Kwa wafugaji wa kuku wa kisasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa wafugaji wa kuku wa kisasa

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Mlachake, Oct 23, 2009.

 1. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2009
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,924
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Hey JF Members.

  Ee bwana kuna mtu anaweza kunipa msaada wa mchanganuo wa kufuga kuku. Naona soko la kuku ni kubwa sana. Hii ni biashara ambayo soko lake liko tayari. hotels, functions, vibanda vya chipss.. Yeyote mwenye idea naomba msaada please!

   
 2. Kisusi Mohammed

  Kisusi Mohammed JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2009
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 442
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Ni nzuri sana kama una eneo kubwa na halina magonjwa ya kuwadhuru kuku hao, kikubwa hapo ni unataka kufuga kuku wa aina gani, kiasi gani, na lengo la kuwafuga ni lipi?
   
 3. M

  Mwambashi Member

  #3
  Oct 23, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vipi business idea ya Coaster umeachana nayo???
   
 4. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2009
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,924
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  kaka nataka nianze na kuku 1,000. Actually I want that to be my reliable businees yaaani niachane na hizi ajira tunazo danganyana nazo
  thanks
   
 5. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2009
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,924
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Coaster mzee mfuko mdogo! hapo parefu kidogo mzee!!! 40m kwa mwajiriwa ni parefu kidogo
   
 6. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Fuga nguruwe wewee au fungua maduka manzese na Ubungo external kama upo ndarisalama.

  kuku kichefuchefu!! wakipata ugonjwa usiku, mpaka ukiamka huna hata wa ushahidi.
   
 7. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2009
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,924
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  mzee nimekusoma!!
   
 8. GP

  GP JF-Expert Member

  #8
  Oct 23, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  mkuu ulishawai kufuga kuku, japo 50??.
  maana kama ni wale broilers wakipata ugonjwa unaweza kupata presha, tena kama pesa ndo za FINCA, itakula kwako.
  bora kuku wa mayai, ila ndio hivyo uwe na mtaji mnene coz wanakula kwa miezi 5-6 ndo waanze kutaga mayai!
   
 9. safariwafungo

  safariwafungo Senior Member

  #9
  Oct 23, 2009
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 136
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  hapo sawa ila idea ya kusubili mpaka upate 40m hapana ilikuwa haivutii (there waz no growth orientation), swahiba karibu katika kada hii ya ujasiliamali hata hivyo si lazima uache kazi ndoo uingie kwani jambo zuri na la busara katika ujasiliamali ni kuhakikisha unamiliki mtandao ambao utakuwa unakuingizia fedha hata kama upo kwenye machela, mathalani wewe umeliona hilo na kutaka kujikita ktk kuku. Good idea, and for further info just ni PM.
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Oct 23, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kuku ni biashara nzuri sana lakini inabidi uwe mjanja,,,
  kwanza jifunze kutengeneza chakula cha kuku mwenyewe
  usiwe unanunua
  pili usiwe mbahili...hakikisha wanakula vizuri na madawa ya
  kupulizia kwenye mabanda unatumia
  anza na kuku 2000,
  good luck.
   
 11. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2009
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,556
  Likes Received: 1,324
  Trophy Points: 280
  Mkuu Karibu GMBD Consult ltd tunao uzoefu wa kutosha kuandaa michanganuo kutoa ushauri wa mradi wa kuku(broilers, layers, cross breeds n.k) pia tunao uzoefu wa kutosha kwenye kunenepesha ngombe(cattle fattening), ufugaji wa nguruwe n.k Tuna mifano mingi Korogwe 9 kilomtre kutoka Segera on the way to Moshi kuna shamba la nguruwe (400) na Kuku (6,000), Cattle fatterning in Mtibwa, e.t.c Pia tunao uzoefu wa kutosha kwenye animal feed processing(Dodoma - Mapusa Rajab), Mbezi Luis (M & M Food Procesor) e.t.c karibu sana. wasiliana nasi +255715 737302 au +255784 737302 ama kwa email info@gmconsultz.com pia tembelea website yetu www.gmconsultz.com
   
 12. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  well said, ni sawa kabisa, kujifunzia unaweza anza na cha kununua, ila faida hamna, tengeneza chakula mwenyewe, hakikisha usafi wa vyombo na banda, zuia ubichi bandani, hakikisha wakiumwa tu, watenge ukianza kusitasita ndo anavyosema huyo banda zima linakwisha.
  unaweza fuga kiasi chochote ila as a precaution nakushauri weka 200 banda moja kwa kuanzia ila pata ushauri wa vipimo per sq mita.
   
