuni saridalama

nani kakwambia kuzaliwa dar ndo ujanja ????
 
Sasa sema kwa mliokuja dar, sio mnaoishi dar. Mimi naishi Dar pia lkn sikuja. My first day ilikuwa Ocean Road Hosp, wajanja wa jiji tulizaliwa pale, madogo zetu wakafuatia Muhimbili kwenye manyau.

Karibuni saridalama
Siyo ujanja kuzaliwa dar,sawa sisi ni wakuja lkn tumewaacha mbali kimaendeleo.wakuja oyeeeeeeeee!!
 
Huu uzi pelekeni kule FB au kwa yule uncle wamagamba......
 
wakuu ebu tukumbushane, wale tuliotokea mikoani na kuhamia dar...je ulikuja dar kwa usafiri gani?? ulifikia kwa nani?? vipi experience yako ndani ya mwezi mmoja?? NIni kilikushangaza sana??

mi nakumbuka nilipokuja mwaka 1990, nilipanda gari ya mizigo kutokea mwanza, tulitumia siku tatu, baada ya kusimama singida na dodoma. nilishangaa sana kuona nyumba karibu zote zina umeme, hata kwa shangazi nilipofikia. balabala ya kawawa na al hassani mwinyi zilikua single road.

JOTO lilinifanya nilale uchi wa mnyama, niliapa sitorudi kijijini mpaka kieleweke..hatimaye kimeeleweka

nipe experience zenu wakuu

Ulilala uchi wa mnyama? mkuu mitego hiyo na ulielala naye.
 
Sasa sema kwa mliokuja dar, sio mnaoishi dar. Mimi naishi Dar pia lkn sikuja. My first day ilikuwa Ocean Road Hosp, wajanja wa jiji tulizaliwa pale, madogo zetu wakafuatia Muhimbili kwenye manyau.

Karibuni saridalama

Usingetutaja wazaliwa wa muhimbili ningekumind, enzi zile panaitwa Muhimbili Medical (health) Centre. Eti siku hiz4 muhimbili national hospital, daah raha sana! Hata paka wazoefu wamepungua sasa
 
Back
Top Bottom