Hivi punde
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,554
- 8,583
KWA MABINTI
Mabinti wengi wanapokuwa kwenye uhusiano na mwanaume wanayempenda, na mwanaume huyo kumuhakikishia Kumuoa. Inapotokea mwanaume huyo kutaka Ngono (sex), uwezakano wa mabinti kukataa ni asilimia 0.0001 (0.0001 %) sawa na hakuna KABISA.
Kama akitokea amekataa basi huyo mwanaume hampendi, haamini kama kweli anamanisha kuwa naye, huyo mwanaume si king'ang'anizi kutaka wa sex au huwa hawana mazoea ya kukaa sehemu za faragha.
Nimekaa na mabinti na nimeona wana UDHAIFU mkubwa sana Katika kuwakatalia wanaume wanaowapenda kufanya Ngono.
Hivyo naomba nitumie nafasi hii kuwakumbusha mambo yafuatayo kuhusu mwanaume ..
Kama unampa ili umridhishe, basi kaa ukifahamu mwanaume si mtu wa kuridhika, mpe Leo, mpe kesho na bado atataka tena.
Kama unampa ili Asichepuke, basi unajidanganya..! Tamaa ya ngono na mwanaume ni kama mapacha wa tumbo moja. Kama Biblia ingeruhusu wanaume kuoa mke zaidi ya mmoja, basi ungejikuta wewe ni wa pili (bi mdogo), au ungetafutiwa mke mwenzako kama wewe ndio ulitangulia.
Ni Yesu tu aingilie kati na aushike moyo wake.
Kama unampa ili kudumisha Upendo.. Pole..! Mara Baada ya kuona uchi wako, upendo kwa wanaume wengi hupungua, maana unakuwa hauna JIPYA kwake. Angalia utaishia kuweka msiba usiokuwa na waombolezaji.
Kama unampa ili Akuoe, FIKIRI UPYA..! Chanzo cha ndoa si wewe Kuvua Sketi yako, ndoa ni Agano takatifu ambalo mwanzilishi wake ni Mungu mwenyewe. JITAMBUE, USIJIRAHISISHE...! Kama unampa ili ASIKUACHE, Labda nikuambie ni nani unayepaswa kumuogopa..!
Haina haja ya kuogopa kuachwa na mwanaume (asiye na Hofu ya Mungu) maana hana sehemu ya kukupeleka, bali muogope Mungu ambaye aliyeshika maisha yako na mwenye uwezo wa kukuhukumu Katika Jehanum ya MILELE, kwa dhambi hiyo ya Uzinzi unayoifanya.
Mabinti wengi Leo wameumizwa Katika Mapenzi, wanafanya ngono kuwaridhisha wanaume huku wakimkasirisha Mungu na wengine hata kuacha IMANI (Wokovu) kabisa.
Ujumbe huu ukasaidie kukutoa kwenye maangamizo ambayo Ibilisi ameendaa kwa ajili yako. "Ndoa bila kuvua Sketi INAWEZEKANA, UKIAMUA "
Mwanamke JITAMBUE, JITHAMINI na UJIAMINI.
YESU MBELE MWANAUME NYUMA
Warumi 8 : 31