 13. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  asanteni sana na mie nimepata idea hapo kwenye hiyo Biashara
   
 14. k

  kisikichampingo Senior Member

  #14
  Nov 4, 2009
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 129
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Biashara ya kuku poa. Ila kwa wafanyakazi, nawapa ushauri wa bureeeeeeeee, msifuge kuku. Endeleeni tu na kazi zenu, jioni na weekend mkapumzika? Ila muwe na bajeti. Siyo mtu unapata laki 3, unataka kukimbizana na watu kama sisi-kwenye pombe upo, gari unataka, wanawake wewe.Headache za nini!?
   
 15. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #15
  Nov 4, 2009
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,924
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280


  Yaani umenichekesha kweli. Unajua umenigusa na hapo kwenye Red!!
  huo ndo ukweli!!!! lakini sisi wafanyakazi ndo tunajazaga Bar mida ya jioni.
   
 16. M

  Malila JF-Expert Member

  #16
  Nov 4, 2009
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,412
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Naam kama ni idea ziko lundo,shida iko kutekeleza idea husika.
   
 17. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #17
  Nov 17, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280

  Mlachake, una experience kwenye ufugaji kuku? kama huna basi,
  kuanza na kuku 1000 utakuja kulia!!! Na kama ni lazima uanze na kuku wengi,basi usiwe na mkono wa birika, kwamba usiwe bahiri!!

  Lazima utafute part time animal scientist ambae atakuwa mara kwa mara anakushauri suala zima la poutry management!!! aidha,usiwe bahiri, hususani kwenye feeding!!! poultry keeper wengi wana-collapse kv wanataka kubana matumizi kwenye chakula---manake wale jamaa wanafukia ile mbaya!!!

  in order to have productive layers or broilers, lazima kwenye masuala ya misosi wajiachie!!! and even more important, especially kama ni kuku wa mayai, tenga bajeti ya chakula pembeni na usiichezee kwa kitu kingine chochote kile, iwe pale ready for feeding!! Kama utapata mtaalamu, akakupa techinques za kutengeneza chakula itakuwa more wise kwako, kwavile feed cost ipo juu sana!!!

  BUT be careful, usi-opt tu kutengeneza chakula chao wakati feed chemistry haunayo!!! kama ni wa mayai, badala ya kuanza kutaga after 5 ro 6 months, wataanza after 8 months!!!Kama unazani hutaweza kufanya mixing vizuri, u better ukajilipue kwenye vyakula vya madukani ambavyo ni very expensive- but don' worry, bei hiyo haitakufanya upate hasara, but itapunguza faida!! na kitu kingine muhimu, don buy day old chicks mitaani, utakuja kulia!!!hizo ni few hints, but the project, inalipa wangu!!!

  Mengine yote, unaweza kushauriwa na animal scientist, but the first good strategy--- tafuta kijana ambae tayari ameajiriwa kwenye suala zima la utunzaji kuku--- mchomoe anakofanya kazi na mpe mshahara mkubwa zaidi, na mpangie room very close na yalipo mabanda yako!!! uki-opt kujenga annex ya kukaa poultry keeper, itakuwa ni more productive idea! wish u all the best
   
 18. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #18
  Nov 17, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mradi wa kuku ni mzuri haswa pale ambapo unakuwa na uzoefu wa jinsi ya kuwatunza na kufuatilia soko lake. Kwa mtizamo wangu naona kama unapendelea zaidi kuku wa nyama ambao kiasi fulani ni wagumu kuliko kuku wa mayai.

  Ni muhimu ukiangalia yafuatayo kwa ustawi wa kuku wa nyama.

  1. Kuwa na banda zuri lenye hewa ya kutosha pamoja na joto la kutosha (unaweza kupata vitabu kutoka kenye veterinary mbali mbali). Banda ni wastani wa mita 4 kwa 4 kwa kuku 200 wa nyama au 100 wa mayai. Hakikisha banda ni safi na umelipulizia dawa kabla ya kuingiza kuku (unaweza kutumia detto).

  2a. Kwa mtu unaeanza ni vizuri kutumia chakula cha kiwandani kwa ubora kwani mara nyingi vyakula vya kujitengenezea vinaweza kuwa ma upungufu au kutengeezwa katika mazingira yasiyo mazuri na hatimaye kuwa na matokeo duni. Kumbuka wanahitaji vakula veyenye virutubisho tofauti kulingana na umri (mfano starter & finisher kwa broiler)

  2b. Hakikisha wanapata chanjo ya newcastle wiki ya pili kwa kukuwapya utakaowaleta. Ni muhimu sana. Pia viatamini na madini kama utakavyoshauriwa na watalamu wa mifugo

  3a. Kama una uwezo mzuri ni vizuri kufuga kwa awamu. Mathalani wapishane kwa wiki 2, (yaani unaingiza kukuwapya kila baada ya wiki mbili). Hii inakupa nafasi nzuri haswa kupunguza gharama za malisho na nafasi, kwani kadri wanapokuwa ndivyo unavyoongeza nafasi ya banda. Kumbuka broiler.

  3b. Hakikisha kuna vyombo vya chakula na maji vya kutosha. Kuku wa nyama hawahitaji kwenda umbali mrefu kutafuta maji, na viwe na maji pamoja na chakula wakati wote.

  3c. Hudumia kuku wadogo kwanza, ndipo umalizie kwa wakubwa. Usafi ni muhimu sana. Kuwe na masodasti na hakikisha hakuna unyevu unyevu ili wasipate maambukizo ya magonjwa ya baridi.vifo vingi sana huweza kutokea. Ni vizuri ukahakikisha kuwa hakuna kuku wa kienyeji, kwani mara nyingi huwa chanzo cha magonjwa.

  4. Soko ndio kichaa kikubwa katika biashara ya kuku wa nyama, na faida yote hupotea baada ya kukomaa endapo soko linakosekana. Jiandae vyema kama ikiwezekana baada ya kufikisha uzito stahili (baada ya wiki 5-6) unawachinja wote na kuwauza au kuwahifandhi ndani ya jokofu na kuwauuza taratibu.

  Baada ya hapa unaweza kuangalia nafasi yako ya kukuwa na kuwa uzoefu kupanua biashara. Ushauri wa wataalamu ni muhimu sana kufanikisha malengo, ila pia kumbuka ubabaishaji ni mwingi Afrika!
   
 19. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #19
  Nov 17, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mkuu tazama hizo picha hapo chini;

  [​IMG]

  nilikuwa mmikoa ya kusini just three weeks ago, tutatembelea banda la mkulima mmoja na kuona jinsi alivyojikwamua kwa ufugaji kuku wa kienyeji. Alianza kufugia kwenye banda la kupikia, then sasa amejenga banda jipya, anafuga kwa kutumia njia bora zaidi kuku wale wale wa kienyeji. Kwa hivyo haihitaji kuanza na maelfu ya kuku, bali kidogo kadri unavyoweza, kikubwa ni kuhakikisha unawapatia huduma bora zikiwamo chakula na madawa....

  cheers..!
   

  Attached Files:

 20. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #20
  Nov 17, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mkuu naona shule hapo imetulia........!

  Lakini mbona mnazungumzia haya makuku ya kisasa tu? Je, ufuguja wa kitaalam wa kuku wa KIENYEJI unakuwaje? Kumbuka hawa nao wana soko zuri sana..........!
   
Loading...